Lutheran Primary School Moshi ilivyokuwa 1958 na sasa

Gold...
Ikiwa wewe huamini niliyoandika hakuna neno.

Ila kaa ukijua nimesimama kwingi nikikieleza kitabu hiki.

Elewa pia review ya kitabu imechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Naamini unaijua University of Cambridge.
Haya yote zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Wewe unaniuliza maswali ya kitabu cha Abdul Sykes leo.
Kuchapwa Cambridge Journal of History siyo hoja. Wao kazi yao ni kuchapisha mawazo kwa nia njema. Unless umeonyesha kupotoka ndiyo wanaweza kukatalia. Kwa vile unachoandika huwa ni opinion na siyo historia, hawana ubavu wa kuikataa opinion yako. Opinion siyo fact.
 
Mwaka 1958 wengine tumeshamaliza Primary School (1 - 4) tuko Middle School darasa la sita! Naomba mtuamini tukikosoa historia isimuliwayo na vijana.
Lo! Umekula chumvi. Mimi naanza shule wewe uko mwaka wa mwisho (lower primary school), ila sema tu, mimi nilianza shule zee zima la miaka 12. Enzi zetu unamaliza la nne kama ni mvulana unauoa, kama msichana unaolewa.
 
Gold...
Kinachokuudhi ni mimi kuandika historia iliyosahihisha historia iliyozoeleka.

Kwa nini hujiulizi kitu gani kiliwafanya waandhishi kuandika historia isiyo ya kweli?
Sidhani imeandikwa historia isiyo kweli. Mitazamo na hisia za waandishi ndiyo zinaleta tofauti. Kuna mahali nimesema unayoyandika wewe ni opinion. Na kwa opinion yako unasema historia imepindwa. Kwangu mimi naona haikupindwa. Waandioshi wa huko nyuma wameongelea juu ya TAA umuhimu wa TAA katika swala la uhuru. Hao wote unaowasema hawakuonekana katika historia, wote wapo. Bibi Titi Mohamed amejaa katika historia ya Tanganyika. Wapo wake na Sykes, Kitwana Kondo, John Rupia n.k. katika hiyo historira.

Ni kweli baada ya kuanzishwa TANU, umaarufu wa TAA na na nafasi yake katika kutetea haki za mwafrika na kuanzisha vuguvugu la uhuru ulianza kufifia. Lakini hilo halikufanyika kidini, kwa sababu TANU iliondoka na waasisi wa TAAA na wakawa waasisi wa TANU. Utakubaliana na mimi kuwa hata CCM imekuwa ni kama umeaua umaarufu wa TANU. Hii ni pamoja pia kusahaulika waasisi wa TANU. Baada ya kuanzishwa CCM vile vyama vilivyokuwepo ni kama vimesahaulika, na vinaonekana katika maandiko machache tu. Kusahaulika au kurudi nyuma umaarufu wa TAA, TANU, Afro Shiraz Party n.k. siyo kwa sababu ya dinio za wanachama bali kuendana na wakati, yaliyopita huchukuwa back door na kuwaachia wenye hizo fani kutafiti na kuandika. Kwa hiyo na wewe kwa upande mmoja una haki kutafiti na kuandika maoni yako, lakini tatizo lako ni pake unapotaka kuyafanya maoini yako kuwa fact. Fact ambayo unadhani TAA au hata TANU na viongozi wake hawatajwi kwa sababu za kidini. Mpaka leo hii utaona kila chama kimnaongelea juu ya baba wa taifa. Miaka 100 ijayo baba wa taifa labda hatatamkwa bungeni mara moja kwa kwa mwaka. Lakini hiyo haitakuwa na maana siyo muhimu au wamemsahau. Lakini wenye interest kama wewe wanaweza kutafiti na kuandika juu yake.
 
LUTHERAN PRIMARY SCHOOL MOSHI KAMA ILIVYOKUWA 1950s NA SASA

Nilianza darasa la kwanza mwaka wa 1958 kwenye jengo hilo hapo chini lililokuwa ni Kanisa la Kilutheri.

Baada ya miaka mingi nilifika Moshi kuangalia pale nilipoanza shule.

Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 20 December, 1986 na nikapiga picha hiyo ya kwanza nimesimama kwenye mlango wa kuingilia kanisani ambako ndiko nilipoanza kusoma.

Ile piano ambayo Mwalimu Paul alikuwa akipiga na sisi wanafunzi tukiimba ''hyms,'' ilikuwa pale pale ilipokuwa mwaka wa 1958.

Piano ile ilirejesha kwangu kumbukumbu nyingi pamoja na nyimbo nilizojifunza pale na zote nikizikumbuka kama vile niliziimba jana ---''Damu ya Kondoo,''Ni Nani Aliyetuumba ni Mungu Mwenyewe,'' ''Ewe Mwezi ni Rafiki Yangu,'' ''Tunamsifu Baba Marehemu Kingi George.''

Kuzunguka kanisa kulikuwa na bustani nzuri ya maua ya rangi tofauti na kulikuwa na ukoka uliopandwa kiasi huoni ardhi.

Mwalimu Paul alikuwa mtu mzima na ndiye aliyeniandikisha shule nikiwa na miaka sita.

Alikuwa siku zote akivaa pama hata darasani.

Alikuwa akitufundisha kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni.

Miaka miwili tu mama yangu alikuwa amefariki na ndiyo sababu ya mimi kuchukuliwa na mama yangu mdogo na kujanae Moshi alipokuwa akifanya kazi katika Nursing Home ya Mgiriki Dr. Georgedis nianze shule.

Hospitali hii ilikuwa makhsusi kwa Wazungu tu.

Kwa kuwa Mwalimu Paul alikuwa akitufunza kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni nilikuwa na kawaida ya kukaa kwenye ukoka kwenye bustani peke yangu na wakati mwingine nikilala chali kuangalia juu mawinguni nikitegemea kumuona mama yangu.

Namkumbuka mwanafunzi mwenzangu umri sawa na mimi akiitwa Njuguna wakati mwingine akija kukaa na mimi pale bustanini.

Njuguna alikuwa mzuri na nikipenda sana awe karibu yangu.

Miaka ilisogea na pamoja tukawa wakubwa kiasi miaka miaka 12 hivi.

Siku moja kwenye fete alipewa microphone akaambiwa aimbe nyimbo yoyote aitakayo.

Junguna akaimba, "Oh Carol," ya Neil Sedaka kwa ustadi mkubwa sana.

Kila niisikiapo nyimbo hii humkumbuka Njuguna.

Njuguna ametangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.

Namkumbuka Hidaya yeye tukifuatana pamoja kwenda shule.

Siku moja nikauliza kama Hidaya yuko mjini.

Nikafahamishwa kuwa amefariki miezi michache iliyopita.

Alikuwa nurse Hospitali ya Mawenzi.

Majonzi yalinijia ingawa tulipoachana sote tulikuwa watoto wadogo labda wa miaka 10.

Miaka imekwenda wapi?

Picha hiyo ya pili nimeipiga tarehe kama hii ya leo mwaka jana nikapiga sehemu ile niliyosimama mwaka wa 1986 miaka 36 iliyopita.

Kanisa ambalo ndani yake ndiko lilipokuwa darasa langu la kwanza pamebadilika sana kama inavyoonekana kwenye picha.

View attachment 2163433
Hongera sana ndugu au nikuite baba,pole kwa kufiwa na mzazi
Ila nafurahi upo mzima wa afya baba yangu kazaliwa 1955 kafariki 2002 nikiwa na miaka 6.
 
Kama lugha huelewi, bora tu mwambie MS ajikite kwenye masuala mapana ya Kitaifa hivi sasa, badala ya hadithi na simulizi za Wajomba zake marehemu.
Sema usemavyo,ni ujuha na utumwa kuona dahari kutumia lugha ngeni hasa ya mkoloni na bwana wa biashara ya utumwa
 
Sidhani imeandikwa historia isiyo kweli. Mitazamo na hisia za waandishi ndiyo zinaleta tofauti. Kuna mahali nimesema unayoyandika wewe ni opinion. Na kwa opinion yako unasema historia imepindwa. Kwangu mimi naona haikupindwa. Waandioshi wa huko nyuma wameongelea juu ya TAA umuhimu wa TAA katika swala la uhuru. Hao wote unaowasema hawakuonekana katika historia, wote wapo. Bibi Titi Mohamed amejaa katika historia ya Tanganyika. Wapo wake na Sykes, Kitwana Kondo, John Rupia n.k. katika hiyo historira.

Ni kweli baada ya kuanzishwa TANU, umaarufu wa TAA na na nafasi yake katika kutetea haki za mwafrika na kuanzisha vuguvugu la uhuru ulianza kufifia. Lakini hilo halikufanyika kidini, kwa sababu TANU iliondoka na waasisi wa TAAA na wakawa waasisi wa TANU. Utakubaliana na mimi kuwa hata CCM imekuwa ni kama umeaua umaarufu wa TANU. Hii ni pamoja pia kusahaulika waasisi wa TANU. Baada ya kuanzishwa CCM vile vyama vilivyokuwepo ni kama vimesahaulika, na vinaonekana katika maandiko machache tu. Kusahaulika au kurudi nyuma umaarufu wa TAA, TANU, Afro Shiraz Party n.k. siyo kwa sababu ya dinio za wanachama bali kuendana na wakati, yaliyopita huchukuwa back door na kuwaachia wenye hizo fani kutafiti na kuandika. Kwa hiyo na wewe kwa upande mmoja una haki kutafiti na kuandika maoni yako, lakini tatizo lako ni pake unapotaka kuyafanya maoini yako kuwa fact. Fact ambayo unadhani TAA au hata TANU na viongozi wake hawatajwi kwa sababu za kidini. Mpaka leo hii utaona kila chama kimnaongelea juu ya baba wa taifa. Miaka 100 ijayo baba wa taifa labda hatatamkwa bungeni mara moja kwa kwa mwaka. Lakini hiyo haitakuwa na maana siyo muhimu au wamemsahau. Lakini wenye interest kama wewe wanaweza kutafiti na kuandika juu yake.
Wacha porojo,mashuleni tumefundishwa Uhuru ni nyerere na nyerere ni Uhuru,Nani aliwajua akina Sykes huko shule ya msingi na o level!?..ndiyo maana kitabu kilipotokea kila mtu alishangaa
 
Kuchapwa Cambridge Journal of History siyo hoja. Wao kazi yao ni kuchapisha mawazo kwa nia njema. Unless umeonyesha kupotoka ndiyo wanaweza kukatalia. Kwa vile unachoandika huwa ni opinion na siyo historia, hawana ubavu wa kuikataa opinion yako. Opinion siyo fact.
Ksk,
Hakika umesema kweli.

Lakini unafikaje hadi unachapwa Cambridge Journal of African History?
 
Wacha porojo,mashuleni tumefundishwa Uhuru ni nyerere na nyerere ni Uhuru,Nani aliwajua akina Sykes huko shule ya msingi na o level!?..ndiyo maana kitabu kilipotokea kila mtu alishangaa
Ina...
Mshangao ule ulikuwa wa mshtuko.

Wanajiuliza mbona historia hii hatukosomeshwa?

Hili ndilo lililofanya kitabu kipendeke kama unavyoona hapa tuko katika mjadala mkali.

Kitabu kinakimbilia toleo la tano.
Huu ni mwaka wa 24 kitabu kinajadiliwa kama kimechapwa jana.

Unakijua kitabu chochote wa mfano huu?
 
Mkaza...
Walijaribu kabla yangu kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika bila ya kumtaja Abdul Sykes wala baba yake katika kuundwa kwa African Association na TANU.
Matokeo yake nadhani sote tunayajua.
Na Mwalim Cecil Matola, V.Kyaruzi , C. Mtamila na wengine
Kwahiyo Historia haikamiliki bila kuwataja Abdul Sykes na Baba yake!
Tumeandika historia mpya si ya TANU tu bali hata historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Historia ya Mwl Nyerere umeieleza kwa ''cherry-pick'' unapoeleza jambola ''Wazee wako'' .

Nyerere anaonekana zaidi anapopewa sh 200 na Mshume Kiyate akanunue mboga !

Pale anapokaaingiwa mayai nyumbani kwa Abdul Sykes n.k

Hutamsoma Nyerere kama katibu wa Tawi la Tabora, wala kumsikia kama mtu aliyeleta mapinduzi ndania ya siasa za Dar es Salaam kwa kukiwekea chama misingi wa Katiba na kukisambaza majimboni kwa nguvu kuliko ilivyowahi kutokea.

Role ya Nyerere ilikuwa transformation ya chama kutoka katika 'jamii au Familia'' kuwa chama cha siasa. Huo ndio msingi wa kuandika katiba ya chama.

Nyerere alibaini kukiacha chama kilivyo kutatokea matatizo kitakapopanuka zaidi.

Matatizo ni yale aliyoeleza Mohamed Said katika kitabu chake yakimhusisha Abdul Sykes na wahuni walipovamia Ofisi na kubagaza baba zao.

Ile ilikuwa ''red flag'' ya chama kukosa muongozo.

Uchaguzi wa Arnatouglo unadhahirisha kwamba chama kilikuwa katika ''transition'' iliyosaidia sana transformation kwenda TANU na ku define siasa za nchi hii hadi leo.

Kwako Nyerere ni daraja la kumpamba Abdul Sykes, lakini historia inasahihisha hilo ndio maana Nyerere hayupo miaka 20 lakini ''anajibu'' hoja zako kutoka alipo! hahitaji kuandikiwa kitabu kuna uhitaji wa vitabu vinavyomhusu.
 
Nguruvi...
Hapana inaelekea huna taarifa nini kilitokea baada ya Prof. Haroub Othman kusoma kitabu changu.

Prof. Haroub alishtuka na akafanya mazungumzo na Nyerere na akamuomba aandike kumbukumbu zake kwani kitabu cha Abdul Sykes kimekuja na mambo mengi ambayo bahati mbaya hayakuwa yanafahamika na hata yeye kwake yalikuwa mageni.

Hiki ndicho chanzo cha kuandikwa Nyerere Biography.

Hayo mengine sioni haja ya kuyasemea.
Una haki ya kuamini upendavyo.

Niliyoandika siwezi kuyabadili yapo yanasomwa sasa mwaka wa 24.
 
Ina...
Mshangao ule ulikuwa wa mshtuko.

Wanajiuliza mbona historia hii hatukosomeshwa?

Hili ndilo lililofanya kitabu kipendeke kama unavyoona hapa tuko katika mjadala mkali.

Kitabu kinakimbilia toleo la tano.
Huu ni mwaka wa 24 kitabu kinajadiliwa kama kimechapwa jana.

Unakijua kitabu chochote wa mfano huu?
kwa.kweli hakika mshangao ulionishika na hamu ya kusoma kitabu hiki ilihal ndio kwanza nipo.kidato cha tano nilishangaa sana.miaka ming imepita .
 
Na Mwalim Cecil Matola, V.Kyaruzi , C. Mtamila na wengine
Kwahiyo Historia haikamiliki bila kuwataja Abdul Sykes na Baba yake!
Mkuu Nguruvi3, nilikuwa nimeng'atuka lakini umbeya wa Mohamed Said umeniamsha...

Katika historia ya uhuru huyo Abdul Sykes wake alikuwa nini na nani (what and who was he?) Katika historia ya TANU aliwahi kuwa nani zaidi ya kujaribu kujishindanisha eti na wa kuja, Mwalimu Nyerere kugombea uongozi? Je alipata kura ngapi?

Na hata baada ya kushindwa vibaya na Baba wa Taifa, alikuwa na wadhifa gani ndani ya TANU hadi tunapata uhuru mwaka 1961? Kumbuka mpwe wake, Mohamed Said, anakiri wengi wa wapiga kura walikuwa ni hao hao wazee wake.

Abdul Sykes hakuwahi hata siku moja kuwa kiongozi mkuu wa TAA wala TANU. Sifa pekee anayodaiwa kuwa nayo na mpwa wake, Mohamed Said, eti ni kuwa bingwa wa kutwaa uongozi kwa mateke na mangumi, are you kidding me?

Na hata baada ya matumizi ya mateke na mangumi, Abdul Sykes hakuweza kuchaguliwa kuwa kiongozi mkuu na badala yake akatafutwa wa kuja, Dr. Vedasto Kyaruzi kukiongoza chama cha TAA kabla ya kufanyiwa fitna na wakoloni kwa kupewa uhamisho!

Mohamed Said, nakushauri upumzike ule matunda ya umbeya uliyoueneza hadi huko kwa mabeberu halafu unajitapa wao kuzichapisha hadithi zako! Kwa nini wasizichapishe? Toka lini walijitoa katika kuchapisha simulizi za watu kama wewe?
 
Mag...
Mbona mimi naandika bila ya kutukana?
Huu ni mjadala tu.

Historia iliandikwa lakini mimi nikaona ina makosa nimenyanyua kalamu kusahihisha.
Mbona hili jambo limekukasirisha kiasi hiki?

Abdul Sykes mwaka wa 1950 aliingia katika uongozi wa TAA kama Secretary pamoja na Dr. Vedasto Kyaruzi akiwa President.

Baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwira Abdul Sykes akawa Act. President na Secretary.

Nikiwasoma sharti wakati mwingine nacheka.

Dr. Kyaruzi kama kutafutwa alitafutwa na Schneider Abdillah Plantan kwa kuwa yeye ndiye alisimama kidete kumtoa rais wa TAA wa wakati ule ambae yeye ni kaka yake, Mwalimu Abdulkarim Thomas Plantan waingie vijana wabadlishe mwelekeo wa chama.

Ninao mswada wa kitabu alichoandika Dr. Kyaruzi, "The Muhaya Doctor," mna mengi watu hawayajui kuhusu nyakati zile za 1950s.

Hawa akina Plantan na akina Sykes ni ndugu kwa kuoleana toka wako Mozambique na walipokuja GermanOstafirka wakiwa na Hermann von Wissman kama askari mamluki wakawa wamefungamana na kuwa kitu kimoja chini ya Chief Mohosh kiongozi wao toka walipokuwa Kwa Likunyi, Imhambane, Mozambique ambae hapa Tanganyika alikuja kujulikana kama Affande Plantan.

Wajerumani wakamfanya Chief Mohosh ndiye mkuu wa Germany Constabulary na huyu ndiye aliyemlea Kleist Sykes.

Sykes Mbuwane baba yake Kleist alifariki kwa kufamaji Mto Ruaha wakati wanarudi kutoka Kalenga katika vita na Mkwawa.

Nakueleza haya yote kutaka wewe ujue ni nguvu gani familia hizi mbili za Sykes na Plantan walikuwanazo mjini Dar es Salaam.

Schneider Abdillah Plantan na Kleist Sykes walipigana Vita vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918) wakiwa ''battalion'' moja dhidi ya Waingereza na walikuwa wakizungumza Kijerumani.

Baada ya kuasisi African Assoiation 1929 Kleist aliunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933 ili kutenganisha African Association na mambo ya Uislam.

Schneider Plantan yeye akajakuwa Secretary wa Daawat Islamiyya (Wito kwa Waislam) iliyoanzishwa na Sheikh Hassan bin Ameir.

Hawa wote unaowasoma hapa walikua wanasiasa na pia viongozi wa jumuiyya za Kiislam.

Hawa ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika TANU na harakati za kupigania uhuru.

Jina la Nyerere kuwa kiongozi wa TAA lilipitishwa nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe na waliompitisha ni Mwapachu, Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyka.

Uchaguzi wa Arnautoglo kati ya Abdul Sykes na Nyerere nimeeleza mara nyingi sana.

Listowel katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika,'' (1965) kaeleza uchaguzi huu na kaandika kuwa Nyerere alipita kwa kura chache (Angalia uk. 221).

Ufinyu wa ushindi wa Nyerere nimeeleza sababu zake mara nyingi hapa JF.

Wewe kusoma kwenyewe historia hii shida unataka uje hapa uwanjani upambane na mimi mtu ambae hii historia si kuwa naijua kwa kuwa ni historia yangu bali nimetafiti na kuandika kitabu.

Viongozi ndiyo hao hapo chini baada ya uchaguzi ule wa April 1953:

''In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]''

Hii ndiyo historia ya TANU ikiwa nyinyi mna nyingine isiyokuwa hii na mna nyaraka zisizokuwa hizi tuwekeeni hapa tuzisome.

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

1648987335211.png

Thomas Abdulkarim Plantan
 
Mag...
Mbona mimi naandika bila ya kutukana?
Huu ni mjadala tu.

Historia iliandikwa lakini mimi nikaona ina makosa nimenyanyua kalamu kusahihisha.
Mbona hili jambo limekukasirisha kiasi hiki?

Abdul Sykes mwaka wa 1950 aliingia katika uongozi wa TAA kama Secretary pamoja na Dr. Vedasto Kyaruzi akiwa President.

Baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwira Abdul Sykes akawa Act. President na Secretary.

Nikiwasoma sharti wakati mwingine nacheka.

Dr. Kyaruzi kama kutafutwa alitafutwa na Schneider Abdillah Plantan kwa kuwa yeye ndiye alisimama kidete kumtoa rais wa TAA wa wakati ule ambae yeye ni kaka yake, Mwalimu Abdulkarim Thomas Plantan.

Hawa akina Plantan na akina Sykes ni ndugu kwa kuoleana toka wako Mozambique na walipokuja GermanOstafirka wakiwa na Hermann von Wissman kama askari mamluki wakawa wamefungamana na kuwa kitu kimoja chini ya Chief Mohosh kiongozi wao toka walipokuwa Kwa Likunyi, Imhambane, Mozambique ambae hapa Tanganyika alikuja kujulikana kama Affande Plantan.

Wajerumani wakamfanya Chief Mohosh ndiye mkuu wa Germany Constabulary na huyu ndiye aliyemlea baba yake Kleist Sykes, Sykes Mbuwane aliyekufamaji Mto Ruaha wakati wanarudi katika vita na Mkwawa.

Nakueleza haya yote kutaka wewe ujue ni nguvu gani familia hizi mbili za Sykes na Plantan walikuwanazo mjini Dar es Salaam.

Schneider Abdillah Plantan na Kleist Sykes walipigana Vita vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918) dhidi ya Wiangereza na walikuwa wakizungumza Kijerumani.

Baada ya kuasisi African Assoiation 1929 Kleist aliunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933 ili kutenganisha African Association na mambo ya Uislam.

Schneider Plantan yeye akajakuwa Secretary wa Daawat Islamiyya iliyoanzishwa na Sheikh Hassan bin Ameir.

Hawa wote unaowasoma hapa walikua wanasiasa na pia viongozi wa taasisi za Kiislam.

Hawa ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika TANU na harakati za kupigania uhuru.

Jina la Nyerere kuwa kiongozi lilipitishwa nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe na waliompitisha ni Mwapachu, Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyka.

Uchaguzi wa Arnautoglo kati ya Abdul Sykes na Nyerere nimeeleza mara nyingi sana.

Listowel katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika,'' (1965) kaeleza uchaguzi huu na kaandika kuwa Nyerere alipita kwa kura chache (Angalia uk. 221).

Ufinyu wa ushindi wa Nyerere nimeeleza sababu zake mara nyingi hapa JF.

Wewe kusoma kwenyewe historia hii shida unataka uje hapa uwanjani upambane na mimi mtu ambae hii historia si kuwa naijua kwa kuwa ni historia yangu bali nimetafiti na kuandika kitabu.

Viongozi ndiyo hao hapo chini baada ya uchaguzi ule:

''In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]''

Hii ndiyo historia ya TANU ikiwa nyinyi mna nyingine isiyokuwa hii na mna nyaraka zisizokuwa hizi tuwekeeni hapa tuzisome.

[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Thomas Abdulkarim Plantan
Kwa vile wewe unajua hiyo habari kwenye kitabu cha Listowel, kwanini usituwekee hapa page husika tuisome? Huyo Listowel alikuwapo kwenye mkutano wa Arnatoglou? Kwanini umuamini Listowel kama single source ya hoja yako?
 
Gold ...
Umenitukana.
Sifanyi mjadala na mtu mwenye kutukana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom