Katika hali ya kawada naomba nitume rai yangu kwa viongozi wetu wa chadema kuacha mara moja mazungumzo ya siri waliyonayo na lowasa,kwani watanzania hawatakielewa chama chao wanachokipenda (cdm),lowasa amewaomba viongozi wa chadema wakubali kumsafisha katika kashifa mbalimbali za ufisadi na rushwa zinazomkabili.
Suala la ufisadi sasa viongozi wetu wa cdm mmeanza kuliona la kawaida na kushindwa kulielezea kwa kina namna linavyolimaliza taifa letu,kwani bado mirija wa mafisadi ipo wazi wazi lakini humliongelei arumeru au mnasubili mazungumzo yenu na lowasa yakwame ndio tena muwe na nguvu za kuchukizwa na ufisadi.
Kumbukeni lowasa akiingia madarakani ataua upizani kwani si mtu anayependa kupewa changamoto na washindani wake wa kisiasa,lakini pia watanzania wana nia ya kuwa na viongozi safi na serikali safi,tafadhali sana tunataka kuona serikali ya cdm madarakani na si serikali ya mseto anayoiahidi lowasa,kama yeye ana nia ya dhati basi aende akagombee ubunge monduli halafu asubilie kuja kuisaidia cdm na si cdm imsaidie kuingia madarakani kwa nkisingizio cha serikali ya mseto.je akiwasaliti mtawaeleza nini watanzania kama si chama kutoaminiwa wa wananchi walio na imani na cdm.
Mkuu Ritz,
Acha kudanganya, huyo changudoa wa siasa ameshapigwa marufuku kukanyaga uwanja wa kampeni Arumeru
Mkuu Mungi,
Nani mwenye uwezo wa kumpiga marufuku Lowassa kufika Arumeru.
Hivi unajua kuwa Lowassa, ndio anaratibu kampeni za kila siku za Sioi, tangu zizinduliwe rasmi na Mkapa.
Wanabodi.
Habari za uhakika ambazo zimethibitishwa na marafiki wa Lowassa, zinasema mbunge huyu wa Monduli amejipanga kuweka kambi Arumeru Mashariki katika wiki ya mwisho ya lala salama ya kampeni.
Hilo litakuwa kombora la mwisho la kuimaliza Chadema huko Arumeru Mashariki.
Kwenda kwa Lowassa, Arumeru ni wazi njia itakuwa ni nyeupe kwa mgombea wa CCM, Sioi kutokana na umahiri wa mwanasiasa huyo, si tu katika kuratibu kampeni, bali hata kukubalika na kuheshimiwa na wananchi wa jimbo hilo jamii ya Kimasai na Wameru.
Inasemekana Lowassa ndio alikuwa akiratibu kampeni za kila siku mgombea wa CCM.
Kwa mujibu wa makada wa Chadema waliopo Arumeru wanasema hata kabla ya ujio huo wa Lowassa, Chadema kimekuwa kikikumbana na upinzani mkali kinapojaribu kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kutokana na wananchi jamii ya Wamasai na Wameru kuwagomea si tu kuingia ndani ya nyumba zao kwa ajili ya kampeni, bali hata kuwasogelea.
Lowassa akifika Arumeru Mashariki si ndio itakuwa balaa kwa Chadema.
Lowasa yupi?
Yule gamba tulieambiwa na Nape?
Au yupi huyo!!
unamaanisha Lowassa baba mkwe ?? hapo mbona watakuwa wametimiliza usemi wa LUSINDE kuwa wapewe ubunge kwa ajili ya kuisadia familia kiuchumi. ujio wa Lowassa utageuza issue nzima ya kampeni kwenda kwenye baba mkwe kumtafutia mkwewe ulaji badala ya kutatua matatizo ya wananchi wa arumeru. ningemshauri akae pembeni kama kweli anampenda mkwewe badala ya kumharibia yeye akiwa kama DISGRACED PRIME MINISTER.Wanabodi.