Maalim Seif akataa maamuzi ya ZEC, atoa tamko zito

Seif ni zuzu. Yaani mwenyekiti wa ZEC kaweka mpaka vifungu yeye anaishia kutoa porojo. hahahaha pole seif, labda usingeungana na fisadi lowasa ungeweza kupona. Pamoja na kuwa Zanzibar kunauonevu sana kwa watu wa pemba, ila na wewe seif unachuki sana kuhusu mapinduzi ndiyo maana hutakaa kuwa rais wa Zanzibar ktk maisha yako, kwani wenzako mapinduzi wanayaenzi wewe unabeza kana kwamba unataka kurudisha usultan.

sijawahi kuona mtu anaandika upuuzi huu toka nizaliwe
 
Wanandugu jisomeeni wenyewe!!!
attachment.php
attachment.php

Naona picha kama hazifunguki kwa wanao tumia app, ila kwa ufupi kazungumziaa yafuatayo.

1. Mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi

2. Anahoji kwa nini Makamu wa ZEC akamatwe na vikosi vya ulinzi na kupelekwa pasipojulikana

3.Kama uchaguzi umefutwa kutokana na dosari, basi hata wa rais wa jamhuri ufutwe kwani wote hao waliandikishwa kwenye daftari moja na kudumu zanzibar na walipiga kura kituo kimoja.

4. Hatambui maamuzi ya mwenyekiti wa ZEC kwani hakuna kikao cha tume kilichokaa kukubaliana na hilo na pia kusema kwamba hayo ni maamuzi binafsi ya mwenyekiti

5. Anaiomba umoja wa kitaifa na nchi jirani kuingilia kati

Hilo tamko ''zito'' lipo wapi sasa?
 
muungano uko chin ya ccm watalazimisha matokeo ili zenji iendelee kuwa chini ya ccm kwa ajili ya kuendeleza muungano.
Kama ni hivyo itamkwe bayana kwamba nchi ni ya chama kimoja. Kwanini kudhalilisha wagombea kumbe hata wakishinda hawatapewa
 
Alafu watu wanao kuchafua na kudhulumu wana nchi haki yao ni 3 tu kwanini tusiamuwe jambo
 
Seif ni zuzu. Yaani mwenyekiti wa ZEC kaweka mpaka vifungu yeye anaishia kutoa porojo. hahahaha pole seif, labda usingeungana na fisadi lowasa ungeweza kupona. Pamoja na kuwa Zanzibar kunauonevu sana kwa watu wa pemba, ila na wewe seif unachuki sana kuhusu mapinduzi ndiyo maana hutakaa kuwa rais wa Zanzibar ktk maisha yako, kwani wenzako mapinduzi wanayaenzi wewe unabeza kana kwamba unataka kurudisha usultan.
Haya sasa si mapenzi ni mahaba niue ==huoni, husikii wala huhisi UKWELI wa mambo. Hongera sana maana msingi wa hoja yake haionekani>>>>3.Kama uchaguzi umefutwa kutokana na dosari, basi hata wa rais wa jamhuri ufutwe kwani wote hao waliandikishwa kwenye daftari moja na kudumu zanzibar na walipiga kura kituo kimoja.
 
CCM hawakufuata sheria toka mwanzo.

na ndiyo hapo sheria ingetakiwa kuanza kuchukua mkondo wake kama ushahidi ungefikishwa kunakostahili badala ya kutafuta fujo ambayo siyo lazima itoe haki kwa anayestahili. wafikirie walemavu, wagonjwa,wazee na watoto. uyasikie kwa mwenzako yasikufike chumbani kwako mkuu.
 
Seif ni zuzu. Yaani mwenyekiti wa ZEC kaweka mpaka vifungu yeye anaishia kutoa porojo. hahahaha pole seif, labda usingeungana na fisadi lowasa ungeweza kupona. Pamoja na kuwa Zanzibar kunauonevu sana kwa watu wa pemba, ila na wewe seif unachuki sana kuhusu mapinduzi ndiyo maana hutakaa kuwa rais wa Zanzibar ktk maisha yako, kwani wenzako mapinduzi wanayaenzi wewe unabeza kana kwamba unataka kurudisha usultan.

acha upoyoyo wewe achieni nchi
 
Kama ni hivyo itamkwe bayana kwamba nchi ni ya chama kimoja. Kwanini kudhalilisha wagombea kumbe hata wakishinda hawatapewa

Yani ni kama umephotocopy maneno yangu niliyomwambia mtu mapema leo. Yani tunatumia mabilioni kununua BVR (ambazo faida yake sikuona maana siku ya kupiga kura hakuna sehemu walicheki fingerprint zangu)...mabilioni mengine kuandaa uchaguzi..watu wanapoteza mda wao kusimama masaa kwa masaa juani kwenye foleni kupiga kura..mwisho wa siku sauti yao haiheshimiki. Ni bota turudi kwenye chama kimoja..wachaguane wenyewe dodoma huko tujue nchi hii demokrasia hakuna.
 
Wakishinda upinzani uchaguzi unakuwa batili ,wakishinda watawala uchaguzi automatically unakuwa huru na wa haki.
Inasemekana Seif hajawahi shindwa uchaguzi, sema safari hii ameamua kukomaa khaki yake isinyang'anywe
 
Back
Top Bottom