JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Pedro said:wazazi wetu walisoma bure, sisi tulisoma bure na sasa tunatesa.
Pedro,
umeshapata kujiuliza serikali ilitoa wapi fedha za kusomesha wazazi wako, pamoja na wewe bure?! kwasababu hakuna kitu cha bure dunia hii.
inawezekana we did not pay out of our pocket, lakini serikali ilitumia kodi tulizokuwa tunalipa kugharamia elimu,afya,ulinzi etc etc.
hii dhana ya kusema elimu bure ni kiini macho cha kuwaziba midomo,kuwatia unyonge, na kuwasomba msukule, wananchi. once ukiwaambia hivyo basi wanaona kama ni fadhila na hawatakiwi kuhoji jambo lolote.
Mwanakijiji,
Nitajaribu kuchangia vipengele vifuatavyo kama ulivyoviainisha.
Madini:
si kweli kwamba Mwalimu aliamua kilimo ndiyo kiwe uti wa mgongo wa taifa. kilimo tayari kilikuwa uti wa mgongo.
jambo aliloamua Mwalimu ni kwamba viwanda vya nguo ndiyo viwe injini ya uchumi wetu kuelekea industrialization. rejea hotuba ya mei mosi kule mbeya.
matatizo ya madini kuvamiwa na wageni ni ya uongozi na siasa. ziko nchi nyingi tu zimechimba madini bila kuvamiwa na wageni. mbona botswana hawana matatizo hayo ya DRC,Angola,...?
vilevile ni maandalizi gani yalifanyika kujenga uwezo wa kuchimba madini yetu? badala ya kufungua vyuo vya siasa bora tungejenga vyuo vya madini[engineers,technicians etc]
hata idara za geology na mining engineering hazikuwa idara za mwanzo kuanzishwa pale chuo kikuu. we simply didnt have a vision.
Siasa za Dunia:
actually hakuna anayemlaumu Mwalimu kwa kutofungamana na upande wowote. katika foreign policy ni wachache wanaomkaribia.
kipindi cha utawala wa Mwalimu tulikuwa tunapata misaada toka EAST na WEST kuliko nchi nyingi za dunia ya tatu. what we did na hiyo misaada ni kitendawili.
sikubaliani na dhana kwamba ati ni bora kuwa masikini lakini huru. hiyo ni dhana ya kukata tamaa. tunaweza kuwa huru na wenye maendeleo vilevile.
Azimio la Arusha:
Mwalimu mwenye alishasema kwamba alikosea kutaifisha mali na viwanda kwa haraka namna ile. wengi wetu tunapinga ile JAZBA na PUPA iliyotumika ktk kuendesha zoezi hilo.
vilevile kudai kwamba ati asingetaifisha mashamba leo hii Tanzania ingekuwa na matatizo ya ardhi kama Zimbabwe ni kupotosha. settler community ktk Tanganyika ilikuwa ndogo mno. vilevile isingeweza kustawi kwasababu tuliamua kuwa wajamaa, na ardhi,kabla hata ya 1967, iliamuliwa iwe mali ya taifa.
Hatukupaswa kutaifisha mashamba na viwanda vilivyokuwa vikizalisha tayari. Tulipaswa kuanzisha vyetu along side hivyo vilivyokuwepo.