Ukitaja mlipuko wa moto wa aina hiyo basi si kwa UBT pekee, fikiria na huku katikati ya jiji kwenye mlundikano wa majengo na miundo mbinu hafifu na uwingi wa wafanyakazi, sijui, labda, Mwenyezi Mungu atuepushie na maafa ya maji bahari ya Hindi.
I do support you completely. Tembelea mitaa ya karuta/Moro na India/Moro utashangaa. Kanakwamba haitoshi wahandisi wanaozijenga nyumba hizi ni wahindi na waafrika wenye elimu isiyo na shahada, pia hutumia mabango ya makontrakta wazoefu kwa gharama ya sh. 1,500,000/= kwa kila orofa inayopandishwa. Wenye mabango hawa ndio huchanganya udongo unaokwenda Chuo cha Aridhi kwa ajili ya kutathiminiwa. Ngoma inakuja pale Tibaijuka anapomwona mkaazi wa manzese na kumsahau jirani yake wa Posta & K'koo. Ambapo kwa ukaribu wa majengo vyumbani ni giza tupu. Au tunasubiri tume yakiisha tokea.