Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 64
- 100
Wanasheria au Mawakili, Mahakimu na Majaji hawako juu ya Sheria bali pia wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na hata kushtakiwa kama mtu mwingine yeyote.
Makala hii inahusu jinsi ya kuwawajibisha waliotajwa hapo juu kwa makosa ya kimaadili tu.
1: TUANZE NA MAWAKILI BINAFSI
Sheria zinazosimamia maadili na mwenendo wa Mawakili wa kujitegemea nchini Tanzania (the legal framework governing the conduct of Advocates in Tanzania)
{i}: The Advocates Act [CAP. 341 R.E 2019]
{ii} The Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations, GN. No. 118, 2018.
{iii} The Advocates (Disciplinary and other Proceedings) Rules G.N. No. 120, 2018.
{iv} The Notaries Public and Commissioner for Oaths Act.
{v} Tanganyika Law Society Act na rules zake (though the rules are not enforceable yet-hazitumiki).
MAKOSA YA KITAALUMA KWA MAWAKILI BINAFSI (ADVOCATES PROFESSIONAL MISCONDUCTS).
(i) Kufanya kazi ya Uwakili wakati hauna vigezo/sifa, mfano haujawahi kuwa Wakili au ni Wakili lakini hauja renew leseni au umesimamishwa au kufutwa Uwakili (Unqualified practice). Section 41 ya Sheria ya Mawakili.
(ii) Lack of integrity (kukosa uadilifu). Kanuni ya 2 & 6 ya Kanuni za Maadili ya Mawakili (Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations, GN. No. 118, 2018).
(iii) Kutumia watu au mawakala kujipatia wateja (touting). Section 47 ya Sheria ya Mawakili na Regulation 128.
(iv) Kuingia makubaliano na mteja ya kulipana kesi ikiisha (Champerty / contingency fee). Regulation 81
(v) Uzembe. Regulation 14
{vi} Kushindwa kutunza siri za wateja (breach of confidentiality). Regulation 30.
(vii) Kusimamia kesi ambayo una maslahi (conflict of interests). Regulations 35, 45, 52, 53.
(viii) Kutoza wateja malipo zaidi au chini ya kiwango kilichowekwa na sheria (Undercutting or overcharging). Regulation 6(1)(l)
(ix) Kutumia vibaya pesa za mteja (misappropriation of clients money) unatakiwa uwe na akaunti mbili, ya Wakili na ya Mteja. Regulation 6(1)(f).
(x) Matangazo (advertisements). Regulation 127
(xi) Na kadhalika.
DISCIPLINARY AUTHORITIES (VYOMBO AU MAMLAKA ZINAZOWEZA KUWAWAJIBISHA MAWAKILI WA KUJITEGEMEA):
Nikisema disciplinary authority (mamlaka ya nidhamu) namaanisha mtu au mamlaka iliyopewa nguvu kisheria kuchukua hatua za nidhamu dhidi ya Mawakili.
Kwa Mawakili wa kujitegemea, wanawajibishwa na mamlaka zifuatazo.
{i} CHIEF JUSTICE (JAJI MKUU)
Ana Mamlaka ya kumuonya au kumsimamisha Wakili kwa muda fulani au kuamuru jina lake lifutwe kwenye Roll, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi.
Maamuzi ya Jaji Mkuu yanaweza kukatiwa rufaa Mahakama ya Rufani ambayo uamuzi wake utakua wa mwisho. Section 22(1) (2)(a) & (c)(ii) of the Advocates Act.
NB: Ukiondoa Jaji Mkuu, Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani hawana mamlaka hayo. Sheria iko Kimya. Ila Majaji wote wa Mahakama Kuu wanayo Mamlaka hiyo kama tutakavyoona hapo mbeleni.
{ii} HIGH COURT FULL BENCH (JOPO LA MAHAKAMA KUU) - Lina Mamlaka ya kumuonya au kumsimamisha Wakili kwa muda fulani au kuamuru jina lake lifutwe kwenye Roll, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi. Maamuzi ya Jopo hili hukatiwa rufaa kwenye Kamati (ya Maadili) ya Mawakili (Sio Mahakama ya Rufani). Section 22(2)(a) & (c)(i).
{iii} JUDGE OF THE HIGH COURT (JAJI WA MAHAKAMA KUU) - Ana mamlaka ya kumsimamisha Wakili kwa muda, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi, na kisha kulipeleka suala husika kwenye JOPO LA MAHAKAMA Kuu ambayo itathibitisha, kubadilisha au kutengua uamuzi huo. Maamuzi ya Jopo la Mahakama Kuu hukatiwa rufaa kwenye Kamati ya Mawakili.
-Ina maana Jaji akikusimamisha Uwakili, huwezi kukata rufaa moja kwa moja kwenda kwenye Kamati ya Mawakili au popote kabla ya jopo la Mahakama Kuu kuamua. Section 22(2)(b) ya Sheria ya Mawakili.
Zingatia: Majaji wanamwajibisha Wakili kama akionesha utovu wa nidhamu Mahakamani wakati kesi inaendelea. Lakini kama ni huko nje ya Mahakama, mamlaka hayo imeachiwa Kamati ya Mawakili.
{iv} ADVOCATES COMMITTEE (KAMATI YA MAWAKILI). Wengine wanaiita Kamati ya Maadili ya Mawakili.
Zamani Kamati ilikuwa moja tu nchi nzima lakini kufuatia marekebisho ya Sheria ya mwaka 2021, (the Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3), Act 2021, Act no. 5), sheria imeanzisha Kamati za Maadili za Mawakili kila Mkoa ili kurahisisha upatikanaji haki na kumwezesha mwananchi anayemlalamikia Wakili kwa ukiukaji wa maadili kushughulikia tatizo lake katika ngazi ya Mkoa badala ya kusafiri kuifuata Kamati ya Maadili katika ngazi ya taifa.
Hivyo kwa sasa tuna.
(a) Kamati ya maadili ya Mawakili katika ngazi ya taifa (National Advocates Committee) na
(b) Kamati za Maadili za Mawakili kwa ngazi za Mikoa.
{a} NATIONAL ADVOCATES COMMITTEE (KAMATI YA MAWAKILI NGAZI YA TAIFA): Hiki ndio chombo kikuu cha kuwawajibisha Mawakili nchini Tanzania.
Zamani Kamati hii ilikuwa inapokea na kusikiliza kwa mara ya kwanza malalamiko yote yanayohusu Mawakili kama vile utovu wa nidhamu, uzembe n.k. Lakini sasa hivi mambo hayo yote yanaanzia mikoani. Hivyo, National Advocates Committee inapokea na kusikiliza rufaa zinazotoka huko mikoani na zinazotoka Mahakama Kuu. (Haina original jurisdiction)
Maamuzi yake yanakatiwa rufaa Mahakama Kuu ambapo husikilizwa na jopo la Majaji wasiopungua watatu. Rejea section 24A(1) & (4) ya Sheria ya Mawakili.
{b} KAMATI ZA MAADILI ZA MAWAKILI KWA NGAZI YA MIKOA. Imeanzishwa chini ya kifungu cha 4A(1) cha Sheria ya Mawakili, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2021. Maamuzi yake hukatiwa rufaa National Advocates Committee (Kamati ya Mawakili ngazi ya Taifa)
Haina mamlaka kumvua mtu Uwakili. Kama adhabu husika ni kufuta jina la Wakili kwenye orodha ya Mawakili, itabidi wapeleke uamuzi na mapendekezo kwenye Kamati ya Mawakili ngazi ya Taifa (National Advocates Committee). Rejea Section 4B(3) ya Sheria ya Mawakili.
MAWAKILI WA SERIKALI (LAWYERS IN PUBLIC SERVICE)
Mawakili wa Serikali ni wanasheria walioajiriwa Serikalini.
SHERIA ZINAZOSIMAMIA MAADILI NA MWENENDO WA MAWAKILI WA SERIKALI (LEGAL FRAMEWORK REGULATING THE CONDUCT OF LAWYERS IN PUBLIC SERVICE).
Kwa upande wa Mawakili wa Serikali, ukitaka kujua maadili yao na vyombo vinavyohusika kuwawajibisha soma sheria zifuatazo (Laws Governing Ethics of State Attorneys and Lawyers in Public Service).
{i} The Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019].
{ii}The Code of Ethics and Professional Conduct for Law Officers, State Attorneys and Legal Officers.
{iii} The National Prosecutions Service Act [CAP. 430 R.E 2019]
{iv} The Attorney General (Discharge of Duties) Guidelines for Practising State Attorneys and Law Officers, 2020.
{v} The Advocates Act na regulations zake etc.
Pamoja na sheria tajwa hapo juu, kwa kuwa Mawakili wa Serikali ni watumishi wa Umma, wanatakiwa pia kuzingatia Kanuni na maadili ya utumishi wa umma kama yalivyoainishwa katika sheria za utumishi wa umma zifuatazo;
{vi} Public Service Act, CAP 298, R.E 2002
{vii} Public Service Regulations, 2003
{viii} Public Service Disciplinary Code of Good Practice, G.N 53/2007
{ix} Standing Orders for the Public service, 2009 (GN 493/2009.
{x} Public Leadership Code of Ethics [CAP 398 R.E 2002]
{xi} The Code of Ethics and Conduct for the Public Service.
MAKOSA YA KINIDHAMU KWA MAWAKILI WA SERIKALI (WHAT AMOUNTS TO BREACH OF DISCIPLINE BY STATE ATTORNEYS).
1: Kufanya kazi ya Uwakili (wa Serikali) wakati huna vigezo (unqualified practice). Section 16 of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019].
2: Kwenda Mahakamani kama Wakili wa kujitegemea au kufanya kazi za Uwakili binafsi. Section 17(A) of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019.
3: Kufanya kazi zingine nje ya mipaka ya Wizara au idara husika.
4: Kukosa uadilifu.
5: Kuvujisha siri (breach of confidentiality) n.k.
MAMLAKA ZINAZOSHUGHULIKIA MAADILI YA MAWAKILI WA SERIKALI (DISCIPLINARY AUTHORITIES FOR LAWYERS IN PUBLIC SERVICE).
1: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (ATTORNEY GENERAL). Anasimamia nidhamu ya Mawakili wa Serikali wanaofanya kazi Kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Section 7(1)(e) of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019] na Order 4(l) ya Amri ya Mabadiliko ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (The Office of the Attorney General (Re-structure) Order, G.N. No. 48, 2018).
2: MWANASHERIA MKUU MSAIDIZI (DEPUTY ATTORNEY GENERAL). Anasimamia nidhamu ya Mawakili wa Serikali wanaofanya kazi Kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Section 7(1)(e) of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019] na Order 6(2)e ya Amri ya Mabadiliko ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (the Office of the Attorney General (Re-structure) Order, G.N. No. 48, 2018).
3: SOLICITOR GENERALI (WAKILI MKUU WA SERIKALI) anasimamia nidhamu ya wale Mawakili wa Serikali wanaofanya kazi kwenye Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Soma Order 4(1)(j) ya the Office of the Solicitor General (Establishment) Order, GN. No. 50, 2018.
4: THE DEPUTY SOLICITOR GENERAL (WAKILI MKUU MSAIDIZI). Anasimamia nidhamu ya wale Mawakili wa Serikali wanaofanya kazi Kwenye Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Soma Order 6(2) ya the Office of the Solicitor General (Establishment) Order, GN. No. 50, 2018.
5: OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA (NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES) au tuseme Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (Director of Public Prosecutions - DPP). Anasimamia nidhamu ya wale Mawakili wa Serikali wanaofaniya kazi Kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Order 4(i) of of the National Prosecutions Services (Establishment) Order, GN No. 49, 2018.
6: MWENDESHA MASHTAKA MSAIDIZI (DEPUTY DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTION). Anasimamia nidhamu ya wale Mawakili wa Serikali wanaofanya kazi Kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (National Prosecutions Services). Section 5(2), 9(1)(h) ya National Prosecutions Service Act [CAP. 430 R.E. 2022] na Order 6(2) of the National Prosecutions Services (Establishment) Order, GN No. 49, 2018.
7: WAAJIRI KWENYE WIZARA AU MAMLAKA HUSIKA (respective employers in the ministries, local government authorities, independent departments, agencies, public corporations and parastatal organizations. Section 21(3) of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019].
8: KAMATI YA MAWAKILI (ADVOCATES COMMITTEE). Section 27(3) of the Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act [CAP. 268 R.E. 2019]
Lakini kwa kuwa Mawakili wa Serikali ni watumishi wa Umma, hivyo wako chini ya Sheria ya utumishi wa Umma (Public Service Act) na kanuni zake, hivyo wanawajibishwa pia na mamlaka zifuatazo ambazo zinasimamia maadili ya watumishi wa umma.
9: MHESHIMIWA RAIS (PRESIDENT).
Ana mamlaka ya kumuondoa mtumishi wa umma lakini pia anasikiliza rufaa za watumishi wa umma ambapo maamuzi yake ni ya mwisho. Section 24 & 25 of the Public Service Act.
10: KATIBU MKUU (CHIEF SECRETARY): Anasimamia maadili ya watumishi wa umma walioteuliwa na Rais. Section 4(3)(d), 4(4), 25(1) of the Public Service Act.
11: TUME YA UTUMISHI WA UMMA (PUBLIC SERVICE COMMISSION).
Inapokea na kusikiliza rufaa za watumishi wa umma. Section 10(1)(d) of the Public Service Act.
12: WAZIRI ANAYEHUSIKA NA SERIKALI ZA MITAA (MINISTER RESPONSIBLE FOR LOCAL GOVERNMENT). Anasimamia Maadili ya serikali za mitaa. Section 5(1)(a)(ii)
13: WATENDAJI AU CEO (CHIEF EXECUTIVE OFFICERS) WA KILA WIZARA, IDARA, MKOA AU SERIKALI ZA MITAA. Wanasimamia maadili ya watumishi wa umma ambao sio wateule wa Rais, wanaofanya kazi chini ya idara au vitengo vyao. Section 6(1)(b) of the Public Service Act.
MAJAJI NA MAHAKIMU
Disciplinary Authorities (vyombo au Mamlaka zinazoweza kuwawajibisha Mahakimu na Majaji).
Kwa upande wa Mahakimu na Majaji, ukitaka kujua maadili yao na vyombo vinavyohusika kuwawajibisha soma sheria zifuatazo.
1: The Judiciary Administration Act No. 4 of 2011.
2: The Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania.
Kwa ufafanuzi zaidi tukutane kwenye makala nyingine.
------MWISHO-------
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke 0754575246 WhatsApp).
zakariamaseke@gmail.com
Natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili.
Unaruhusiwa kushare lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.