Live: Kizota Dodoma

Huenda kuna mengi yamefichika kwa huyu mwanadada mahiri, tusubiri tu. Aliyeomba kura na kusema hajazunguka mikoani hajapita. Tazama matokeo ktk uk wa 34 wa thread hii.

yapi yamefichika?inaonekana una habari..lete info
 
Kumbe kuna watanzania wengine wana uraia wa nchi mbili siku hizi? This is news to me.

Huku ni kughushi kwingine! Kesi itapoanza itabidi atangaze ana uraia wa nchi gani. Akisema Tanzania basi moja kwa moja hatakuwa tena Raia wa uingereza. Akisema uingereza moja kwa moja hatakuwa raia wa Tanzania. Na hapa mjadala wa kisheria utaibuka, anashtakiwa kama raia wa nchi gani(maana uraia unatanabihisha vile vile aina ya mfumo wa kisheria utakaotumika na mahali gani). Inaweza pia kutazamwa ni uraia upi aliupata karibuni zaidi ya mwingine. Lakini kama alikuwa anatumia uraia yote miwili kwa wakati mmoja basi anakesi ya kujibu ya kughushi ama utapeli kwa mujibu wa sheria zetu. Kama habari ilivyoandikwa ndivyo hali halisi ilivyo

JJ
 
I think there's something wrong with Bhanji, sio bure. Yaani yeye anabwagwa kila uchaguzi. She ought to think twice before contesting!
Bado tu wakati wake haujafika watampa tu,Mfano hai Asha Baraka amejaribu mara nyingi Chamani na hadi kwenye Nafasi ya ubunge anapigwa chini tena Mara zote kwa Kura Chache Safari hii kajimwaga tena na kapata! Kujikwa si kuanguka hata iwe mara kadhaa wa kadhaa.
 
Uwaziri sio urais wa Tanzania, hayo tumeyaona toka enzi za Mkapa maana angalau Mwinyi hakuingia kwa mikogo, aliingia kimya kimya na kuondoka kimya kimya,

Tatizo ni Mkapa na Muungwana, walioingia kwa mikogo mingi, mimi mpaka leo sielewi huko juu kuna nini, maana wakiwa chini wanakuwa na maneno mengi mazuri, lakini wakifika tu basi wanakuwa mabubu,

kabla ya kuingia Ikulu, kuna siku nilikaa chini na Muungwana, ambapo aliniambia kwa uchungu jinsi alivyochoshwa na viongozi wazee, na kanipa mfano clear wa Kibaki, kwamba kazi yake ni kulala tu na kukingiwa kifua na wasaidizi wake,

Alipoingia Ikulu tu, akamchagua Kingunge, ambaye alishaamua kustaafu, na sasa Msekwa, kwa hiyo mkuu wangu huko Ikulu kuna something sijui ni nini kinachowabadili mawazo once wakiingia tu huko! Lakini kabla ya kuingia wanakuwa na maneno mengi mazuri!
Mtu wa makamo ES ; nimekupata uzuri kabisa. Narejea moja ya shule ulizojitahidi kutupatia huko nyuma,umetufundisha kufahamu President ni mtu Presidency ni Taasisi. Jana amewaeleza watanzania wote ktk mkutano mkuu,anasema wanadamu wako ktk makundi manne ya rika, nayo ni Watoto,Vijana,Makamo na Wazee; ameendelea kusema kuwa yeye na Karume ni watu wa Makamo hivyo walihitaji mtu wa rika la Uzee kuwasaidia. Niseme tu amejieleza vya kutosha na ni imani yetu kuwa sisi watu wa kawaida tumemuelewa. Jana Huyu Mkubwa alirejea vita aliyopigwa yeye kabla hajakaa kiti kile huko nyuma,hakujitaja bali ujumbe ulikuwa wazi sana.

Kurejea hoja ya kuna nini kule Ikulu mpaka hawa jamaa wanabadilika nadhani jibu ni watu wa aina yako Mkuu ES,maana wewe mwenyewe ni mtu wake wa karibu na ulimnnukuu akisema yeye na wazee ni tofauti lakini nadhani kitu kimoja mnakisahau kuwa yeye ni Rais na kazi yake ni Presidency ambayo ana mamlaka nayo kwa asilimia nyingi lakini kwa kutegemea ushauri wenu wakuu,tukubali tu kuwa anajitahidi kadri awezavyo lakini si rahisi kwake kubadili mwuelekeo wa nchi kwa 5yrs tu,mind u CCM hasa ni ile atakayoileta 2012 maana ina jukumu la kmzalisha mrithi wake.

Usikate tamaa,mshaurini kwa dhati ya roho zenu ,atawasikia lakini pia ni haki na wajibu kwake kuwa karibu na wazee.
Natoa hoja
 
MNATAKA MUUNGWANA AFANYE NINI ZAIDI YA HAYA???!!!

Kaka FD,

Pole sana, Watanzania wanataka Rais ambaye ni Jaji Mkuu hapo hapo, na pia awe na mamlaka ya kuwa Kamanda wa Magereza ili mambo yaende kwa kasi ya mwanga wa jua!!!!

Pole sana:::

Mimi nilimsikiliza Mheshimiwa Rais, kwa ujumla alijibu mambo mengi sana ikiwa pamoja na lile lililompa Mh. Zitto Umaarufu mkubwa kwa upuuzi wetu!!!

Kwa mfano,,, Mh. Rais amesema Waziri hana mamlaka ya kubadilisha hata kifungu kimoja kwenye mkataba wa madini, kila kilichopo kule aidha kiko kwenye sheria ya madini au ya kodi; Akasema lile lilomfanya kusema ku-review mikataba iliyokuwa ile 15% ya corporate tax ambayo makampuni mengi yanamekubali kuondoa kifungu hicho,,, na kwenye mkataba wa Buzwagi haikuwepo pia, hivyo Mh. Karamaji hakukosea kitu chochote,,, Mh. Zitto amesikia hotuba ya Rais naomba atoke kimasomaso aje kutuambia kwamba kuna hoja kweli lile alilokuwa analipigia kelele Bungeni?

Tuacheni mambo ya kufanya vitu jumla jumla, twende hoja kwa hoja!!!
 
Haya tuendelee na kumkoma nyani giledi...
Kilitime na FD, wajomba mbona majina ya wasomi wengi yametupwa nje?...

Mheshimiwa Mkandara,

Nina jibu moja katika hili, kwamba viongozi wanatokana na jamii! composition ya jamii ina wasomi, wasanii, wasiosoma etc...

Mwanzoni, binafsi nilikuwa nabata shida sana kujua kwa nini John Komba na Khadija Kopa wachaguliwe kwenye NEC!

Lakini ukweli unarudi pale pale jamii yetu ni duni kwa mambo ya elimu, kwa hiyo Wajumbe wa Mkutano mkuu wapo wengi ambao hawana uwezo wa kutofautisha darasa la 12, 14, stashahada, shahada, shahada ya uzamili, na shahada ya falsafa... kwa hiyo kwao hakuna tofauti ya Dr. Mathayo na Mh. John Komba...

Jamii ya walarushwa inazaa viongozi walarushwa pia, rushwa ya CCM, mzizi wake uko kwenye jamii ndio maana mwenyekiti wa TCD, Mzee John Cheyo alisema wazi kwamba CCM ikishindwa kukemea rushwa,,, vyama vya upinzani ndio itakuwa tatizo kubwa... so... twendelee hivi hivi ndio jamii yetu!!!

Na niwazi pia kwamba kuimarika kwa upinzani lazima kutokane na CCM, kwa hiyo CCM ikiwa na wara rushwa wengine watatoka hapo, watapenyeza upinzani kwa vigezo vingine kumbe ndio hivyo tena mshiko haupatikani vizuri,,, wakifika huko wakipata ngoma rushwa ngoma mdundo....
 
Huku ni kughushi kwingine! Kesi itapoanza itabidi atangaze ana uraia wa nchi gani. Akisema Tanzania basi moja kwa moja hatakuwa tena Raia wa uingereza.
JJ

Mnyika,

Hiyo statement sio sahihi, akisema yeye ni raia wa Tanzania, hawezi kupoteza uraia wa Uingereza. Kupoteza uraia wa Uingereza ni kugumu mno na pia muda wowote ukitaka kuurudisha unarudisha kirahisi.

Hapo wanachofanya ni kupoteza uraia wa Tanzania, lakini akifanya hivyo basi tayari ataanza kupata protection ya Uingereza.

Mtu akiwa na uraia wa nchi mbili na kufanya kosa kwenye nchi moja, basi protection ya ile nchi nyingine huwa haifanyi kazi.

Itakuwa vizuri kumhukumu akiwa Mtanzania kuliko kumnyang'anya uraia wa Tanzania maana hapo anaweza kufaidika kwa protection ya UK, ikiwemo right ya kuonana na balozi wake, akipigwa kidogo tu, tayari JK atapata habari.
 
Mheshimiwa Mkandara,

kwa hiyo Wajumbe wa Mkutano mkuu wapo wengi ambao hawana uwezo wa kutofautisha darasa la 12, 14, stashahada, shahada, shahada ya uzamili, na shahada ya falsafa... kwa hiyo kwao hakuna tofauti ya Dr. Mathayo na Mh. John Komba...

Nakubaliana na wewe kwenye hili, wajumbe wa NEC ni kama kioo cha jamii...ila mfano uliutoa una walakini Dr Mathayo si msomi hana tofauti na Mh Komba ...nadhani unajua hilo. Dr Chenge na Mh Komba, ama Prof Mwakyusa na Mh Komba
 
Huku ni kughushi kwingine! Kesi itapoanza itabidi atangaze ana uraia wa nchi gani. Akisema Tanzania basi moja kwa moja hatakuwa tena Raia wa uingereza. Akisema uingereza moja kwa moja hatakuwa raia wa Tanzania. Na hapa mjadala wa kisheria utaibuka, anashtakiwa kama raia wa nchi gani(maana uraia unatanabihisha vile vile aina ya mfumo wa kisheria utakaotumika na mahali gani). Inaweza pia kutazamwa ni uraia upi aliupata karibuni zaidi ya mwingine. Lakini kama alikuwa anatumia uraia yote miwili kwa wakati mmoja basi anakesi ya kujibu ya kughushi ama utapeli kwa mujibu wa sheria zetu. Kama habari ilivyoandikwa ndivyo hali halisi ilivyo

JJ

Nadhani anashtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi anakoshtakiwa, bila kujali uraia wake, kwa mujibu wa sheria inayoendana na kosa analotuhumiwa mahali pale. Katika charge sheet, mwendesha mashtaka ni lazima ataje ni sheria gani mtuhumiwa anadaiwa kuivunja, ya nchi gani. Au mnasemaje wanasheria?
 
...............Mimi nilimsikiliza Mheshimiwa Rais, kwa ujumla alijibu mambo mengi sana ikiwa pamoja na lile lililompa Mh. Zitto Umaarufu mkubwa kwa upuuzi wetu!!!

Kwa mfano,,, Mh. Rais amesema Waziri hana mamlaka ya kubadilisha hata kifungu kimoja kwenye mkataba wa madini, kila kilichopo kule aidha kiko kwenye sheria ya madini au ya kodi; Akasema lile lilomfanya kusema ku-review mikataba iliyokuwa ile 15% ya corporate tax ambayo makampuni mengi yanamekubali kuondoa kifungu hicho,,, na kwenye mkataba wa Buzwagi haikuwepo pia, hivyo Mh. Karamaji hakukosea kitu chochote,,, Mh. Zitto amesikia hotuba ya Rais naomba atoke kimasomaso aje kutuambia kwamba kuna hoja kweli lile alilokuwa analipigia kelele Bungeni?

Tuacheni mambo ya kufanya vitu jumla jumla, twende hoja kwa hoja!!!

Unajua mambo mengine msiwe mnachukulia kirahisi rahisi, wakti kuna hoja NZITO

Kilitime ....hivi ulishawahi kusoma maelezo ya Prof Shivji kuhusiana na hoja ya Mh Zitto na kweli ukaona JK kajibu hoja inayompatia umaarufu Mh Zitto!!!!......................sijui kaijibiwa wapi....................hebu tufungue macho niwapi alipoijibu

Kilitime......unapaswa kuelewa hii vita yetu........tunataka Mikataba yenye manufaa Kwa taifa iwe wazi at least wabunge wetu wakihitaji kuiona na waione...............kwani wale ndio wawakilishi wetu.

Kilitime........yes Waziri hana mamlaka ya kubadili mkataba......hivi Karamagi alifanya nini kule Uingereza with his "Ball Pen"

Noo man !..................................JK naona ni mpole sana hata kuliko Mwinyi na Mkapa

Hivi kweli inaingia akilini only 1.9% (FD reported) ndio mchango wa madini ktk pato la Taifa!!!???

Hivi lile neno la kumuwajibisha mtu kwa manufaa ya umma liliishia wakati wa Rais Mwinyi tu na haliko tena ktk lugha yetu!!....................ina maana hivi sasa ndio tuna viongozi Safi sana kuliko wakti ule eehh!!........................siku hizi akina Karamagi wanapeta tu!!

Anyway...........we have a long way to go kama hata sisi hapa JF tutakuwa tunakubali majibu rahisi rahisi namna hiyo
 
Put your self in Muungwana's shoes. What would you do on fighting corruption? what are your basis for that decision?.

Tunahitaji kuijadili point hii (FD) ili kumsaidia JK. najaribu kufikiri kwamba:

Huyu/hawa ndiyo rafiki zangu wa karibu mno nashinda na ninakula nao siku zote.
ndiyo wananijua in and out,
ndiyo kwa kiasi kikubwa wamenifanya niwe Rais kupitia midomo yao, magazeti/media zao na hata pesa zao, bila wao leo nisingeitwa Rais.

Leo hawa ndiyo wanatuhumiwa mafisadi na ushahidi una mazingira ya ukweli ndani yake.

Nasikia kichwa kinauma
 
Mpaka jioni hii, utawala wa juu kwenye site yao huu hapa: Jamaa wanaendelea na usingizi mzito

leaders_kiswahili.jpg
 
Kilitime: acha kidogo ukada; hebu soma maelezo ya Ogah hapo juu. Kuna hoja nzito ulizochokoza ambazo nafikiri unastahiki kuzijibu mkuu!
 
Unajua mambo mengine msiwe mnachukulia kirahisi rahisi, wakti kuna hoja NZITO

Kilitime ....hivi ulishawahi kusoma maelezo ya Prof Shivji kuhusiana na hoja ya Mh Zitto na kweli ukaona JK kajibu hoja inayompatia umaarufu Mh Zitto!!!!......................sijui kaijibiwa wapi....................hebu tufungue macho niwapi alipoijibu
Hivi ulimsikiliza Kikwete,,, mkataba umeuona,,, unaweza kutuwekee kipengele ambaco kimeenda tofauti na sheria iliyoko sasa?

Kilitime......unapaswa kuelewa hii vita yetu........tunataka Mikataba yenye manufaa Kwa taifa iwe wazi at least wabunge wetu wakihitaji kuiona na waione...............kwani wale ndio wawakilishi wetu.
Kweli kabisa na rais amesema anaomba hiyo tume itakayokuwa inasheheni wataalamu na upande wa upinzani ulilete hiyo formula mpya,,, iliyopo ndio aliyotumia waziri,,, so no wrong doing otherwise please leta hapa!

Kilitime........yes Waziri hana mamlaka ya kubadili mkataba......hivi Karamagi alifanya nini kule Uingereza with his "Ball Pen"
Nimesema waziri hana mamlaka ya kutoa kodi au kuongeza kodi kwa mwekezaji yeyote, zote lazima zitoke kwenye sheria ya madini au ya fedha... full stop... in other words waziri hana power ya nkunegotiate... hili ndilo alilosema Rais. Ni kodi gani ambayo Mwekezaji amesamehewa na Waziri wakati iko kwenye sheria,,, ilete hapa tuchambue?

Noo man !..................................JK naona ni mpole sana hata kuliko Mwinyi na Mkapa
Hii nakubaliana nayo, kwani alishasema katika mambo anayo-regret ni kumwonea mtu... naye hakupenda kumuadhibu Karamaji kwa kosa la bunge kutunga sheria mbaya,,, does it make sense to you... waziri awajibike kutekeleza sheria ya bunge kama ilivyo....
Hivi kweli inaingia akilini only 1.9% (FD reported) ndio mchango wa madini ktk pato la Taifa!!!???

Mzee Rais alisema kwamba mchango wa Madini kwenye Pato la Taifa ni 1.9%,,, lakini kwenye suala la foreign currency ni asimilia nyingi kidogo sikumbuki kama alitaja numba kamili,,, lakini kama una-another source yenye authority ya hiyo information ambayo itakuwa tofauti na hii tuletee!!! simple

Hivi lile neno la kumuwajibisha mtu kwa manufaa ya umma liliishia wakati wa Rais Mwinyi tu na haliko tena ktk lugha yetu!!....................ina maana hivi sasa ndio tuna viongozi Safi sana kuliko wakti ule eehh!!........................siku hizi akina Karamagi wanapeta tu!!
Kumuwajibisha mtu kwa manufaa ya umma lipo,,, lakini sharti uwe na mkosaji...

Anyway...........we have a long way to go kama hata sisi hapa JF tutakuwa tunakubali majibu rahisi rahisi namna hiyo

Sure we do! especially kama sisi tunabeba mambo juu juu tu!!! kosa la bunge unamwazibu waziri, kosa la waziri unamwazibu kilitime...
 
Kilitime: acha kidogo ukada; hebu soma maelezo ya Ogah hapo juu. Kuna hoja nzito ulizochokoza ambazo nafikiri unastahiki kuzijibu mkuu!

Mzee Kilitime na Ukada wapi kwa wapi kaka yangu!!! Nilishasema niko Huru mkuu!!! Ndio maana nachambua kama karanga pande zote!!!
 
Makamba -secretary general

Amos Makala-FEdha

Kidawa-Oganizainesheni

Membe-Mahusiano ya mambo ya nje

Source:Nchimbi
 
[/SIZE]

???????????????

ndio manaake,wewe ulitaka nani awe,Makambna anakipenda chama ..mapenzi yake yote yako katika chama,unajua kwanini makamba alisema I lvoe CCm?anajua uwezo wake kichwani ni mdogo na akimwaga na chama hana pa kukimbilia,kwa kifupi ni kilaza
..viongozi wa nmana hii ndio maana tunaendela kuwa masikini
Kwi kwi kwi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom