Lowassa aiteka CC na NEC...

Unatangaza mwisho wa CCM yaani kifo cha CCM ni sasa, watu wanaona hawadanganyiki!CCM wakimkumbatia EL wamejiua kisiasa elewa hilo!

Mtaweka post nyingi tuu humu JF za kutetea Boss wenu lakini Watanzania wa leo si wajinga ni waelewa, nyinyi na Bossi wenu mmekwisha! Why EL, ni mwizi na mnafiki period!!!!!!!!

Hivi Lowasa akifukuzwa katika chama matatizo yetu yataisha na CCM sasa itakua kipenzi cha Watanzania? Hivi madudu yote yanayofanyika nchi nzima kote huko ni Lowasa na wafuasi wake?
 
Lowassa ni mtu makini kuliko mnavyofikir angekua mwanasiasa mwingine asingeweza kuhimili mikiki,ndani ya ccm kuanzia top leaders mpaka mwenyekiti wa mtaa ni corrupt,hoja ya kumtoa lowassa kafara ni dhaifu kama ni kusafisha ccm Jk alipaswa aanze wafuate wengine,JK nchi imemshinda anabaki kutafuta mchawi,amalize kikao issue ya jairo,luhanjo,utouh na ngeleja iko mezani,CDM wako mezani kazi kwake apige mzigo aache uwoga
 
Unatangaza mwisho wa CCM yaani kifo cha CCM ni sasa, watu wanaona hawadanganyiki!CCM wakimkumbatia EL wamejiua kisiasa elewa hilo!

Mtaweka post nyingi tuu humu JF za kutetea Boss wenu lakini Watanzania wa leo si wajinga ni waelewa, nyinyi na Bossi wenu mmekwisha! Why EL, ni mwizi na mnafiki period!!!!!!!!


Mi nawashangaa watu wanavyozua mambo hapa,lowassa hakumbatiwi nyie vuteni subira mtasikia kilio kikubwa sana toka kambi ya lowassa muda si mrefu!!!achaneni na hizi hadithi!
 
Mambo hadharani, Edward Ngoyai Lowassa hatimaye amefanikiwa kupenyeza hoja yake ya CCJ ili kukwamisha hoja ya Kujivua Gamba. Habari za uhakika kutoka ndani ya vikao vya CC vinavyofanyika hapa Dodoma zinaeleza kuwa Lowassa, akipewa nguvu na Chiligati, Kinana na Mukama, amefanikiwa kumpa kigugumizi Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete kwa kuweka mezani hoja ya CCJ ambayo wachambuzi wanadai kuwa itawatia tunduni akina Samwel Sitta na Nape Nnauye.

Kutokana na hilo, hoja/mada juu ya kujivua gamba huenda isijadiliwe. Hadi nakwenda laptopuni jana, ajenda moja tu juu ya uchumi wa CCM ndiyo iliyojadiliwa hapa Dodoma. CC kikiwa ni kikao cha juu kabisa cha maamuzi kimeshindwa kumgusa kabisa Lowassa, Chenge na wafuasi wao. Wafuasi wa Lowassa wameapa kumpigania Mkuu wao hadi mwisho na kuhakikisha kuwa hagusiki.

Nimemnukuu mtu wa karibu wa Lowassa akitamba kuwa Lowassa hataguswa kamwe. Si mwingine ila ni Ole Millya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha. Maji yanazidi unga....Mimi ni Vuta-Nkuvute kutoka Dodoma nikiripotia JamiiForums.

Mambo Jambo!!!!

There are only two ways to live your life. One is as though nothing is a miracle. The other is as though everything is a miracle.
-- Albert Einstein
 
Watu walitaka anzisha ccj ili kuondokana na uchafu wa magamba, so it is not a big deal kwa watanzania.
Deal ni ufisadi na kujilimbikizia mali, huku ukiacha watanzania wakiteseka kwa magonjwa , umasikini ulikithiri na elimu duni.
CCJ si ishu inayo wasumbua wa TZ

Ndugu yangu waliotaka kuanzisha CCJ ilikua kwa manufaa binafsi na njaa zao. Hawana tofauti yoyote na viongozi wenzao ndani ya CCM. Wanawaza mali na madaraka kwa njia yoyote hata kama ni wizi wa kura ama risasi.
 
unajidanganya,rais kikwete anajua umuhimu wa el lwenye chama,nakuhakikishia chama kiatoka imara na el ataendelea kuwa mnec,na baadae mungu akimpa afya awaongoze watz

wee mwanga nini....... Nani kakwambia huyu fisadi la kutupwa atakuwa rais wa watanzania........ Labda huko kwao longdong na kiserian kwa masai wenzake...... Na lazima akina nape wajue..... Huyu jamaa ni hatari sana.... Wakiendelea kumlea naye watammwakyembe...... Labda nape na wenzake waondoke kwenye chama.....

 

CCM ni chama makini kimepitia misukosuko mingi tu.. huu nao utapita tu... suluhu litapatikana watu wataekana sawa

nina hakika hauzungumzii Richmond, epa, dowans, sukari et al
 
TUHUMA NYETI CCM LA UFISADI WA LOWASSA NA CHENGE NI KAMA USEMI WA KWENYE BIBLIA KWAMBA MJUMBE YEYOTE WA NEC ASIYE NA DOA JUU YA KOSA HILO AKAWATUPI JIWE LA KWANZA

Jamani kuishi kwingi kuona mengi; hivi nani angetegemea kuona vile vikao vya NEC enzi hizo ambazo CCM ilikua ni CCM kweli chini ya Mwalimu Nyerere kuona mtuhumiwa wao anageuka kuwa mtu wa kuchagua shitaka la kusikilizwa na hata namna gani maamuzi yawe??????

Hakika hii CCM ya sasa kwishny, bure kabisa tena hamna kitu cha maana kutarajiwa kutoka huko Dodoma zaidi ya wajumbe kuuziana chai tu na kumsikiliza mtuhumiwa mwenye dau kubwa kuliko wengine ndio wimbo wake kuimbwa usiku kucha

Huu usemi wa Lowassa kuiteka NEC yao ya CCM na hata kuipendekezea AJENDA GANI WAIZUNGUMZE (uanzishaji tu wa CCJ ambayo kamwe haikutupunguzia wananchi chochote kwenye kodi zetu kule benki kuu na kuacha kuajidili ufisadi) huko Dodoma ni sawa tu na kusema kwamba mtuhumiwa kateka yeyote yule awe ameiteka mahakama kiasi cha kuwafanya hakimu pamoja na mwendesha mashitaka kumshabikia.

Ndio, nasema nisawa na kusema kwamba hawa maafisa waheshimiwa sana wote wageuke kuwa mashabiki wake hapo mahakamani na hata kule kuomba japo tone la busara zakwe (kwa mtaji wa nywele nyeupe) akawachagulie KESI NYINGINE KABISA ya kuweza kusikiliza kwa siku hiyo; ama kweli kesi ya ngedere kwa tumbili!!!!!!!!!
 
KIGUGUMIZI CHA CCM KUJIVUA GAMBA DODOMA INA UJUMBE KWAMBA HIYO SARATANI IMESAMBAA MNO MWILINI HADI IKULU KIASI KWAMBA HATA PA KUWEZA KUKATA ILI MGONJWA AENDELEE KUISHI JAPO KWA MATUMAINI HMNA

Wingi wa mafisadi ndani ya CCM kama ambavyo wengine wanavyodai hapa hata siku moja haiwezi fisadi aliyekamatwa tayari na wananchi dhambi zake zikayeyuka tu eti kwa sababu ni kosa lililotendwa na wana CCM wengi sana, hapana!!

Hata kama zaidi ya theluthi tatu ya wana CCM wangetuhumiwa kuwa ni mafisadi, na kiukweli ndivyo hali halisi inavyoonyesha siku zote katikaa vitabu vyeusi mikononi mwetu wananchi juu yao, lakini HILO PEKEE kamwe haliondoi ukweli kwamba zoezi la kuvua gamba ndani ya chama hicho lazima ianzie mahala na kila faili kupitiwa kwa wakati wake.

Kwa msingi huo, kama ambavyo CCM lenyewe tu lilivyojitokeza na kukiri kuchukizwa na gamba kati kati yake na kuanza kujikana kujisafish na tatizo hilo sugu ili KIWEZE KUPENDEKA TENA nchini, hadi hivi sasa macho yote ni kusubiri kitu gani kinachotokea kwa kufunuliwa kwa faili zao akina
Mafisadi waliokubuhu - Chenge na Edward Lowassa huko Dodoma.

Lakini kwa bahati mbaya sana CCM ikifanyia mzaha swala la Ufisadi na mafisadi huko kwenye kikao cha huko basi sote tuhesabu tu kwamba hilo ndilo litakalokua sanda na jeneza la kisiasa nchini.

Hili la Lowassa kulialia eti kwa nini asulubiwe WAKATI YEYE ALITUKWAPULIA WANANCHI SI KWA FAIDA YA FAMILIA YAKE BALI NI KULE KULITUNISHA DHANA ILE ILE YA 'MASLAHI YA CHAMA' ndio kwanza limeongezea kuchafua mambo zaidi kwa CCMmpaka dakika hii na CHADEMA sasa kuonekana kuwa ni wakweli kupindukia juu ya tuhuma zote juu hawa magamba.

Ndio, nasema mpaka hapo tu ni kwamba amefanya kesi yake iwe mbaya zaidi na wala sidhani kama hiyo CCM anayodai kuifaidisha na wizi huo kweli wWATAMWACHI JAPO KA-KIPENYO kwenda kusema nje kile anachokiita yeye UKWELI WOTE JUU YA UFISADI WA RICHMOND alias DOWANS au kwa jina lingine SI-MBIONI.
 
Lowasa is a professional gambler hu knows when to fold a hand and when to call for cards.... Kama kuna anayedoubt uwezo wa jamaa in playing dirty games jus wait and see..
 
kuna watu wanajua fitina za siasa sio el aka mamvi, yeye najua kutumia pesa sio mdomo kama mnabisha tulia muone mambo yanavyokwenda!

you might be ryt ni kama uko akilini mwangu. Lowasa atawashangaza watanzania and nachelea kusema raisi watanzania ajae ni lowasa.
 
Chuki zenu na story za kumchafua lowassa zinawaponza lowassa ni miongoni washupavu walioko tanzania yeye alikubali kujiuzulu kwa dhana ya uwajibikaji ni viongozi wangapi wamekutwa na kashfa tena za moja kwa moja lakini bado wanang'ang'ania nyadhifa zao?

Ya Ngeleja, Jairo hamjayaona? why Lowassa? Chenge alikutwa na hela nyingi tu na akajiuzulu lakini haandamwi kama lowassa jiulizeni kwa nn?

Na siku zote mti wenye matunda ndo hupigwa mawe lakini endeleeni mwisho wa siku mtabaki na aibu ka nilivyosema awali tunarudi arusha na ushindi na mapokezi makubwa yanawangojea ndo hapo mtakapokufa na vijiba vya roho
No wonder that you resemble your avater and name!
 
Huyu EL wenu ananipa taabu kabisa. Kuna gazeti liliwahi kuandika kwamba Waziri mkuu mstaafu ni shoga. Hapo Mkuchika akaja juu kuliko kimbunga. Mambo yalisha poa.

Lakikini taktriban mara mbili hivi EL amewahi kuwajibu waandishi wa habari kwamba JK hakukutana Barabarani. Bahati mbaya hakuna aliyeuliza walikutana wapi au wamekuwa wakikutana kwa njia ipi?

Najaribu kuunganisha pragraph hizo mbili naona kama tunahangaishwa na upuuzi uliwahi kufanyika ktk maisha.
 
Hapa ndipo ninaposema kwamba watu akili hazilingani, unajua mtu anayetambua kosa na kuwajibika iwapo yeye mwenyewe au wenzake wamemtia lawamani huyo ndio mtu anae faa ila kuna baadhi ya watu watakupinga.

Hakika lowasa angekuwa mchafu walah naapa asingeachia ngazi ya uwaziri mkuu.
Maana asili aachi jasiri kama ingekuwa nia yake ni kuvurunda angekaa tu watu wangesema mwisho wasiku wangenyamanza.
Tanzania kwa hali tuliyofikia inapaswa tuwe na maamuzi yakukurupuka vinginevyo ni hakuna.
Binafsi sioni ubaya wa lowasa zaidi yakupenda ile style ya kumpiga chini kiongozi mbovu pale pale bila kumung'unya maneno.




mo2.jpg


sisasa ni mchezo mchafu, weledi wa kupanga hoja na kuzipangua ndio kufanikiwa.

Lowasa namwona ni mtu makini pekee katika serikali ya kikwete ambaye pekee aliyethubutu kujivua gamba binafsi kwa kujiuzuru uwaziri mkuu baada ya kashfa ya rishmond.

Wangapi wana kashfa nzito lakini kikwete anakula nao sahani moja? Naweza sema lowasa ni shujaa kwani viongozi wabovu wamejaa serikali ya tanzania kuanzia na mkulu mwenyewe lakini hakuna hata mmoja anayethubutu kujiuzuru au kuwajibishwa, badala yake wamejenga dhana ya kulindana.
 
Lowasa aka Tb Joshua ana roho ngumu sana na amwamua kupambana kufa na kupona.
 
Back
Top Bottom