Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,491
- 2,104
Hivi Watanzania ni nani aliyeturoga? Kwenye hiyo link ya www.4icu.org UDSM iko nafasi ya 15 na Hubert Kairuki Memorial University iko nafasi ya 48 hebu linganisha na hii orodha yako, tutaendelea na uchakachuaji hata lini?
Nionavyo mimi huu siyo wakati wa kutambiana ni chuo gani bora kuliko kingine. Tukubali kwamba vyuo vyote vimeidhinishwa kutoa elimu ya juu baada ya kukamilisha vigezo vinavyotakiwa. Sasa graduates wote tuungane kila mtu kwa fani yake kuleta maendeleo katika nchi yetu. Nchi iko taabani kiuchumi huku wasomi wakibishana chuo gani ni bora na chuo gani si lolote. Tunahitaji digrii zetu zichangie katika kuondoa umaskini hapa nchini. Tumia kila mbinu kuhakikisha digrii yako inachangia maendeleo na siyo kukaa tu ukijisifu umesoma chuo bora huku huoneshi tofauti na mtu hata aliyeishia darasa la saba, inawezekana yeye akakuzidi kwa sababu alifundishwa kupanda mazao shambani kwa mstari na sasa elimu hiyo anaitumia kuongeza tija katika kilimo. Je wewe hiyo digrii yako unaitumiaje? Inawezekana una digrii ya kilimo lakini hutaki kwenda kijijini kuwsaidia wakulima eti kwa kuwa wewe ni msomi! Tubadilike jamani.