Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Pia baada ya kupiga kura nimeenda kazini kwangu, ambako pia kuna kituo, jambo la kushangaza ni kuwa kituoni hapo mabox yote ni ya rangi nyeupe(mifuniko), na sijui discrepancy hiyo inaelezwaje!(sijanote utofautishaji wowote), na nilipouliza wakasema kuwa yameletwa yakiwa hivyohivyo, huenda ndio ukosefu wa vifaa wenyewe..nahofia sana kura hizo kuharibika, maana zitachukuliwa kuwa zote ni za Mbunge, kumbe zingine ni za Rais!

Hii hatari sana. lakini nadhani wanaweza wakayaandika na marker pens. Zanzibar nimeona masanduku yameandikwa.
 
Vijana this time wameushangaza Uma, ni wengi sana tofauti na ilivyotegemewa

Ni kweli NDU, mimi nimewakuta vijana wengi sana tofauti na 2005. Nimeshuhudia akina dada wawili wakiwapigia wenzao mbalimbali wakiwahimiza waamke kuja kupiga kura. Watu wako gado.
 
dw swahili wamesema kuwa kuanzia saa kumi askari atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho na watakaokuja baada ya hapo hawataruhusiwa kupiga kura.so wakuu shime tuwahi kufika vituoni kabla ya saa kumi ( habari kutoka visiwani)
 
Ni kweli NDU, mimi nimewakuta vijana wengi sana tofauti na 2005. Nimeshuhudia akina dada wawili wakiwapigia wenzao mbalimbali wakiwahimiza waamke kuja kupiga kura. Watu wako gado.

Huu mwamko wa Vijana unampa BP Mama Salma Kikwete maana anajua kura nyingi za vijana zitaenda kwa Dr. Slaa.
 
Kwa wenzangu waliopiga kura nina swali moja, Je wamegundua kitu gani kuhusu karani anayekunja karatasi za kura? Kwetu alikuwa na story nyingi na maelekezo ya jinsi ya kupiga kura. Kinachostua ni kuwa akionesha jinsi ya kupiga kura kidole chake kinakuwa tooooooo partisan and partial. Kanionesha karatasi ya kwanza ( it was too suggestive) nikamgombeza nikadhani ataelewa, akanipa ya pili ( he was instructive) nikamfokea akakaa kimya hakurudia.

Wenzagu nipeni expirience yenu kwenye hilo.
 
Kasoro ndogondogo kama hizo zinaweza kurekebishwa na wasimamizi wenyewe si mpaka watu waanze kupiga kelele au maagizo toka tume ya uchaguzi.
 
Prof. Lipumba - Dira ya Mabadiliko kapigia Kura Mbagala.

attachment.php

Usalama sehemu nyingi kama kawa:

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00011.jpg
    DSC00011.jpg
    32.2 KB · Views: 137
  • DSC00012.jpg
    DSC00012.jpg
    37.1 KB · Views: 139
  • DSC00013.jpg
    DSC00013.jpg
    34.5 KB · Views: 130
Morogoro pia hali inaripotiwa kuwa ni shwari ila kwa sasa watu ni wachache sana ikilinganishwa na asubuhi.
 
dw swahili wamesema kuwa kuanzia saa kumi askari atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho na watakaokuja baada ya hapo hawataruhusiwa kupiga kura.so wakuu shime tuwahi kufika vituoni kabla ya saa kumi ( habari kutoka visiwani)

Ukizungukwa na majuha na wewe unakuwa juha well habari kutoka visiwani chadema imepamba moto na ushindi ni mkubwa sana tulinde kura zetu tu CUF wasije kutuibia.
 
dw swahili wamesema kuwa kuanzia saa kumi askari atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho na watakaokuja baada ya hapo hawataruhusiwa kupiga kura.so wakuu shime tuwahi kufika vituoni kabla ya saa kumi ( habari kutoka visiwani)

Hiyo ni kwa sheria gani Mkuu. Maana mwisho wa kufunga kituo ni saa 12 jioni.
 
Chalinze Pwani hali inaripotiwa kuwa ni tulivu sana. Shule ya msingi Msoga ndipo JK atapiga kura yake.
 
Rizwani Kikwete akihojiwa baada ya kupiga kura.

Anadai suala la Wanachuo kushindwa kupiga kura kwenye vituo vyao limekuzwa kisiasa kwani walijulishwa toka mwezi wa 4. Wanapaswa kwenda kutumia haki yao.
 
Hiyo ni kwa sheria gani Mkuu. Maana mwisho wa kufunga kituo ni saa 12 jioni.

huo ndio utaratibu mkuu, labda hujamuelewa Nyani vizuri
ni kweli kupanga mstari mwisho ni saa kumi jioni, yaani ikifika saa kumi askari anapanga mstari kwa mtu wa mwisho, hivyo mtu atakayekuja na kumkuta police kwenye folen basi imekula kwake, ila kupiga kura mwisho ni saa kumi na mbili, kwa hiyo huo mstari uliozuiliwa na police utaenda mpaka saa kumi na mbili
 
Jakaya Kikwete ndo anaingia sasa kupiga Kura saa 5.40 asubuhi.
 
Back
Top Bottom