Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Southern Giant

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
321
550
Habari ya uzima wana JF moja kwa moja niingie ktk mada bila ya kupoteza muda Je..? umewahi kuachwa na bus au kuchelewa kufika stendi kwaajili ya safari na ukakuta bus limesha ondoka kisha ukatumia bodaboda kufukuzia bus embu tueleze ilikuaje na gharama za kulifukuza zilikua kiasi gani.


Mimi niliachwa na bus enzi zile stendi ipo Ubungo nilikuwa naelekea Dodoma na bus ya Al-Saedy tiketi iliandikwa safari inaanza saa 4:00 asubuhi nafika pale majira ya saa 3:50 asubuhi naambiwa gari imeshaondoka muda si mrefu nilivurugwa ikabidi nichukue namba za konda akaniambia hawako mbali nichukue bodaboda wao wataenda mdogomdogo, chap nikavuta bodaboda nikaanza kuifukuzia nilikuja kuipata kibaha bodaboda ananiambia gharama yake nilibaki hoi ni bora ningeongezea kidogo nipande bus nyingine ikawa mzozo ila konda akalipa kwa kumuahidi nikifika Dodoma nitamlipa maana pale sikuwa na kitu, nilipofika Dodoma nikamkimbia sikumlipa kitu.


Je wewe ilishawahi kukutokea tueleze ilivyokua ...
 
Habari ya uzima wana JF moja kwa moja niingie ktk mada bila ya kupoteza muda Je..? umewahi kuachwa na bus au kuchelewa kufika stendi kwaajili ya safari na ukakuta bus limesha ondoka kisha ukatumia bodaboda kufukuzia bus embu tueleze ilikuaje na gharama za kulifukuza zilikua kiasi gani.


Mimi niliachwa na bus enzi zile stendi ipo ubungo nilikua naelekea dodoma na bus ya Al-Saedy tiketi iliandikwa safari inaanza saa 10:00 asubuhi nafika pale majira ya saa 3:50 asubuhi naambiwa gari imeshaondoka muda si mrefu nilivurugwa ikabidi nichukue namba za konda akaniambia hawako mbali nichukue bodaboda wao wataenda mdogomdogo, chap nikavuta bodaboda nikaanza kuifukuzia nilikuja kuipata kibaha bodaboda ananiambia gharama yake nilibaki hoi ni bora ningeongezea kidogo nipande bus nyengine ikawa mzozo ila konda akalipa kwa kumuahidi nikifika dodoma nitamlipa maana pale sikua na kitu, nilipofika dodoma nikamkimbia sikumlipa kitu.


Je wewe ilishawahi kukutokea tueleze ilivyokua ...
Mkuu, Ubungo kuna mabasi yalikuwa yanaruhusiwa kuondoka saa 10:00 asubuhi? Nakumbuka mabasi yalianza safari saa 12:00 asubuhi.
 
Gharama ya kufukuza basi kwa boda Bora ununue tiketi ingine panda basi la nyuma
Hiki kitu nlikitambua baada ya kuwa nimefanya makosa ila nilijifunza. Mwaka jana mwishoni nilikata tiketi mtandaoni ya kwenda Mwanza kwa bus la kampuni ya Happy Nation, tiketi ilionesha bus linatoka pale Shekilango saa tisa kamili.

Nimefika Shekilango saa tisa kasoro nikiwa na bodaboda naambiwa bus limetoka hapa sasa hivi, nikaanza kulikimbiza lakini silipati, nikaenda mpaka Mbezi silioni maana nilikuwa natizama plate number za mabus ya kampuni hiyo ninayopishana nayo.

Kufika Mbezi naambiwa limeondoka nikaanza kulifukuza tena ila nikawa nashangaa mbona magari ninayoyapita hayana hii plate number?

Nikaja kugundua baadae kuwa plate number ya kwenye tiketi haikuwa plate number ya basi liliondoka😂😂😂😂,nikapanda bus lingine la kampuni hiyo mpaka Moro ndio nikakutana na bus la Mwanza, ila mpaka napata hilo bus lao jingine lililonifikisha Moro nilikuwa nimeshatoboka kinoma.

Na tangu hiyo siku nimeagana na safari kwa kutumia kampuni ya HAPPY NATION hata bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom