Live: Kizota Dodoma

ndio manaake,wewe ulitaka nani awe,Makambna anakipenda chama ..mapenzi yake yote yako katika chama,unajua kwanini makamba alisema I lvoe CCm?anajua uwezo wake kichwani ni mdogo na akimwaga na chama hana pa kukimbilia,kwa kifupi ni kilaza
..viongozi wa nmana hii ndio maana tunaendela kuwa masikini
Kwi kwi kwi

Nakupata mkombozi, kweli sisiemu haimtupi mtu.
Tupo pamoja!
 
Bara

Zakia Meghji
Pindi Chana
Abarahaman Kinana
Andrew Chenge
Anna Makinda
Rostam Aziz
Dr Kigoda

Visiwani

Maua Daftari
Mohd Seif Khatib
Yusup Mohd Yusuph
Samiha Suluhu
Fatma S Ally
Gharib Bilal
Omar Yusuph

Baadhi ya walioanguka

Kingunge
Wassira
Guninita
Pinda
Rehema Nchimbi
 
that was my question kwa Kingune kupata kura alizopata kwenye NEC na bila ya shaka amelipia gharama ya kukurupuka!
 
Kilitime,
nafikiri wahitaji msaada wa kutafutiwa yaliyozungumzwa huko nyuma juu ya mwenendo mzima wa Karamagi and his team...............im sorry, i wish ningekuwa na muda huo wa kupitia hizo mada za huko nyuma............................kama ulishindwa kumake-sense out of yaliyochambuliwa kuhusu anayofanya Karamagi.......sidhani kama tunahitaji mtu mwenye macho kuambiwa tazama tena.............do not fall on to the trap........kipenda roho.........and i don't think umefikia hatua hiyo.

Kilitime..........pato la Taifa ni pato la Taifa and nothing else....the percentage tells you all!!.........huwezi kuja eti kusema.....sijui in foreign currency ni asilimia nyingi!!!!! teh teh teh what is asilimia nyingi unayotaka tuishangilie hapa...............the end point ni ile ile 1.9% period............kiwango ambacho sitaki hata kuamini kuwa naishi humu duniani.

Hivi kweli kwa mikataba kama ya Richmond na Buzwagi........bado unaona hakuna mkosaji!!!!............NB hapa simaanishi karamagi peke yake......no.....ni pamoja na team yake nzima...................hivi ulikuwa wapi wakati watu wakichambua baadhiya vipengele vya Buzwagi??

Umesema JK ana-regret pale alipomuonea mtu kwa makosa sio yake na hivyo anogopa kufanya hivyo kwa Karamagi..................huu ndio tunauuita UDHAIFU. President Ukikosea unarekebisha na unawajibisha/unawapa ONYO KALI waliokukosesha...........bado JK ni dhaifu ktk hili

Yes, i said it kuwa we have a long way to go...........yes yes kwasababu kama hizi za kutetea uozo ulio wazi..................we are here at JF kupiga vita sheria na mikataba mibovu na wabunge WAVIVU (ofcourse the majority) wa kufikiri na wabinafsi.

Kutetea Kosa eti kwa kuwa ni "Business as Usual" or eti kwakuwa sheria zilizotungwa ni mbovu and still unatekeleza........What have we (wananchi) put you in for.......ili ukafanye UTUMBO??.........this is very low in my opinion
 
Kuna habari za kuaminika kabisa kutoka Dodoma zinazosema wajumbe wateule wa NEC wamemnyima kingunge kura kuingia central committee (CC). Sijui tafsiri ya hii ni nini. je, ni dalili za mabadiliko yenye manufaa kwa chama? kazi ipo.
 
Kuna habari za kuaminika kabisa kutoka Dodoma zinazosema wajumbe wateule wa NEC wamemnyima kingunge kura kuingia central committee (CC). Sijui tafsiri ya hii ni nini. je, ni dalili za mabadiliko yenye manufaa kwa chama? kazi ipo.

..kwani huyu si ndio mmoja ya washauri muhimu wa mhishimiwa?ua siku hizi kibao kimegeuka?
 
raimwema, jamani someni kidogo thread walizoanzisha wenzenu, maana breaking news kama imeshakuwa broken, basi inabakia kuwa ni break new. Tunashukuru kwa mchango wako.
 
Kuanguka kwa Kingunge, lilikuwa ni suala la wakati tu, maana huko nyuma niliwahi kusema kuwa kwenye kikao cha kamati kuu cha kwanza chini ya Muungwana kama mwenyekiti, jinsi alivyomkaripia Kingunge kama mtoto mdogo, pale Kingunge alipodai Mahita afukuzwe kazi mara moja, nikawakumbusha tena majuzi kwenye kikao cha cc ambapo tena Kingunge alipotaka wabunge wawili wale wa "rushwa" wafukuzwe, alivyoshushuliwa na Muungwana,

Na pia nikawakumbusha kuwa mwenyekiti wa ccm ndiye huwapigania watu anaowataka kuingia cc, asiowataka hawawezi kuingia huko hata kama noma na iwe, na katika siasa za ccm, hata uwe na nguvu kiasi gani, kama huingii cc, wewe ni msindikizaji tu,

Swali la msingi hapa ni je Kingunge atakasirika na kugeuka mpinzani ndani ya ccm?, au atajiunga na asilia? Ataingia Chadema? Kumbuka hii ni mara yake ya kwanza kupigwa chini katika siasa, au naye atajiunga na kina Sumaye, na Salim kwenda kupewa counselling kwa Malecela, ya namna ya kuishi baada ya kushindwa uchaguzi?
 
Ogah,
Unajua huyu mjomba anataka kutupa hesabu zile zile za kutumia GNP ktk GDP, wanajaribu kuepuka kutumia takwimu za fedha yetu ya Madafu..lakini ukweli ni kwamba Canadian Barrick na wengine wote wawekeshaji toka nje, huchangia kwetu GDP lakini huko kwao ni huchangia GNP yao na tunapojaribu kutumia takwimu zao za GNP kuepuka fedha zetu za madafu ni kujivika kanzu sisi wenyewe (Tunajidanganya). After all asilimia hata siku moja haiwezi kubadilika wala kubadilisha reality.
Kilitime,
Uchaguzi umekwisha sasa ni wakati wa vitendo, yote tisa usia mdogo kwenu CCM - Put your money where your mouth is!...
 
Kingunge chali! Unimaginable! Hii hakika sijawahi kusikia hadi makamo haya niliyofikia. Ngoja tuone yatakayotokea, je Mwungwana hana mlango wa kumrudisha ndani kama mshauri wake? Au ni hatua za kum-phase out kingunge (mmh! lakini sidhani, mbona ni yeye mwenyewe aliyemteua kuwa waziri wa kitu kisichokuwapo, hadi wenye kusema yao wakadai ati Kingunge ndio mchawi wa CCM kwa hiyo kila serikali lazima awepo!) Mnakumbuka zile enzi za "waziri asiye na wizara maalum"? (kizungu waliita "minister without portfolio"!)
 
wewe nafikiri haupo dunia hii !
HABARI ZA MOTONI MKUU ??

Hapa motoni kijiji cha Unyanyembe poa tu. Nyie vipi huko peponi pamoja na mafisadi wenzako? Nasikia mmemaliza kikao chenu cha ufisadi kule Kizota...na mwaka huu mtatumaliza sisi wadanganyika.

Btw, tuendelee kukata ishu usianza kubadilisha mada. Na kama huna hoja, tafadhali usilete vioja.
 
sio kubadirisha hoja shetani,
swali ulilouliza ndilo lililonishangaza ! haya tuendelee na mada !
 
Ngoja na mimi nianze kupondea JF kama wanasisiem hapa

yaani inakuwaje sasa hivi ni wanasisiemu tu ndio wanachangia hapa kwenye mtandao? inabidi kuwe na balance? hii JF inaanza kukosa muelekeo sasa, mbona hakuna vyama vingine hapa?

yaani huyu KadaMpinzani yuko all over na analeta tu mambo ya sisiemu? hii JF imekosa mwelekeo. BTW mbona watu wanakuwa banned kisha wanarudi na majina mengine?
 
Ngoja na mimi nianze kupondea JF kama wanasisiem hapa

yaani inakuwaje sasa hivi ni wanasisiemu tu ndio wanachangia hapa kwenye mtandao? inabidi kuwe na balance? hii JF inaanza kukosa muelekeo sasa, mbona hakuna vyama vingine hapa?

yaani huyu KadaMpinzani yuko all over na analeta tu mambo ya sisiemu? hii JF imekosa mwelekeo. BTW mbona watu wanakuwa banned kisha wanarudi na majina mengine?

We lete vitu vyako, kama umeona wana CCM wamewazidi nguvu upinzani ni mtazamo wako na fikra zako.

Lete fikra mmbadala na endelevu na wewe shabikia chako kama kimeleta lolote hapa Tanzania!

CCM ipo JUUUUUUUUU!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom