Live on Star TV: Bajeti 2012/13 utekelezaji na utashi wa kisiasa

Nampongeza ndugu marcus(activist) namuomba aungane na rev mtikila wafungue kesi kuhusu bajeti ya tanzania isivyotekeleza!!
 
Ni furaha kuona kipindi kimerudi tena.

Moja, Tulikuwa na budget ya trilioni 13 kwa mwaka 2011/2012 malengo hayakufikiwa sasa malengo ya 2012/2013 ni trilioni 15, haijaelezwa wazi kwamba ni kitu gani kilitukwamisha kwa mwaka wa fedha uliopita na kipi kitafanyika tutafanya tufikie malengo kwa mwaka unaoanza July 2012.

Mbili; bado hatujaweza kupanua wigo wa kodi, bado tunawaza mfanyakazi, bia, soda na sigara

Tatu, ili kupambana na mfumuko wa bei, naona serikali inalenga kupunguza kiasi cha hela kwenye mzunguko, hii ni sawa kama njia ya muda mfupi, hii ni njia aliyotumia mkapa alipoingia madarakani, lakini njia ya muda mrefu ni kuongeza uzalishaji, hakuna mipango ya wazi ya kuongeza uzalishaji

Nne; Vyama vya siasa vitaendelea kulipwa zaidi ya bilioni 1.2 kwa mwezi, CCM zaidi ya milioni 800, CDM zaidi ya milioni 200, CUF zaidi ya milioni 117, hii ni dhuluma kwa watanzania
 
Star TV tunaomba mtujibu kwa nini hamrushi matangao ya moja kwa moja mkutano huu wa bunge kama ilivyokuwa kawaida yenu ????? !!!!!!

kwani mnajua wazi kua kituo chenu kina sikika nchi nzima tofauti na vituo vingine kwa nini mumeamua kutufanyia hivyo watanzania wenzenu ??????
 
1. Jinsi serikali inavyotekeleza bajeti yake: ni 62% tu imetekelezwa
2. Tanzania hatukusanyi mapato, ni karibia bil500 hawajakusanya kutoka kwenye madini tu, kiujumla ni $bil1 mil hazikusanywi
3. 10% ya bajeti ni matumizi ya magari
4. Bajeti hii ni mbaya kuliko iliyopita
5. Halmashauri ya Hanang wamenunua pikipiki kwa sh mil27
 
Yahya.

Tatizo kubwa la Tanzania uchumi wetu unatumikia siasa.
 
Last edited by a moderator:
Hivi watu wakiacha kuvuta sigara na kunywa pombe serikali haitafanya chochote?
 
Serikali iliyopo iliingia madarakani kwa kutumia mtandao, yaani kikundi fulani kilipanga kumuingiza kiongozi waliomtaka madarakani! Watu hawa hawakuwa na ajenda yoyote wala mpango wowote wa kuleta maendeleo.

Kwa mtindo huu hakutakuwa na bajeti itakayopangwa na serikali hii itakayo toa kipaumbele kwenye maendeleo. Na mwishowe hata kujiendesha kama serikali itakwama.
 
Majadala mzuri sana, hongera sana Yahya.

Kwa matazamo wangu hii bajeti wala haina nia ya kutukwamua watanzania, coz hata wao wenyewe serikali wanaonyesha kuwa bajeti hii itakuza uchumi wetu kwa 0.4% yaani kutoka 6.4% hadi 6.8%, kwa hiyo naomba watanzania na bunge tuipinge kwa nguvu zetu zote.
Lakini katika vipao mbele vya serikali sijaona elimu ipo sehemu gani.

Sasa kama serikali inapuuza elimu ambayo ndo msingi wa taifa lolote lile. Nimekuwa nikisikiliza bajeti za nchi nyingine za Africa Mashariki ziomejitahidi sana kuweka kipao mbele katika elimu.

Kwa mtizamo wangu naomba naona serikali imeamua kujiondoa kuchangia elimu. Naomba irudi ili tuongeze kipao mbele cha elimu
 
jamani hawa viongozi wetu kama hawana uwezo wa kuandaa mambo ya kulidhisha yaanc hata kudesa maon ya wataalam hawawezi
 
Serikali iliyopo iliingia madarakani kwa kutumia mtandao, yaani kikundi fulani kilipanga kumuingiza kiongozi waliomtaka madarakani! Watu hawa hawakuwa na ajenda yoyote wala mpango wowote wa kuleta maendeleo.

Kwa mtindo huu hakutakuwa na bajeti itakayopangwa na serikali hii itakayo toa kipaumbele kwenye maendeleo. Na mwishowe hata kujiendesha kama serikali itakwama.

Kuna tatizo kubwa la kusimamia utekelezaji wa bajeti na utungaji wa bajeti inayoitwa ya wananchi,huku watendaji wa Serikali kushindwa kusimamia sheria ya vijiji kwa kuitisha miktano mikuu ya vijiji kila baada ya miezi mitatu,ili wananchi wasikilize mapato na matumizi,waibue miradi na washauri serikali,bajeti inaenda kutumikia wananchi vijijin ambako wananchi wanasemwa kwenye makaratasi ya serikali na siyo kwenye maeneo ya wananchi.

Diwani anakwenda full council akiwa amebeba ajenda yake na siyo ya wananchi kupitia WADC,hivyo bajeti hubaki ni ya viongozi na siyo ya wananchi.Miradi inayosemwa itatekelezwa utashangaa wananchi hawaijui.,atatekeleza nani?
 
Wanasiasa wa nchi hii wamejaa usanii. Sijawahi kusikia bajeti ambayo haina makosa. Ikifika bungeni utasikia wabunge wanaikosoa tena huku jasho likiwatoka na mishipa kuwasimama. Mwisho wanaipitisha bila kupingwa. Hatari sana, mwanasiasa wa nchi hii ndiyo adui wa mwananchi.
 
Star TV tunaomba mtujibu kwa nini hamrushi matangao ya moja kwa moja mkutano huu wa bunge kama ilivyokuwa kawaida yenu ????? !!!!!!

kwani mnajua wazi kua kituo chenu kina sikika nchi nzima tofauti na vituo vingine kwa nini mumeamua kutufanyia hivyo watanzania wenzenu ??????


JIBU Tayari umepata. Stay tuned Kesho. Kingine!
 
Yahya,
Hongera kwa mjadala mzuri...
Bajeti zilizopita (ukitoa kindi cha mwl JK), bajeti hii na bajeti zijazo kamwe hazitaweza kumsaidia mwananchi wa kawaida! hii ni kutokana na ukweli kuwa;-

1. Mipango yetu mingi tunapangiwa na nchi za kibeberu kupitia wabakaji wao wa kiuchumi yaani Economic Hit Man (EHM). Hawa wabakaji ndio tuliowapa dhamana ya kutuendeshea uchumi wetu tukiwaona kuwa ni wasomi wenye exprnce za WB na IMF.
2. Sera zote za maendeleo tunaandikiwa na hao EHM mfano sera ya madini, fedha, BOT act nk
3.Sisi kama nchi tunafumbia macho mambo yenye maslahi ya kitaifa mfano ktk bajeti hii imetoa misamaha ya kodi kwa vifaa vya kuchimbia madini eti emaamuliwa na nchi wanachama wa EA! hivi hizi nchi jirani tulioungana nazo wanachimba madini kwa kiasi gani kwa ujumla wao ukilinganisha na sisi?...

.... kama nchi tuwe na sera na mikakati yetu wenyewe japo itakuwa ni vigumu sana kuwazuia hawa EHM ambao tumewapa dhamana ya kututawala kwa sasa...
 
Bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha Dr. Mugimwa haija mukomboa mwananchi,wakati anasoma budget basi kwenye runinga tukasoma kenya waanza kulipa wazee, vikwazo vya tozo barabarani vya ondolewa kenya.

Ukweli nilitegemea ukombozi huu kwa budget yetu lakini maneno ya waziri ya kawa yaleyale ya mkulo,nilimuona anafurahia zaidi kuwa waziri wa fedha kuliko kuongekea maisha ya wananchi wa chini na wazee hivi iko wapi kauli mbiu ya kilimo kwanza ili basi budgeti ingesomwa kufufua kilimo cha pamba katani tumbaku.

Lakini budgeti inaongelea wafanya biashara tena kwa mbwembwe kanakwamba nchi hii kila mtu ni mfanyabiashara ukweli inasikitisha sana budgeti ingeongelea kuboresha elimu kwa mkakati wa pekee wa kujenga maabara za shule za kata hii pia ndoto eti wametenga budgeti ya kurudisha jkt hili sijapongeza hatakidogo mi naijua jkt nilijiunga mwaka 1993 Mlale jkt ukweli nilicho kiona ni aibu tupu badala ya utaifa labda kufyatua bunduki na kukimbizana kama punda.

Je, wakubwa hii jkt wanamrudishia fisi mwanakondo? Akatafune vizuri kule wanawake mabinti wazuri wanapofika wanapelekwa rest house kupika na kustarehesha wakubwa tu hii haija angaliwa ninachojua watoto wa kike wa vigogo hawatapelekwa huko wazo hili zuri lakini chafu jaribuni vitu vingine kuhusisha maoni ya waliopitia jkt watoe maoni nini labda kifanywe labda zianzishwe kambi za watoto wakike na wakiume na askari wa jinsia zao vinginevyo Tanzania ya watoto wawanyonge inaenda kuangamia na UKIMWI karibu budgeti mpya na upofu wa mambo mapya
 
Tumewasikia wadau mbalimbali wakisema walishirikishwa kwenye kuandaa hi bajeti, Lakini wanasema mawazo yao na maoni yao hayakuingizwa kwenye Bajeti, Tatizo lipo kwa waandaji ambao kazi yao ni kukopi na Kupest bajeti zilizopita watumishi wetu hawahitaji kuumiza akili kuangalia mambo muhimu ktk kupanga Bajeti na Matokeo yake ndo haya tunayo yaona
 
Yahya, mimi naomba, uwaulize hao Wageni hapo studio, je serikali huwa inaeleza utekelezaji wa bajeti iliyopita?:thinking:
 
Kaka Yahaya budget ya mwaka huu ni budget ambayo ni kiini macho kwa sababu ifuatayo hivi inakuwaje serikali iongeze trilion 2 kutoka budget ya mwaka jana na zote ziende kwenye matumizi ya kawaida?

Na serikali hiyohiyo imepunguza matumizi ya maendeleo kwa zaidi ya bilion 400? Hiyo ni kutokana na serikali yetu kuongeza mikoa na wilaya ili waweze kulipata fadhila kwa marafi wa watawala bila kuwa na aibu wala haya na kwakujua kuwa watanzania niwajinga kupitiliza na pale watanzania wakiamka kudai haki yao wanaambiwa wanavunja aman na utulivu wa nchi.

Swali je kulikuwa na umuhimu gani kwa serikali kuongeza mikoa na wilaya wakati tumeona kuna baadhi ya mikoa na wilaya imekaa mwaka mzima bila mkuu wa mkoa na wilaya na mambo yakaenda? Jaman serikali inapotupeleka ni kubaya sana chonde chonde watanzania tushikamane tukomboe nchi yetu
 
Back
Top Bottom