Maalim Seif amevunja sheria ya katiba mpya ashtakiwe

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amelalamikiwa kuwa amevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011kutokana na kitendo cha kuwafundisha wananchi mambo ya kuzingatiwa kuwemo katika mfumo wa Muungano.
Hayo yameelezwa na Chama cha National League for Democracy, (NLD) katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Haji Mussa.
Alisema kwamba Maalim Seif amevunja kifungu cha 18 cha sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba mwaka huu.

Alisema sheria hiyo inakataza mtu au taasisi yoyote kuhamasisha, kushawishi au kufanya kampeni zenye lengo la kuwataka wananchi kufuata matakwa ya chama au mtu katika mjadala wa katiba.

Khamis alisema Desemba 24, mwaka huu Maalim Seif aliwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mchakato wa katiba mpya wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kibandamaiti, Zanzibar.

“Bahati mbaya, Maalim Seif hotuba yake imewashawishi watu kutenda mambo anayoyataka yeye, kitendo ambacho kinyume na sheria,” alisema Khamis.
Alisema kuwa Zanzibar inaogozwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria, Maalim Seif akiwa kiongozi wa kitaifa hakupaswa kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mjadala wa katiba mpya ya Muungano.

Alisema kwamba chama chake kinaamini Wazanzibari wana akili timamu na wanazijua kero za muungano na wana uwezo wa kuzieleza bila ya kufundishwa na kiongozi au chama cha siasa.

Alisema katika mkutano wake Maalim Seif aliwataka wananchi kudai Zanzibar iwe na benki kuu yake, Jeshi la polisi, urais wa Muungano utokane na zamu na kuwe na usawa katika nafasi za ubalozi.
“NLD inavishauri vyombo vya sheria kuifanyia kazi hutuba ya Maalim Seif na sheria ichukuwe mkondo wake,” alisema Khamis.

Alisema wakati huu wa kuelekea mjadala wa katiba mpya siyo jambo la busara kwa vyama vya siasa au asasi za kiraia kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika katiba mpya.

SOURCE:NIPASHE
 
sasa hapa angekuwa ni kiongozi wa chadema amehutubia wananchi wa bara na kuwataka kudai serikali yao ya Tanganyika tayari angekuwa amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kwenda kinyume na sheria hii.Lakini kwa vile aliyesema ni mshirika wao watakaa kimya.
 
Maalim Seif ni official CCM.

Hata serikali ya mapinduzi Zanzibar inatekeleza sera za CCM kwahiyo Maalim naye anatekeleza sera za CCM.

CUF Zanzibar officially is DEAD.

Sioni namna polisi wanavyoweza kumkamata makamu wa rais wa CCM.
 
Wataalam wa sheria pigieni kelele hili jambo.Hata kama sheria ni mbovu lakini itende haki kwa yeyote anayeivunja.Sheria iwe msumeno.Watakapoanza kukamata viongozi wa chadema kwa kuvunja sheria hii basi watu wapaze sauti waseme waanze kumkamata kwanza Maalim Seif aliyechochea na kuwafudisha wazanzibar ya kusema kwenye katiba mpya
 
Hapo ndipo utagundua sheria hii iliwekwa mahususi kwa ajili ya watu fulani
 
Sheria kandamizi mno,itafika mahali tutatoa maoni tukiwa uvunguni kwa kutumia michrophone kwa hofu ya kukamatwa.
Katiba ya wananchi kwa nini tunatungiwa sheria ya kufungwa midomo?
 
Sheria kandamizi mno,itafika mahali tutatoa maoni tukiwa uvunguni kwa kutumia michrophone kwa hofu ya kukamatwa.
Katiba ya wananchi kwa nini tunatungiwa sheria ya kufungwa midomo?

Mkuu Buyegiboseba,
Sheria hii kandamizi iliwekwa kwa ajili ya watu fulani.Sasa Watanzania wanahoji kama haikuwekwa kwa ajili ya watu fulani akamatwe Maalim seif anayewafundisha wazanzibar cha kusema.Nakuapia angetamka hayo kiongozi yeyote wa Chadema angekuwa ameshakamatwa na kuswekwa lupango.
 
Hapo ndipo utagundua sheria hii iliwekwa mahususi kwa ajili ya watu fulani

Nakubaliana na wewe fmpiganaji,hii imewekwa kwa ajili ya viongozi wa chadema angekua mbowe/slaa/mnyika kafanya hivyo angekuta defender tano zipo chini ya jukwaa zinamsubili ashuke wamkamate
lakin seif ni mwana ccm mwenzao hapo hakuna kinachoendelea
 
Wako wapi wale waloiokuwa wanausifia mswada wa sheria hii wakati unajadiliwa bungeni wakati wenzao wametoka?
Tungependa waje waisifie sheria hii na m ambo yake.
 
Wako wapi wale waloiokuwa wanausifia mswada wa sheria hii wakati unajadiliwa bungeni wakati wenzao wametoka?
Tungependa waje waisifie sheria hii na m ambo yake.

mkuu Hume,Mungu hamfichi mnafiki kwani cuf waliusifu mno na kuitukana chadema kwa kila baya.Sasa Maalim Seif amekuwa mtu wa kwanza kuivunja sheria hii waziwazi
 
Hakamatwi mtu labda angesema mambo yanayoichukiza ruling party hapo angeshughulikiwa fasta.
 
Hakamatwi mtu labda angesema mambo yanayoichukiza ruling party hapo angeshughulikiwa fasta.
 
baba wa Taifa Nyerere alikuwa anaibadilisha katiba ya Tanzania kinyemela kivyake vyake tu bila ya kuwajulisha raia wa Tanzania mpaka akafikia kuliondoa jina la Tanganyika katika document zote za serikali!!!
sasa je Nyerere hakuvunja sheria za nchi????:nerd:
 
ni kifungu cha katiba mpya ya Zanzibar hiyo iliyobadilishwa na karume kwa ajili ya kulinda taifa la Zanzibar...imempa nguvu zaidi shujaa wa Zanzibar Seif, kuzidi kuwajenga wazanzibari kulinda taifa lao na mali zao:A S 465:
 
Back
Top Bottom