Lowassa kuweka kambi Arumeru Mashariki kupangua mikakati yote ya CHADEMA

Kama lengo lako tujue na wewe Juma Hamis upo basi tumejua...

Ila umekaa ki CUF CUF hivi, isijekuwa Mtatiro umeingia kivingine
 
Katika hali ya kawada naomba nitume rai yangu kwa viongozi wetu wa chadema kuacha mara moja mazungumzo ya siri waliyonayo na lowasa,kwani watanzania hawatakielewa chama chao wanachokipenda (cdm),lowasa amewaomba viongozi wa chadema wakubali kumsafisha katika kashifa mbalimbali za ufisadi na rushwa zinazomkabili.

Suala la ufisadi sasa viongozi wetu wa cdm mmeanza kuliona la kawaida na kushindwa kulielezea kwa kina namna linavyolimaliza taifa letu,kwani bado mirija wa mafisadi ipo wazi wazi lakini humliongelei arumeru au mnasubili mazungumzo yenu na lowasa yakwame ndio tena muwe na nguvu za kuchukizwa na ufisadi.

Kumbukeni lowasa akiingia madarakani ataua upizani kwani si mtu anayependa kupewa changamoto na washindani wake wa kisiasa,lakini pia watanzania wana nia ya kuwa na viongozi safi na serikali safi,tafadhali sana tunataka kuona serikali ya cdm madarakani na si serikali ya mseto anayoiahidi lowasa,kama yeye ana nia ya dhati basi aende akagombee ubunge monduli halafu asubilie kuja kuisaidia cdm na si cdm imsaidie kuingia madarakani kwa nkisingizio cha serikali ya mseto.je akiwasaliti mtawaeleza nini watanzania kama si chama kutoaminiwa wa wananchi walio na imani na cdm.
Lowassa ni kiongozi wa watu.
 
Wewe ni Mnafiki, Muongo, Mbea, Mchonganishi, mtu uliye jaa chuki, shirki (hili neno kanifundisha mchunguzi, thanks mchunguzi), dhurma na ghirba na ni mtu usiyekuwa na shukrani, ufahamu, weledi, uungwana na usiyependa heri wala Amani.

nia yako ya kujionyesha kama Mwana CHADEMA kwa kujiandikisha "viongozi wetu chadema" imewekwa wazi na maandishi yako "wananchi hawatakielewa chama chao" na kumaanisha kwamba wewe unasifa zote nilizoziweka hapo juu.

Naomba kuanzia leo ujue kwamba wananchi hatuna shida na ufisadi wa Lowasa, kwa sababu sio ufisadi wa lowasa peke yake uliotukwamisha kwenye umasikini huu wa ajabu tulionao. kilichotufikisha hapa ni ufisadi, uongozi mbovu, ujinga, unafki, ghirba na ushenzi wa chama chenu cha CCM.

Pili wananchi tunajua kwamba viongozi wa CHADEMA wamekwisha kufanya kazi ya kujitolea sababu tunajua sio wajibu wao kuutangazia UMA nani ni mwizi na kaiba nini, bali hii ni kazi ya serikali ya CCM.

Mwisho, wananchi tumeishasikia sana habari za mafisadi na tumekwisha shawishika kwamba dawa ni kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi na kuikabidhi CHADEMA.

Muda wa kuanza kuisakama CHADEMA kwa mapungufu yoyote yale sio huu, nawashangaa sana mnapotaka kutuhadaa watanzania kwa ushenzi huu.

Tunakituhumu chama cha mapinduzi sababu ndio kilichoshika dhamana ya uongozi na kimeshindwa kuitumia, tutakishutumu CHADEMA tutakapokipa dhamana na kikashindwa, tena adhabu yao inaweza kuwa mbaya zaidi ya ile tunayowapa nyie sasa.

Mpaka sasa ninapoandika CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO hakina kosa, mawaa, laumu, na hakistahiri kusakamwa kwa lolote lile. Kama ilivyo TLP, DP, SAU na vyama vingine.

Hizi mbwembwe mnazozozitumia humu ni bora mkaandae mikakati ya kuwaua mafisadi wote japo wale wanaofahamika kwa majina kama huyo lowasa ili mpoteze ushahidi ama sivyo laana ya vilio vya watanzania wanaolala njaa, wanaokufa kwa kukosa huduma bora za afya na wanaoonewa na jeshi la polisi na kunyimwa haki zao chini ya serikali ya chama chenu itaendelea kuwasumbua na mtaweweseka sana mwaka huu
 
hii thread imekosea njia ilitakiwa iende kwenye yale magazeti ya rangirangi(Makolokocho).
 
Lisemwalo lipo na kama halipo laja!

Da S imekaa kama ina ukweli fulani vile !!!!!!!!!! Chonde chonde CDM yale mambo yalitokea kwa Sugu kupata ziara kuwa vipi dogo kwani nini uko tayari au namna gani vile piga chini mzigo ukamilike usawa huu,sugu akachemsha ubongo wake kuwa wana Mbeya hawatamwelewa kamwe hivyo mbele kwa mbele na mvumo wa wananchi leo hii Mbeya bila Sugu akieleweki.

Sasa CDM mkileta za mabobishi du nawapa pole,yani hakuna watu watakufa na nyie kama watzd wakijua mmewachezea chezo.Ni afadhari ya kujulikana kuwa mmeunda Serikali ya mseto sasa kwenye Serikali ya sasa ambayo watu wanaona na kuishika sasa, ya mtu ambae kidogo uwa na woga wa kibinadamu kama Jk,kuliko mcheza sinema ambae inajulikana kuwa anapo toa ahadi leo hatujui kesho atasemaje kuhusu ahadi kishaana tuhuma nyingi zisizo na maelezo yenye kutosha kujenga mwananchi akubaliane nae.

Ila kama ili ni kweli hakika CCM watatawala daima na daima ,kwa kuwa watanzania sio tu watacheka mitaani,bali watawafanyia mambo ambayo hawajawai kukifanyia chama chochote kile,yani itakuwa historia kwa viongozi wa CDM duniani, kwa kuwa sifa ya usaliti ni dhambii mbaya sana sana.

CCM hawajapata kuua kwa tafisri ya kuoganize mambo watu wakakifia chama,yana watu wakafa kwa nia ya kutetea chama,nikimaanisha CCM kama CCM hawajawahi kutoa hamasa umma ukafanya jambo baya la kusababisha wanachama kudhulika kwa nia ya kutetea Chama.Hivyo basi CDM wasifanye mchezo na umma,kwa kuwa CCM wameshacheza na Wananchi na wananchi wanataka mtu ambae ataizindua CCM toka usingizini na pengine kuiweka kando japo kwa muda ili next time ili CCM waone umuhimu wa kumuheshimu Mwananchi.

Kidole na jicho CDM,hakika naomba Mungu kama kuna hayo mazungumzo hakika kama mna hofu na Mungu basi tazameni nyuma na angalieni wale wote waliopoteza maisha kwa nia ya kutetea CDM kufika hapo walipo kwa tumaini kuwa wangekuwa hai basi wangeona faida ya STRUGGLE yao kama sehemu ya jamii katika kuleta mafanikio na kuwa sehemu ya watu waliofanya mabadiliko [Change].Kisha ghafla viongozi waliomhamasisha kuwa watumie njia hii kupata mabadiliko na kusababisha kifo chake leo wageuke dhamira ya marehemu hakika dhambi hiyo ya kugeuka dhamira ya umma na marehemu waliopoteza maisha yao kwa ajili ya CDM watajuta kwa dhambi hiyo kuitenda.

Ndio maana ukienda South africa kuna watu muhimu kwa ANC wanaotambulika na kuenziwa kuwa walipoteza maisha yao wakati wa vita vya ukombozi baadhi ya watu hao makini ni Steven Biko,wakina Oliver Tambo na wengineo wengi.CDM chezeni na mengine wakati mwingine pesa sio kila kitu,mnaweza kuvuta lakini mkatafutwa uraiani faida ya pesa hiyo ni nini,tena mbaya zaidi nyie mkachagua slogan kali na ngumu ya People's Power.

Wanachadema msitake sie tusio na vyama tupigie mstari maneno ya CCM kuwa CDM ni namna gani ndivyo sivyo.Please wanaCDM msichezee maisha ya watu.Nashukuru kuwa mmepunguza mvutano na dola dhidi ya maandamano lakini chini ya MATUAL UNDERSTANDING na mheshimiwa Rais, lakini sio kwa mtu ambae yuko nje ya madaraka kisa he has money and political influence kwa baadhi ya watendaji.AAAAAAAAhhhh CDM acheni hizo!!!!!!!!!!
 
Katika hali ya kawada naomba nitume rai yangu kwa viongozi wetu wa chadema kuacha mara moja mazungumzo ya siri waliyonayo na lowasa,kwani watanzania hawatakielewa chama chao wanachokipenda (cdm),lowasa amewaomba viongozi wa chadema wakubali kumsafisha katika kashifa mbalimbali za ufisadi na rushwa zinazomkabili.

Suala la ufisadi sasa viongozi wetu wa cdm mmeanza kuliona la kawaida na kushindwa kulielezea kwa kina namna linavyolimaliza taifa letu,kwani bado mirija wa mafisadi ipo wazi wazi lakini humliongelei arumeru au mnasubili mazungumzo yenu na lowasa yakwame ndio tena muwe na nguvu za kuchukizwa na ufisadi.

Kumbukeni lowasa akiingia madarakani ataua upizani kwani si mtu anayependa kupewa changamoto na washindani wake wa kisiasa,lakini pia watanzania wana nia ya kuwa na viongozi safi na serikali safi,tafadhali sana tunataka kuona serikali ya cdm madarakani na si serikali ya mseto anayoiahidi lowasa,kama yeye ana nia ya dhati basi aende akagombee ubunge monduli halafu asubilie kuja kuisaidia cdm na si cdm imsaidie kuingia madarakani kwa nkisingizio cha serikali ya mseto.je akiwasaliti mtawaeleza nini watanzania kama si chama kutoaminiwa wa wananchi walio na imani na cdm.

Another ****!!!
 
Katika hali ya kawada naomba nitume rai yangu kwa viongozi wetu wa chadema kuacha mara moja mazungumzo ya siri waliyonayo na lowasa,kwani watanzania hawatakielewa chama chao wanachokipenda (cdm),lowasa amewaomba viongozi wa chadema wakubali kumsafisha katika kashifa mbalimbali za ufisadi na rushwa zinazomkabili.

Suala la ufisadi sasa viongozi wetu wa cdm mmeanza kuliona la kawaida na kushindwa kulielezea kwa kina namna linavyolimaliza taifa letu,kwani bado mirija wa mafisadi ipo wazi wazi lakini humliongelei arumeru au mnasubili mazungumzo yenu na lowasa yakwame ndio tena muwe na nguvu za kuchukizwa na ufisadi.

Kumbukeni lowasa akiingia madarakani ataua upizani kwani si mtu anayependa kupewa changamoto na washindani wake wa kisiasa,lakini pia watanzania wana nia ya kuwa na viongozi safi na serikali safi,tafadhali sana tunataka kuona serikali ya cdm madarakani na si serikali ya mseto anayoiahidi lowasa,kama yeye ana nia ya dhati basi aende akagombee ubunge monduli halafu asubilie kuja kuisaidia cdm na si cdm imsaidie kuingia madarakani kwa nkisingizio cha serikali ya mseto.je akiwasaliti mtawaeleza nini watanzania kama si chama kutoaminiwa wa wananchi walio na imani na cdm.

jamani wanachadema naomba hapa TUFIKIRI KIUNDANI manake we are GREAT THINKERS kama vile napa mwanga fulani maana niko huku kwenye kampeni na sijawai kuona kiongozi yeyote wa chadema anauzungumzia ufsadi wa lowassa
 
Wanabodi.
Habari za uhakika ambazo zimethibitishwa na marafiki wa Lowassa, zinasema mbunge huyu wa Monduli amejipanga kuweka kambi Arumeru Mashariki katika wiki ya mwisho ya lala salama ya kampeni.

Hilo litakuwa kombora la mwisho la kuimaliza Chadema huko Arumeru Mashariki.

Kwenda kwa Lowassa, Arumeru ni wazi njia itakuwa ni nyeupe kwa mgombea wa CCM, Sioi kutokana na umahiri wa mwanasiasa huyo, si tu katika kuratibu kampeni, bali hata kukubalika na kuheshimiwa na wananchi wa jimbo hilo jamii ya Kimasai na Wameru.

Inasemekana Lowassa ndio alikuwa akiratibu kampeni za kila siku mgombea wa CCM.

Kwa mujibu wa makada wa Chadema waliopo Arumeru wanasema hata kabla ya ujio huo wa Lowassa, Chadema kimekuwa kikikumbana na upinzani mkali kinapojaribu kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kutokana na wananchi jamii ya Wamasai na Wameru kuwagomea si tu kuingia ndani ya nyumba zao kwa ajili ya kampeni, bali hata kuwasogelea.

Lowassa akifika Arumeru Mashariki si ndio itakuwa balaa kwa Chadema.
 
lowassa-top-safi.jpg
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa​
ADAIWA KUPIGWA 'STOP' ASISHIRIKI,ASEMA NI UZUSHI WA KIPUUZI, CHADEMA WALIA
Waandishi Wetu, Arumeru na Dar
USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.

Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.

Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.

Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: “Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka.”

Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote” kwenye kampeni hizo.

Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.

Lowassa ajibu
Akizungumza kwa simu kuhusu madai hayo jana, Lowassa aliziita taarifa za kukatazwa kwake kupanda jukwaani kumnadi Sioi kuwa ni “uzushi usiokuwa na msingi.”

Hata hivyo, hakuwa tayari kuweka bayana aina ya ushiriki wake kwenye kampeni hizo zinazoelekea ukingoni, huku CCM kikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mahasimu wao Chadema ambacho kimemsimamisha, Joshua Nassari.

“Kwani kuna nini, hakuna haja ya kuwa na haraka, kwani vyovyote itakavyokuwa mtajua tu,” alisema Lowassa.

Mapema jana asubuhi alipotafutwa kwa simu, Lowassa alisema asingeweza kuzungumza kwani alikuwa kwenye kikao. “Nipigie majira ya mchana kama saa tisa hivi, maana sasa niko kwenye kikao,” alisema.

Hata hivyo, watu walio karibu na kiongozi huyo walisema Lowassa atapanda jukwaani kesho na kwamba tayari ameanza kampeni za kumnadi Sioi kwa kufanya vikao vya ndani na kwamba kikao cha jana ni moja ya vikao hivyo.

“Hizo taarifa kwamba amezuiwa siyo za kweli, mimi nimehakikishiwa kwamba atapanda jukwaani kuanzia Jumapili (kesho) na ninavyofahamu tayari ameanza vikao vya ndani,” alisema mmoja wa watu wa karibu na Lowassa.

Mwana CCM mwingine aliye karibu na kiongozi huyo alisema: “Ni kweli walikuwa wakihaha kumzuia, eti wandai kwamba ushindi ukipatikana itaonekana kwamba ni mafanikio yake, lakini wameshindwa maana hadi sasa tuna uhakika Mzee (Lowassa) atapanda jukwaani."

Habari zaidi zinasema kuwa Mratibu wa Kampenzi za CCM katika uchaguzi huo, Mwigulu Nchemba juzi jioni alikutana na Lowassa kuweka mambo sawa kabla ya kiongozi huyo kupanda jukwaani kesho.

Timu ya kampeni
Tangu kuanza kwa kampeni hizo,inadaiwa kwamba kumekuwapo na hali ya kutokuaminiana ndani ya timu hiyo kunakotokana na kile kilichojiri wakati wa mchakato wa kura za maoni zilizompa ushindi Sioi.

“Tatizo kubwa hapa kwetu ni hilo, hawa wapambe wa mgombea hawaamini kwamba sisi wengine tumekuja kwa ajili ya kutafuta ushindi wa chama, wanatufikiria vinginevyo ndiyo maana unaweza kuona kama tuko makundi tofauti,” alisema mmoja wa makada waliopo Arumeru ambao wanashiriki kampeni hizo.

Kada huyo alisema awali ni kama kulikuwa na timu mbili za kampeni ambazo ni ile ya chama inayoongozwa na Nchemba na timu ya pili ni ile inayoongozwa na wapambe wa mgombea ambao walikuwa na wasiwasi kwamba mgombea wao anaweza kuhujumiwa.

“Lakini sasa naona kama imani inarejea taratibu, wanatuona tunavyochapa kazi na kumpigia kampeni mgombea wetu. Wasichofahamu ni kwamba msuguano huwa kwenye vikao tu, lakini mtu akishateuliwa hakuna haja ya kumpinga kwani kufanya hivyo ni kukiua chama chetu,” alisema kada huyo.

Hata hivyo, kada huyo alisema pamoja na misukosuko ya hapa na pale, kampeni zao zimekuwa zikiimarika kila kukicha na kwamba wana uhakika wa kushinda kiti hicho cha ubunge ambacho kiko wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Jeremia Sumari.

Chadema walia
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM.

Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.

“Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.

Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.

“Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.

Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.

Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu.

Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.

http://mwananchi.co.tz/component/co...s-story/21406-lowassa-aigawa-ccm-arumeru.html
 
Back
Top Bottom