Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,239
- 113,612
Mzee Mwanakijiji wewe una mapenzi binafsi na Mwalimu, hapo sikulaumu kabisa baba yetu wa Taifa ameifanyia Tanzania mambo mengi mazuri tu, wengi tulisoma bure, na wazazi wetu wamesoma bure, amani tunayo lugha moja n.k.
Kauli yako hapo juu ina-imply kuwa iliwezekana kumpinga Mwalimu, na kuwa uhuru wa vyombo vya habri ulikuwepo. Kwa mawazo yangu binafsi kumpinga nyerere haikuwepo kwenye agenda kabisa enzi zake hata kama hatuwezi kuthibitisha hayo kwa maandishi, uhuru wa kusema unachotaka haikuwepo kwenye agenda, achilia mbali magazeti hata kwenye vijiwe na washkaji watu walikuwa wanaogopa kusema vitu vya kupinga maana maofisa wa usalama wa taifa walikuwa wamepenyezwa kwenye kona zote za jamii na ole wako ujifanye unapenda uhuru ungekoma.
Mzee mwanakijiji hapo unamtetea mwalimu kwa mapenzi tu, hoja hapo hamna, aliyempinga mwalimu alikiona cha moto!
Achilia mbali uhuru wa kusema, enzi za Nyerere hata uhuru wa kumiliki chako haukuwepo, akiamua chako si chako basi hakitakuwa chako, anakuja kukuny'ang'anya mara moja, Azimio la Arusha pale aliwanyang'anya watu mali zao bila kujali haki zao za kumiliki kilicho chao, katika miaka ya 80 waziri wake mkuu aliwapelekesha watu kishenzi yeye akiwa raisi akiangalia tu, sijui majamaa ambao walikuwa wananunua mahindi na maharage na ku-supply shule za sekondari wengine wali-supply nyama n.k faida waliyopata katika mauzo hayo walinyang'anywa zote! polisi walikuwa wanakuja na kuwanyanyasa kishenzi kwa amri kutoka juu wakati watu wale walikuwa ni wafanyabiashara tu wanaojituma, ndio maana mpaka leo watanzania wakiona mtu mfanyabiashara anatengeneza pesa wanasema mbaya, wakiona mfanyabiashara anagombea cheo wanaona haifai, sharti uwe mkulima wa kahawa inayouzwa senti moja kwa gunia uwe fukara basi wewe safi.
Nyerere had his weaknesses vile vile hakuwa muumba, hilo lazima tutambue na kulikubali.
Kumbe na wewe umemstukia eehh? Mzee wetu huyu bwana ana mapenzi binafsi tu na Mwalimu na hayo mapenzi yamemgubika kabisaa kiasi kwamba haoni hata yale yaliyodhahiri...