Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,712
Siku hizi wanaume wamekua wakilalamika kuwa wanawake wamekuwa wakipenda hela na hawamtaki mwanaume asiekua na hela.Wanawake nao wamekuwa wakidai kuwa sio kweli kuwa jambo hilo lipo na kama lipo ni kwa wanawake wachache sana.Lakini pia ukitazama mazingira utaona kila upande unazungumza ukweli fulani.Mazingira yanaonesha kuwa pande zote zipo,yaani wanawake wapenda hela wapo na wanawake wanatambua hilo,tofauti ni ukubwa wa tatizo unavyoonekana kwa wanaume na wanawake,wanaume wanadai ni idadi kubwa ya wanawake ndo wanapenda hela.Maisha yamebadilika sana pesa inaonekana kama tool kuu ya kuendesha maisha mpaka inatumika kwenye kuamua nani awe na mahusiano na nani!Ukweli ni huo na wa kulaumiwa anaonekana ni mwanamke coz ndie anaefuatwa na ndie anaekubali au kukataa,hivyo wanaume wamekuwa wakijitoa kwenye lawama hii.Lakini je nani mwanzilishi halali wa kadhia hii?Hivi wanaume wakigoma kuwa wahongaji jambo hili litaisha?Au wanawake watalazimisha?Je nani anaweza kubadili hali hii wanawake au wanaume?Maana inaonekana mapenzi ya bila hela kama hayawezekani siku hizi!