Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,566
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa
ADAIWA KUPIGWA 'STOP' ASISHIRIKI,ASEMA NI UZUSHI WA KIPUUZI, CHADEMA WALIA
Waandishi Wetu, Arumeru na Dar
USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.
Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.
Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.
Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.
Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: "Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka."
Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote" kwenye kampeni hizo.
Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.