Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amelalamikiwa kuwa amevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011kutokana na kitendo cha kuwafundisha wananchi mambo ya kuzingatiwa kuwemo katika mfumo wa Muungano.
Hayo yameelezwa na Chama cha National League for Democracy, (NLD) katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Haji Mussa.
Alisema kwamba Maalim Seif amevunja kifungu cha 18 cha sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba mwaka huu.
Alisema sheria hiyo inakataza mtu au taasisi yoyote kuhamasisha, kushawishi au kufanya kampeni zenye lengo la kuwataka wananchi kufuata matakwa ya chama au mtu katika mjadala wa katiba.
Khamis alisema Desemba 24, mwaka huu Maalim Seif aliwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mchakato wa katiba mpya wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kibandamaiti, Zanzibar.
Bahati mbaya, Maalim Seif hotuba yake imewashawishi watu kutenda mambo anayoyataka yeye, kitendo ambacho kinyume na sheria, alisema Khamis.
Alisema kuwa Zanzibar inaogozwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria, Maalim Seif akiwa kiongozi wa kitaifa hakupaswa kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mjadala wa katiba mpya ya Muungano.
Alisema kwamba chama chake kinaamini Wazanzibari wana akili timamu na wanazijua kero za muungano na wana uwezo wa kuzieleza bila ya kufundishwa na kiongozi au chama cha siasa.
Alisema katika mkutano wake Maalim Seif aliwataka wananchi kudai Zanzibar iwe na benki kuu yake, Jeshi la polisi, urais wa Muungano utokane na zamu na kuwe na usawa katika nafasi za ubalozi.
NLD inavishauri vyombo vya sheria kuifanyia kazi hutuba ya Maalim Seif na sheria ichukuwe mkondo wake, alisema Khamis.
Alisema wakati huu wa kuelekea mjadala wa katiba mpya siyo jambo la busara kwa vyama vya siasa au asasi za kiraia kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika katiba mpya.
SOURCE:NIPASHE