Lowassa afunika Iringa

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli amedhihirisha nguvu kubwa na utajiri wa watu aliyonao, baada ya kupata mapokezi makubwa Mkoani Iringa.Lowassa amewasili Iringa asubuhi hii akiongozana na wabunge karibu wote wa mkoa wa Iringa,kwa ajali ya Harambee ya ujenzi wa kanisa na Kituo Cha radio Cha overcomers.viongozi wote wa Chama tawala Mkoani Iringa na Serikali nzima imempokea Mh Lowassa.
samahan napenda kujua utofaut wa kujiuzulu na kustafu, maana kuna watu wanasema jamaa alijiuzulu kwa ufisadi?
 
Waziri mkuu aliyejiuzulu tu inatosha, sasa tukianza kutoa sababu za aliejiuzulu kwa sababu hii na ile itakuwa kazi, hasa ukiangalia jambo lenyewe linalozungumziwa wala hakuna haja ya yote hayo, halafu kitu kingine ikumbukwe tu hakuna haja ya kumuandama mtu kwa mazuri anayoyafanya pindi apatapo nafasi, kwa hili Ben naomba siasa ikae pembeni.

Haitoshi.Hizo sifa ni zake.

Kumuandama mtu anapofanya mazuri?Mbona vibaka waliopo gerezani wanapopewa kazi ya kulima bustani makosa yao hayafutiki ingawa wamefanya kazi nzuri?Kila kibaka sasa nadhani awe anachangachanga sasa maeneo mbali mbali ili tuhuma zifutike ghafla.

C'me on,Huwezi kujenga jamii adilifu kwa namna hii.Tuache unafiki!
 
Hizi ni mvua za rasharasha tu. Mapokezi makubwa yatakuwa siku anatoka Dodoma akiwa mteule. Hakika siku hiyo Watanzania tutaona ishara kutoka Mbinguni. Kila lakheri KIONGOZI WA DHATI, Edward Lowassa. Kelele za wasioitakia mema Tanzania kamwe zisikutikise.
 
Richmonduli ataadhibika mbele ya Mungu,maana hapa bongo vyombo za sheria ndani ya SISIEM is wastage of time and resources
 
Acha yeye aendelee kumhonga Mungu kwani ni pesa yetu ileeeeee aliichukua kipindi kileeeeee sasa anairudisha kwa mtindo huu..Kudos Lowasa endelea kujenga makanisa watu wamrudie Mungu labda kitaeleweka.
 
@ Ben Saanane, Hakulazimishwa kujiuzulu. Taarifa ilitamka 'ajiangalie halafu achukue uamuzi'. Hakuna sehemu yoyote aliyolazimishwa kujiuzulu. Tatizo mlisha tembea sana na hoja ya ufisadi, sasa ni monotonous kuzidi kuishadidia. Hapo Lowasa ndipo anaawacha kuelekea touch line. 2015 mtarudi tena na hoja ya ufisadi, imeshawachosha watu masikioni.
 
kutafuta uraisi makanisani

Kama alivyofanya Slaa lakini tofauti yao yeye anafanyaa harambee kwa ajili ya kanisa,Slaa aliwatumia watumishi wa makanisa harambee anafanya kwa jina la m4c fungu lake yeye na wajanja wachache wa makao makuu
 
Hahaaa, Ben au bean Saanane? kazi mayo CDM mtajaribu kujikuna huku na kule lakini mwisho wenu chali, Vipi mkuu yule mjukuu wa balozi ana umri gani sasa?

Unapesa ya kumlipia ada ya chekechea IST? Ulichangia nini ktk kumtengeza? Au unauliza ili iweje?
 
huyu si ameshakatazwa na kina nape kutembelea kamanisani kuikosoa serikali? akijifanya anachangisha hela kule kumbe anajipalilia 2015 urais kwa tiketi ya ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom