Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Haaa haaa, sikuinote hiyo. Nadhani ni ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Sijajua kama bendera ya CCM ni sawa kuwa hapo.

Ofisi ya serikali ya mtaa ni ofisi ya SERIKALI parsee, haitakiwi kuwa na bendera ya chama fulani, zaidi ya ile ya Taifa....Hapo ni makosa ya kimsingi(kama kweli ni bendera ya ccm), na inatakiwa ikaondolewe haraka kabla haijaathiri watu wengi zaidi...Hata kama hiyo ni ofisi ya ccm, kwa leo inatumika kwa tukio la kitaifa ambalo ni la neutral ground.
 
PJ, vipi mambo huko A-Town?
A-Town kuko shwari sana...Hakuna fujo, hakuna magari barabarani, watu wote wamekimbilia vituoni, wako serious mno.
Mimi nilipiga kura yangu saa 1.20 kwa usalama kabisa.
Ila chumba kilichokuwa adjacent na mimi walisimamisha upigaji baada ya kama watu 10 kupiga, maana iligundulika kuwa wapigisha kura walikosea kupanga yale mabox ya kutumbukiza kura... walipanga sanduku jeusi kwa rais, na la bluu kwa Mbunge, ambapo ni makosa...sasa sijui hatima ya kura zile itakuwaje!..niliacha kadhia hiyo bado haijapata uFumbuzi.
 
Kuna thread kama kumi zote LIVE kuhusu uchaguzi. Kama kuna MOD yeyote atakayepita hapa, ningeshauri zooooote ziunganishwe na thread hii. Superman, we si MOD ....au!?
 
Baada ya briefing ya hapo juu, sasa naamia katika TV's kuwapa updates: ITV wako Live wanaohoji waandishi sehemu mbalimbali, , TBC pia wanarusha matangazo; , Channel 10 nao wako hewani na Star TV pia.

. . . . . . .

Mkuu Superman
tunashukuru kwa updates, endeleeni kutujuza, tuko pamoja
 
Pia baada ya kupiga kura nimeenda kazini kwangu, ambako pia kuna kituo, jambo la kushangaza ni kuwa kituoni hapo mabox yote ni ya rangi nyeupe(mifuniko), na sijui discrepancy hiyo inaelezwaje!(sijanote utofautishaji wowote), na nilipouliza wakasema kuwa yameletwa yakiwa hivyohivyo, huenda ndio ukosefu wa vifaa wenyewe..nahofia sana kura hizo kuharibika, maana zitachukuliwa kuwa zote ni za Mbunge, kumbe zingine ni za Rais!
 
Mwanza kumekucha, umati mkubwa umejitokeza kupiga kura kiasi kwamba wana usalama wana kazi ya ziada.

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00005.jpg
    DSC00005.jpg
    25.3 KB · Views: 147
Kuna thread kama kumi zote LIVE kuhusu uchaguzi. Kama kuna MOD yeyote atakayepita hapa, ningeshauri zooooote ziunganishwe na thread hii. Superman, we si MOD ....au!? [/QUOTE]
Hahahaaaa!
Mkuu, unamhisihisi jamaa amekaa kimod-mod eeh?
All in all, kweli hizi threads nyingi ziunganishwe...kuna watu humu wana namba za Invisible na PianKiller, hebu muwa-'DIPU':becky::becky:

Star TV wanaripoti kuwa Masanduku ya kupigia kura yamechangwa vituo.

Na pia kuna watu walirudishwa kwa kwenda kituoni na sare za chama.
 
Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro hali ni shwari isipokuwa nako baadhi ya watu hawajaona majina yao.
 
JK Anapigia Kura Msata
Rungwe kapigia Mikocheni
Dr. Slaa Karatu
 
Mgombea Uraisi kupitia ticketi ya NCCR-Mageuzi, Hashimu Rungwe akiwa na mjukuu wake katika kituo cha kupiga kura.

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00006.jpg
    DSC00006.jpg
    31.2 KB · Views: 141
  • DSC00007.jpg
    DSC00007.jpg
    33.8 KB · Views: 142
Charambe Mbagala, baadhi ya vituo bado vimechelewa kufunguliwa.
 
A-Town kuko shwari sana...Hakuna fujo, hakuna magari barabarani, watu wote wamekimbilia vituoni, wako serious mno.
Mimi nilipiga kura yangu saa 1.20 kwa usalama kabisa.
Ila chumba kilichokuwa adjacent na mimi walisimamisha upigaji baada ya kama watu 10 kupiga, maana iligundulika kuwa wapigisha kura walikosea kupanga yale mabox ya kutumbukiza kura... walipanga sanduku jeusi kwa rais, na la bluu kwa Mbunge, ambapo ni makosa...sasa sijui hatima ya kura zile itakuwaje!..niliacha kadhia hiyo bado haijapata uFumbuzi.

Du! Mbona wamechemsha sana?

Bila ya shaka wasimamizi na mawakala wanaweza wakarekebisha hilo.
 
Vijana this time wameushangaza Uma, ni wengi sana tofauti na ilivyotegemewa
 
Kuna thread kama kumi zote LIVE kuhusu uchaguzi. Kama kuna MOD yeyote atakayepita hapa, ningeshauri zooooote ziunganishwe na thread hii. Superman, we si MOD ....au!?

Mkuu, ombi lako nilmelifikisha kwa Invisible. Mimi siyo MOD Mkuu.
 
Back
Top Bottom