Maalim Seif Atikisa Zanzibar, Mabomu Yarindima Kuwatawanya Wafuasi Wake

go CUF go SEIF hawa watu bila kuwakomalia watazidi kuwazalau
wazanzibar andamaneni,susieni shughuli za hawa watu mwisho haki itapatikana tu
we unajua madhara ya kuandamana. kwa sababu wewe upo Bara ndio unasema hivi. hata wazanzibar wanaokaa bara hawataki upuuzi huu. wewe ni nani kuwashurutisha hivi
 
We umeniita nyumbu mi nakuita fisi kwa tabia mlizonazo. Kama ni mabomu na risasi mpigeni Maalimu Seif sio mnamgwaya na kuwaonea wananchi wasio na hatia. Na ni kujitambua we ndiyo uelimike usishabikie uonevu na dhulma gamba wa kisiwandui
Nani kawakusanya hao unaowaita wananchi?
 
Maalim Seif angekusanya familia yake yoote ikae mbele na yeye atangulie ili mabomu yakipigwa nao waone uchungu wa majeraha. sio kutumia watoto wa wengine kwa faida zao za kisiasa. ni ujinga huu. zama zake zimeshapitwa na wakati. tangu 1992 ??? yupo tuu.yupo tuu. mmhh wajameni
Unafikiri watu wanasombwa kwenye mabasi? Wanaenda wenyewe..........

Kama kapitwa na wakati si ndiyo virahisi kumshinda? Mbona anawashinda?
 
Katika uchaguzi wa Oktoba 2015 ni nani hasa alishinda? Mwenyekiti wa CCM alisema kuwa Shein ndiye alishinda lakini kwa kuwa Jecha alishaufuta basi wakakubali tu hivo hivo.
Kama hakuna kukiuka sheria CUF wangeweza andika kitabu chenye matokeo kituo kwa kituo na jimbo kwa jimbo na kuweka jumla yote kama ilivyokuwa.
Kuhusiana na suala hili si vema kuishi kwa kuaminishwa tu ni lazima ukweli uanikwe kwa takwimu ili maridhiano yafanyike
Mshindi huwa anatangazwa na tume, wewe nae acha bangi.
 
Mtu kama wewe unaisaidiaje nchi ili ipate demokrasia ya kweli isiyo na dhulma ??!!. Halafu si ajabu ni aina ya wasomi makombi wasioisaidia nchi hii !!!
Mie nahitaji huduma bora za elimu, afya, maji na umeme ili niishi na mengine yaliyobaki ntajitafutia mwenyewe kwa kutumia akiri na nguvu alizonijaria Mungu. Sihitaji demokrasia ili niishi. Ni wapi utwambie ulikoshuhudia pana demokrasia ya kweli? msipoteze muda wenu kwa vitu ambavyo havipo na havitakaa viwepo hapa ulimwenguni
 


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliitikisa Zanzibar pale alipoanza ziara yake ya siku sita katika Wilaya ya Kaskazini A na kusababisha polisi kuwatawanya wafuasi wake kwa mabomu na risasi huku baadhi wakijeruhiwa.

Wakati wa ziara hiyo, shughuli za biashara zilisimama kwa muda ili kupisha ziara ya Maalim Seif na mamia ya wananchi wake kwa waume walimpokea na kumfuata kila alipoelekea.

Ulinzi uliimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wote wa ziara hiyo na vikosi vya ulinzi na usalama vilionekana vikipiga doria kila mahali.

Akiwa Kinyasini, Jimbo la Chaani ambako alifanya kikao cha ndani, wakazi wa eneo la Kivunge kwa mamia walianza kujikusanya katika maeneo ambako Maalim Seif alitarajiwa kutembelea huku wakijipanga barabarani kumsubiri kiongozi huyo. Hata hivyo, askari wenye silaha waliwatawanya.

Katika kuwatawanya, polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi hali iliyosababisha kizaazaa kwa takriban dakika 30 katika eneo la Kivunge kabla ya kurudi hali ya kawaida.

Baada ya hapo baadhi ya askari waliokuwa na silaha waliwazuia waandishi kusogelea eneo hilo wala kuwapiga picha majeruhi.

Mkazi wa Kivunge ambaye alidai ni miongoni mwa watu waliopatwa na mkasa huo, Omari Makame (32) alisema,“Sisi tumejipanga kwa heshima zote kumsubiri kiongozi wetu kipenzi cha Wazanzibari, tukiimba kwa furaha lakini ghafla tumepata kipigo na mabomu ya machozi, nini hiki kama siyo chuki na choyo kibaya.”

Mkazi mwingine, Haji Omar (27) alisema hata baada ya kuwajeruhi wenzao, polisi wali wakatalia kuwapa fomu za kwenda kupata matibabu na hata walipopelekwa hospitali ya Kivunge, polisi walifika na kuwachukua kwa nguvu.

“Wamekataa ushauri wa madaktari wa hapa kwamba wawapeleke Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja, lakini wamewachukua kwa nguvu wamekwenda nao Kituo cha Polisi Mkokotoni,”
alisema Omar.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi alikiri kuwapo kwa tukio hilo akibainisha kuwa yote hayo yanatokea kwa sababu kuna watu hawataki kufuata sheria, lakini akasema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassina Tawfik ndiye mwenye nafasi ya kufafanua zaidi.

Juhudi za kumpata Tawfik hazikufanikiwa ikielezwa na baadhi ya watendaji wa ofisi yake kuwa bosi wao hapatikani na hawakuwa na mawasiliano na yeye.

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa CUF, Pavu Juma Abdalla alifika katika Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kushuhudia majeruhi hao wakiwa mikononi mwa polisi.

Waliojeruhiwa ni Makame Abdalla Makame (28), mkazi wa Kivunge Bondeni na Shaame Juma Haji (45) mkazi wa Tumbatu Chwaka.

“Tunapigwa kwa sababu ya umma kuonyesha mapenzi kwa Maalim Seif, wangelikuja watu wa vyama vingine wasingelipigwa lakini ipo siku hawa jamaa wataheshimu haki zetu,” alisema mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Haji akisema baadhi ya majeruhi ni ndugu zake.

Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Salim Bimani ambaye alifika hospitali kuwaona majeruhi alisema:“Wenye mabomu na risasi wamewahujumu watu bure kwa sababu za chuki lakini yote hayo yana mwisho.”.

Bimani alisema Chama chake kinalaani kwa nguvu zote uonevu na hujuma hizo walizo tendewa wananchi wasiokuwa na hatia.

“Tunatumia pia kumbukumbu za hujuma hizi za leo kuongeza ushahidi wa kesi yetu tutakaouwasilisha ICC,”alisema Bimani.

Ziara yenyewe
Maalim Seif alianza ziara hiyo ya kwanza Unguja tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio aliosusa kushiriki katika eneo la Kinyasini, Chaani na kupokewa na mamia ya wafuasi wake ambao walikuwa wakiimba “rais! rais! rais!

Aliambatana na viongozi na watendaji wa CUF, akiwamo Naibu Katibu Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui; Bimani; Pavu Abdalla na Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi, Omar Ali Shehe.

Aliondoka Kinyansini kuelekea Gamba, Mkwajuni ambako mamia ya wananchi waliokuwa wakimshangilia walijipanga barabarani na walionekana kuongezeka kadri alivyoelekea Kaskazini na kukaribia Jimbo la Mkwajuni.

Baadaye Maalim Seif aliwahutubia wajumbe wa kamati mbalimbali za wilaya na majimbo akieleza kile alichosema ni mwelekeo wa kisiasa wa chama chake, Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Alisema dunia ilishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki na demokrasia visiwani humo, akidai kwamba pamoja na maonyo ya jamii mbalimbali za kitaifa na kimataifa, watawala waliamua kupora uamuzi wa mamlaka halali ya wananchi kupitia masanduku ya kura ya Oktoba 25, 2015.

“Angalieni watu hawa walivyokosa aibu, umma uliwakataa, mataifa yaliwakataa hata kuwanyima misaada lakini bado hawakuonyesha dalili za kujali kutokana na dhulma waliyotenda.

“Nasema hali hii haitupeleki pema sisi na Taifa kwa ujumla maana iliyoporwa ni haki ya umma na haiwezekani kuisamehe dhambi hii, hivyo mwishowe si mwema na dhuluma haiwezi kudumu kwa muda mrefu asilani, sasa kusema hivyo kuna ubaya gani?”

Hata hivyo, Mwangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU – EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini amesema atawasilisha ripoti kamili na mapendekezo ya umoja huo, kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana Alhamisi ijayo.

Maalim Seif aliwataka wananchi wote, kama walivyoikataa CCM kabla ya uchaguzi, wakati na baada ya kupiga kura Oktoba mwaka jana, kuunga mkono juhudi na mikakati ya CUF, ili kuhakikisha haki inapatikana, uamuzi wao unaheshimiwa, kwa masilahi ya nchi na Taifa kwa jumla.

Viongozi wa chama hicho Wilaya ya Kaskazini A, walimhakikishia Maalim Seif; “sisi tuko tayari kwa lolote, na naona siyo sisi pekee, kwa sasa kila mtu anaisoma namba, tutakuwa bega kwa bega mpaka haki yetu ipatikane,” alisema Makame Bakari, mmoja wa makatibu wa CUF
Mbona Wakikaa Barabarani "Kumsimamisha Mh. Magufuli" Wananchi hawapigwi mabomu? Hata mwanmuziki ambaye jina lake silikumbuki wanamsimamiaga bararani?
Mbona hawa hawakupigwa mabomu?
Na hawa Je Mbona hawatawanywi?
Najua Mtasema JPM ni Rais, Mbona wa Huyu hawakutawanywa?
Na huyu ambaye Jina lake silijui, mbona wake hawatawanywi?

Ila Wapinzani hata Kumzika Mawazo hawaruhusiwi. Ndiyo Tanzania tuliyonayo!
 
Wewe nyumbu tofautisha mkutano ya kuimarisha chama na uchochezi. Sasa mtu anawaambia wafuasi wake wasilipe kodi, wasitii serikali, wasitoe Huduma kwa wasio wanachama wa CUF, wasishiriki hata kuzikana! Huko ndio kuimarisha chama? Jitambue .
Civil disobedience is the active, professed refusal to obey certain laws, demands, and commands of a government, or of an occupying international power.
Mandela aliitwa Gaidi Kupinga Ukandamizaji wa Wachache, Tena yeye alichukua silaha kabisa. (Umkoto weziswe ie Mkuki wa Bwana) Na alisaidiwa Kijeshi na Mwl. Nyerere na Afrika kwa Ujumla. Kuna tofauti gani Zanzibar ya Leo na Afrika Kusini ya 1950s mpaka 1994 Niambieni. Au kuna Tofauti Gani Serikali ya Zanzibar ya Leo na Ile aliyoiangusha Karume?

Jecha na Waliomtuma Kukutokea Machafuko Zanzibar, Waombe yasitokee Machafuko Zanzibar, wasijidanganye ICC itatafuta Kiini na Wataoze jela.
 
wanaharakati wapo jela au wameuawa hizo kiki tu kutuliza raia wenye hasira wamuone sio msaliti
 
Shida kubwa maalim na wafuasi wake wanajidanganya eti 'The Hague' Kwani hao wazungu wanajitapa nao hawajui kwamba Seifu hawezi kupewa nchi! Wanalifahamu. Seifu aachane na hizi siasa za uhemko. Waarabu wanawadanganya sana. Zanzibar ndani ya Muungano varangati anololianzisha watu wake wataumia naye ataishia jela.
 
Mie nahitaji huduma bora za elimu, afya, maji na umeme ili niishi na mengine yaliyobaki ntajitafutia mwenyewe kwa kutumia akiri na nguvu alizonijaria Mungu. Sihitaji demokrasia ili niishi. Ni wapi utwambie ulikoshuhudia pana demokrasia ya kweli? msipoteze muda wenu kwa vitu ambavyo havipo na havitakaa viwepo hapa ulimwenguni

Poor Tz aina ya wakazi wako wanakuangusha, wamekata tamaa ni watumwa wa watawala wanaimba nyimbo za watawala zilizoshindwa kututoa MRISI na najuta kuwa raia sawa Rweye.

Huduma ulizosema kuwa ni kipaumbele chako (elimu, meme, afya na maji) hapa kwetu Tz ndiyo zipo chini kulinganisha na nchi zote zinazotuzunguka. Hapa kwetu tumefanikiwa kitu kimoja tu kama nacho ni cha kujivunia ni USWAHILI
 
Mshindi huwa anatangazwa na tume, wewe nae acha bangi.
sasa ukitaka maridhiano unafanyaje. si lazima uanike ukweli kwa figures! hapo uapata pa kuanzia. ww unaona hali ya Zanziba suluhisho ni mabomu tu!
 
Sefu anataka kujitoa kimasomaso kinafiki kwa damu za wazanzibar, kwani nani aliyewakataza kurudia kupiga kura? Aache uharibifu wa amani huyo yeye anapakwenda, hao washabiki pakiharibika wao ndio hawana pa kwenda na watajuta kumshabikia mnafiki.
Bado tu unatumia makalio kufikili?
 
WAPI BABU DUNI HAJI. nadhani mzew huyu ana busara zaidi ya Seif. alikua na slogan yake ya ndembendembee, kifo cha mendee, chaliiii miguu juu!
ni wakati muafaka chama cha CUF kichukuliwe naye sasa. mpeni retirement benefit Seif akapumzike. People need change, na mawazo mapya. hata mabadiliko ya sura ya mtu tuu nayo ni afya kwa wanachama
Unamjua Duni au unamsikia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom