FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Mwanakijiji,
Sasa mbona wewe mkuu unawaogopa hawa watawala kwamba watakukolimba? Lusekelo yuko pale pale tena anaandika kwenye gazeti la serikali.
Tanzania hatuna freedom of press kama baadhi ya nchi za West lakini pia hali sio mbaya sana kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini. Huenda woga wetu na rushwa vinatuponza zaidi kuliko hata
watawala kutuandama.
Tuwaunge mkono waandishi wazuri ili waendeleze mapambano ya fikra. Mwanakijiji, usiache mapambano na PM, tunataka makala kama ile ya Kasungura ka Lowassa.
Hongera Lowassa kwa kubaki na msimamo wako miaka na miaka bila kuyumba.
Mtanzania, wanasema huku bongo kuwa ukimwandika PM sana anakutafuta na kumkabidhi kijana wake amalizane na wewe. Wengi waandishi wanaandika kwa nia ya kutaka baadaye wanunuliwe!
Kuwa macho.