Shida ya CCM wala siyo magamba. Walikosea sana walipoifanya hiyo ni hoja nadhani walitapatapa. Kinachotakiwa ni kuondoa kero za wananchi kupitia serikali yao. Ni kuiambia serikali itekeleze ilani yake. Magamba siyo sehemu ya ilani ya CCM na siyo iliyokuwa ikiuzwa na CCM wakati wa uchaguzi. Ni muhimu wakarejelea kwenye ilani na kuona ni kwa kiasi gani ilani imetekelezwa!