Zanzibar ni nchi pekee duniani ambapo tume ya uchaguzi yenyewe inaona uchaguzi haukuwa huru na haki wakati vyama vya siasa, wananchi na hata waangalizi wa nje hawajaona wala kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Zanzibar ni nchi pekee duniani ambapo serikali inaandaa uchaguzi yenyewe, inausimamia yenyewe na inalalamika yenyewe kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Tafakari...........:majani7:
Seif kujitangazia matokeo ameanza uchaguzi huu? Mbona chaguzi za nyuma alikua anajitangazia na sheria hii hii ilikuwepo lakini hamkufuta uchaguzi? Kama kujitangazia matokeo imewakuna..mngemshtaki akalipe hiyo fine ya laki 5. Kilichotokea safari hii ni kwamba matokeo aliyotangaza yalienda sawasawa na yaliyokua ZEC. Ndio maana jeshi lilienda bwawani jana likawatimua waangalizi na waandishi wa habari. Na ndio maana mliamua kumshinikiza kibaraka wenu jecha mpaka akatangaza kufuta matokeo akiwa mafichoni na bila kushirikisha tume. Hatua ya kufuta uchaguzi ni kubwa na msingeichukua kama mlikua mnaenda kushinda huo uchaguzi.
Ni kweli mkuu,inaumiza sana kuwa mtanzania!!Tunavumilia kuwa watanzania tu.