Lowassa Vs. Membe - Tanzania's own "Thrilla in Manila"?

Hatuwezi kukabidhi Tanganyika kwa Mzanzibar tuliwajaribu kwa Mwnyi tukayaona so Tanganyika haitakaa itawaliwe na Mzenj Mwingine


Kesho mtasema wazi mnayosema kivulini...hatuwezi kutawaliwa na Muislamu mwengine...... ofcourse now mnasema "mswahili" mwengine...
 
Yawezekana wewe ndio unaendeleza porojo.

Suala la Misri na Tunisia ni tofauti kabisa na Libya.

Katika Misri na Tunisia taratibu za kikatiba za kuacha na kukabidhi madaraka zilifuatwa kama ambavyo Umoja wa Afrika unavyotaka katika suala zima la mabadiliko ya utawala miongoni mwa wanachama wake.

Huko Libya kwa mujibu wa misingi ya Umoja wa Afrika hilo halikufanyika na hivyo mabadiliko na harakati zake zilizokuwa zikiendelea zilikuwa ni kinyume na misingi ya Umoja huo na nchi ambazo ziliunga mkono zilikuwa zikiangalia maslahi yao na sio misingi waliyojiwekea katika umoja huo na ndio maana wakati Umoja wa Afrika ulikataa kuwatambua Waasi wa Benghazi lakini haukukataza taifa moja moja kuwatambua.

Lakini zaidi kitendo cha mabeberu wa magharibi kugeuza ajenda ya kulinda wananchi wa Libya (Principle of Responsibility to Protect -R2P ambayo ukweli nayo ilichakachuliwa) kama Umoja wa Mataifa ulivyoamua na kuingiza ajenda yao ya REGIME CHANGE ni wazi uamuzi wa Tanzania uliosimamiwa na kwa umahiri mkubwa na Membe ni wa kujivunia na wa kulinda Misingi ya Umoja wa Afrika na zaidi heshima ya Bara letu na sio maslahi binafsi kama washindani wake na washindani wa CCM wanavyojitahidi kupotosha.

Matokeo ya nia hii ya upotoshaji wengi ama kwa kujua au kutokujua mmekuwa mkipigia chapuo propaganda za Mabeberu wa Magharibi katika mwanzoni kutetea na sasa kuhalalisha uharamia/maslahi yao dhidi ya taifa la Libya na pia dharau kuu dhidi ya Umoja wa Afrika...

Mkuu walichokifanya Waasi wa Libya hakina tofauti na Alichofanya Marehemu Gadafi zaidi ya Miaka Arobaini iliyopita. Gadafi aliua akaingia na hakuwahi kufanya Ucahguzi and Yet tulikuwa tunamtambua. Museveni aliingia Madarakani Kajeshi and Yet tulimtambua na bado tunamtambua. Kagame aliingia Madarani kwa Mtutu wa Bunduki tulimtambua na Tunamtambua.

Mkuu Kubali kataa katika hili la Libwa kuna Interest za akina Membe zimezimwa. Bila sahaka walikuwa wanampango wa kupokea Pesa ili waje wapambane na Laig'wanan Lowasa
 
Naona sasa wewe unaanza kuuchokonoa muungano wetu uliodumu kwa miaka 47, ambao umekuwa mfano wa kuigwa duniani kote!!

Hivi ule utaratibu wetu wa chama ambao hauko kwenye katiba, wa kupokezana madaraka ya uraisi kati ya Tanganyika na Zanzibar ndio tuseme umekufa? maana ule wa kupokezana kati ya wakristo na waislamu, bado tunauenzi!!

Muungano ulojaa Unafiki hautufai.

Ule Utaratibu wa Kupokezana Urais wa Zanzibar na Tanganyika ulikufa kifo cha kawaida tu na Hata rais wa Zanzibar ni sisi wa Wabara ndio tunaamua nani awe
 
In sad mind I'm contributing to the thread to see how even great thinkers are captivated by CCM such that they cannot fathom the idea of 2015 man of the nation to come outside of CCM!. It is so pathetic to see this even after all unprecedented corruption evils that the nation has witnessed under the rule of the party by the people of the party at the expense of the weary taxpayers. Now I am starting to beleive the casual words uttered by one member of the CCM party -- that CCM is here to rule forever no matter what!

No matter how i distaste the idea of Membe vs Lowassa for the presidency but if it were to be, God forbid, where would I bet my hard earned money? To be sincere, I would give a go for Lowassa. Why? Because the man is not a hypocrite. CCM is full of hypocrite corrupters and it seems to me that Lowassa is only a man who is not a double dealer in the town game. He is corrupt and he knows it but he is not afraid to tell of his corruption as part of grand scheme that contains even his boss -- the chairman of the party himself. Membe is just a hypocrite who pretends he is something when he is nothing. he was eve prepared to sell the nation to a bunch of human right violaters, the so called OIC (Organisation of Islamic gangs).

Thumbs up! Membe is nothing, I don't see a Presidency quality in him, He is jk's puppet! I strongly believe that we will never get a President we want from ccm. To me between those two, I choose none. I can rule this country better than any of ccm leader
 
Kesho mtasema wazi mnayosema kivulini...hatuwezi kutawaliwa na Muislamu mwengine...... ofcourse now mnasema "mswahili" mwengine...

Ha ha ha mkuu Omar vipi kunitia Kinywani Maneno ambayo sijayatamka! Nimesema Wazanzibar hawana nafasi tena ya Kutawala Tanganyika
 
EL hajaingia ikulu siraha zake ni tindikali,polium na thalium akiangia atatumia siraha gani kwa wanao mchallenge
 
Membe eti naye anataka kuwa rais! Nikikumbuka jinsi alivyoshupalia chenji ya rada kwenye vyombo vya habari nakosa kuuona ujasiri na uzalendo wake kwa taifa ili. Hawezi kamwe kulinda na kuheshimu maslahi ya mtz.


Nawe unaamini uzalendo na heshima kwa mtanzania ingelindwa kwa kuruhusu kampuni fulani ambayo ilihusika kuwatapeli watanzania hao kuiamulia nchi yako nini cha jinsi ya kutumia fedha zake

Namkumbuka pia jinsi alivyokuwa anaponda serikali ya mpito ya Libya akiwahusisha wanamapinduzi wale kama wahaini - hadi akawakemea wawakilishi wa Libya nchini walipopandisha bendera mpya. MEMBE HAFAI HATA KIDOGO.

Yule anayefaa kwako angeruhusu kundi la waasi ndani ya ofisi ya balozi nchini mwako kumteka balozi rasmi na kumlazimisha kupeperusha ndmbo ya uasi katika taifa rafiki kinyume cha misingi ya nchi yako na sheria za kimataifa?

 
May be sasa tuseme tuna front runners? hata hivyo hakuna mmoja kati ya Membe na EL aliyetangaza waziwazi nia yake kutaka kugombea 2015, pamoja na hayo hao wote wawili sioni 'Presidential Material'!
 
Mkuu walichokifanya Waasi wa Libya hakina tofauti na Alichofanya Marehemu Gadafi zaidi ya Miaka Arobaini iliyopita. Gadafi aliua akaingia na hakuwahi kufanya Ucahguzi and Yet tulikuwa tunamtambua. Museveni aliingia Madarakani Kajeshi and Yet tulimtambua na bado tunamtambua. Kagame aliingia Madarani kwa Mtutu wa Bunduki tulimtambua na Tunamtambua. Mkuu Kubali kataa katika hili la Libwa kuna Interest za akina Membe zimezimwa. Bila sahaka walikuwa wanampango wa kupokea Pesa ili waje wapambane na Laig'wanan Lowasa

Wakati Ghadafi, Museveni na hata Kagame anaingia kimabavu ulikuwa ni wakati wa OAU na principle ya kutokuingiliana masuala ya ndani bado ilikuwa na nguvu. Lakini pia msingi wa kutotambua mabadiliko ya Kiutawala kinyume cha Katiba kama ambavyo Constitutive Act of African Union na African Charter on Democracy, Governance and Elections zinavyosisitiza bado zilikuwa hazijaidhinishwa.... Zama tofauti...

Lakini pia katika masuala ya kimataifa kuna njia za kushughulikia masuala ya majirani zako ambako daima hautakosa maslahi na jinsi ya kushughulikia masuala ya mataifa ya mbali kijiografia na kihistoria.....
 
In sad mind I'm contributing to the thread to see how even great thinkers are captivated by CCM such that they cannot fathom the idea of 2015 man of the nation to come outside of CCM!. It is so pathetic to see this even after all unprecedented corruption evils that the nation has witnessed under the rule of the party by the people of the party at the expense of the weary taxpayers. Now I am starting to beleive the casual words uttered by one member of the CCM party -- that CCM is here to rule forever no matter what!

No matter how i distaste the idea of Membe vs Lowassa for the presidency but if it were to be, God forbid, where would I bet my hard earned money? To be sincere, I would give a go for Lowassa. Why? Because the man is not a hypocrite. CCM is full of hypocrite corrupters and it seems to me that Lowassa is only a man who is not a double dealer in the town game. He is corrupt and he knows it but he is not afraid to tell of his corruption as part of grand scheme that contains even his boss -- the chairman of the party himself. Membe is just a hypocrite who pretends he is something when he is nothing. he was eve prepared to sell the nation to a bunch of human right violaters, the so called OIC (Organisation of Islamic gangs).
Waheshimiwa mimi nasema hawa watu wote hawafai kabisa, kila mtu anazo kasoro zake tena kubwa tuu; EL ameweka mahela kibao huko Uswiss more than $300Million, tena mbaya zaidi amenunua mijumba mikubwa ya kifahali huko London, hotel moja Leicester, nyingine Trafalgar!!!!! SFO walizigundua na kupata taarifa toka BOT kuwa ni CO za EL akimpa mtoto wake anunue, ukimpa Urais je itakuwaje, si atahamisha nchi nzima!!!!!!!! Mwl Nyerere alimstukia kabla hajafa kuwa huyu jamaa ni mwizi, jamani ya nini kumpigia debe la Urais mwizi??????? Mhs Membe ni bomu hajui kupima upepo President lazima uwe na vision, juzi tu alishindwa kupima upepo wa Libya hadi dakika za mwisho alinganagana kukataa!! Tena anatabia za kujipendekeza kama mwanamke mara OIC mara huko na huko mwanamme lazima uwe na msimamo, usiyumbe maana Urais ni taasisi haitaji mtu wa kuyumba!!!!!!! Mbaya zaidi wote wanatoka chama cha wezi tena hawataki kupeleka wezi mahakamani, hao wote lao ni moja tuta dhurumiwa hadi lini?????????

 
Well.. the two camps are absolutely opposed to each other. Only one will emerge the winner and he would be the only one facing any other challenger for CCM Presidential candidacy in 2015. Will this be a full 12 rounds bout? I mean.. will we see the two camps chopping, upper-cutting each other before the CCM national Congress next year or even later towards 2015?

I'm asking myself why the differences between the two camps have become more pronounced and sharp in the past year?

One is the Minister of Foreign Affairs while the other is the Chair of Parliamentary Standing Committee for Security and Foreign Affairs!

Well.. somebody got to lose and somebody got to win - a tie is not an option. BUT what if they destroy each to the point that even the winner doesn't survive the fight! - well.. SOMEBODY ELSE will reap where he/she didn' sow! Thats my friends is politics!

Lets enjoy the show!

Four years ago, i came with a thread about LOWASSA and MWANDOSYA being the only two contenders for 2015 nomination. I was told that i am too ahead of time; I am still of the opinion that, if Mwandosya stands in good health, because we are told he is not well, the race remains to be between him and Lowassa; but if Mwandosya will not be able to run for health or any other reasons - whatsoever , it is Membe who will be the fall-back position for the camp;but the assumption is, wote watatangaza nia, otherwise hakuna aliyetangaza nia sio Lowassa, Membe wala Mwandosya;
 
Mashauri hoja zako zidi ya Mwakyembe na Mwandosya ziko very shallow!
Ushauri wangu kwa CCM big tribes kama Wanyakyusa,Wahaya,Chaga,Wasukuma,Wanyamwezi wapewe nafasi zingine ila sio URAISI
Maana uwingi wao na usomi wao utashangaa baraza zima la mawaziri wanatoka kumoja na iyo italipeleka taifa kwenye ukabila.
Ona ata historia Mzanaki then Mwinyi sijui mzaramo then Chinga then ****** si unaona vikabila vidogovidogo
Sikatai wapo waliotuangusha
 
Omarilyas,

Mkuu wangu ni vigumu sana kuwaelekeza watu ambao ngoma za kusikia zimeisha kufa. Watu hawaelewi walisemalo hata kama ukiwauliza ktk miaka yao ya uhai ni lini wamesikia machafuko na kuaawa kwa watu Libya wakati Ghadaffi akiwa rais?..waulize tukio hata moja wanalolikumbuka wao kwamba Ghadaffi alienda kijiji ama mji na kuua watu, hawana kumbukumbu hiyo isipokuwa kwa kusoma toka ktk magazeti na vyombo vya habari vya nchi za magharibi..

Leo hii huko Yemen, Bahrain, Syria, na kuliko yote Congo wanakufa watu kama utitiri mbele ya macho yao lakini siwasikii wakisema lolote juu ya hayo. Je, Nyerere hakuua? hakuwaweka ndani au kizuizini wale wote waliompinga waziwazi lakini mbona ndiye kipenzi chetu sote kwa sababu alikuwa na lengo zuri kwa wananchi wake..Vivyo hivyo, mkuu wangu ndio maana unaona watu hapa ni washabiki wakubwa wa Lowassa, mtu ambaye kashika mtandao na anajua namna ya kuwalaghai na kuwakaribisha wajinga ktk mtego utakaowanasa wenyewe..

Binafsi naamini kabisa yote hii ni ku shift fikra za wadanganyika waache kutazama mabo muhimu ya chama kujivua gamba, Katiba mpya na waaze kuzungumzia vita baina ya Membe na Lowassa lakini hakuna vita isipokuwa ni maonesho ya pambano la ngumi baina ya Lowassa na Membe - Mchezo - A sports thing ulopangwa kwa malengo na makubaliano ya ushindani lakini hakuna uadui.
 
Watanzania tukitaka rais nje ya ccm inawezekana, kwani imewezekana zambia, kenya aluta continua
 
Tufanye maandamano siku ya tarehe 09.12.2011 siku hiyo intakuwa ndio siku ya kuzaliwa fikra mpya za kimapambano
 
Ukiona watu tumeshaanza kubadili avator ujue ndie wingu zito linaanza kupotea na blue sky ndio yaanza onekana
Angalia avator yangu harafu tutakumbushana haya mwezi May 2015.
 
Muungano ulojaa Unafiki hautufai.

Ule Utaratibu wa Kupokezana Urais wa Zanzibar na Tanganyika ulikufa kifo cha kawaida tu na Hata rais wa Zanzibar ni sisi wa Wabara ndio tunaamua nani awe

Zanzibar ni nchi na wala rais wao, sasa tupokezane nini?.
 
Natamani sana kupewa ushahidi kwamba lowasa ana mali nyingi sana na anaccount nje na ni mwizi wa mali ya umma.

Tamaa yangu inatokana na sababu nyingi, na nyingine ni za kihistoria ila sababu kubwa ni kwamba sitaki kuingia kwenye dhambi ya kuhukumu bila ushahidi.

Wakati kambona anarejea nchini baada ya mfumo wa vyama vingi kufika nchini, mchungaji mtikila na wakina Fundikira. RIP. walituaminisha kuwa Kambona atatuletea ushahidi wa account za Mwl Nyerere alizokuwa nazo huko ulaya na watahakikisha pesa hizo zinarudishwa nchini. Waandishi walimwandama sana Mwl ajibu hizo hoja. Mwl akawaambia muulizeni aliyesema mpaka awape ushahidi na Mwl hakujibu ama kwa kukanusha au kukubali. Leo kila mmoja anaujua ukweli.

Wakati wa kumpata mgombea wa CCm 2005, Wanamtandao walituaminisha kuwa Dk Salim A Salim, ndiye aliyemuua Karume na Wazanzibar wakaamua kumpa Jk kura zao, wakasahau kabisa swala la zamu ya bara na visiwani, kwa sababu waliaminishwa vyema kwamba Dr ni Muuaji wa Kiongozi pendwa kwao. Omarilyas unalijua hili vizuri. Leo hii Kila mmoja anaujua ukweli.

RAISI AJAYE ATAAMULIWA NA WATANZANIA KUTOKANA NA UZURI WA SERA NA UWEZO WA KUSIMAMIA SERA ZA CHAMA CHAKE, NA KAMWE HAWEZI KUAMULIWA KWA PROPAGANDA ZA UFISADI, WIZI, UMALAYA NA MENGINEYO YASIYOKUWA NA USHAHIDI.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom