Bull Bucka
Member
- Oct 5, 2023
- 34
- 46
Pamoja na kwamba Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kimetengeneza ajira kwa watu wengi, lakini kuna jambo moja linaloendelea pale na linaonekana kufumbiwa macho na mamlaka husika. Jambo hilo ni utapeli.
Juzi nikiwa kwenye pitapita zangu, nikaona watu wamemzingira mama mmoja wa makamu. Mama huyo alikuwa akiangua kilio kwamba yeye alikuwa ameteremka kwenye daladala za Kinyerezi na wakati yupo kwenye daraja la juu la watembea kwa miguu linalounganisha upande wa Kituo cha Daladala cha Mbezi Louis na Magufuli Bus Terminal, alikutana na “ajenti” wa mabasi ya mikoani.
“Ajenti” yule alimshawishi mama yule na kumuuzia tiketi ya kwenda Kondoa na akamuandikia na kukabidhi kisha alipoingia ndani ya stendi akamwambia asubiri kwenye moja ya mabenchi mpaka basi lake litakapofika dakika ishirini baadaye.
Kutokea hapo hakumuona tena bwana yule. Na tiketi aliyokuwa amepewa haikuwa halali. Kwanza haikuwa tiketi halali ya gari aliloahidiwa, na pili gari hilo halifanyi safari za huko alipokuwa anaenda. Basi mama yule akawa amepoteza fedha zake.
Lakini hiyo haikuwa mara ya kwanza kusikia kuhusu watu kutapeliwa pale Magufuli. Kuna taarifa nyingi kuwa wale wanaojiita “maajenti” baadhi yao wako pale kwaajili ya kuchungulia fursa za kuwatapeli abiria wanaoenda mikoani. Inaelezwa kuwa kuna watu wengi safari zao zimekomea pale baada ya “kupigwa” na matapeli.
Ni sawa kwamba kinachoendelea kinatoa ajira kwa watu wengi, lakini kunaweza kuwa na utaratibu mzuri tu. Ni muhimu hao “maajenti” kama wanatambulika na makampuni ya usafirishaji wavae vitambulisho au sare. Kuna baadhi huwa wanavaa hivyo, lakini wengi wao hawana sare wala vitambulisho. Wanauza maneno tu. Tena wanawadaka wateja wanaposhuka tu kwenye daladala. Yaani kabla hujashuka unaona watu wamejaa mlangoni wanakuwania kama mpira.
Mamlaka ziliangalie hili na ziweke msimamo thabiti dhidi ya jambo hilo. Kila ajenti awe na kitambulisho na sare fulani inayomtambulisha, au namba kwenye kizibao au utaratibu mwingine wowote ule utakaofanya hawa watu watambulike kirahisi.
Lakini pia, hata wale maajenti ambao wanatambulika basi wasaidie kuwatambua wale wanaowaharibia kazi kazi yao.