Lissu amlima barua Shibuda

Uroho wa madaraka ndo unamsumbua alihamia CHADEMA ili apate Ubunge baada ya kuangushwa vibaya na CCM sasa anaona Magambani kwake ni kuzuri anatamani kurudi wajameni kha!! Vyeo hivi balaa tupu

Uroho wa madaraka siyo kuwa na roho ya madaraka?!
 
Kwa hiyo ametumwa na wapiga kura wake kwenda bungeni kutetea wabunge waongezewe posho kufikia laki tano kwa siku?! haya ni matusi kwa wapiga kura ambao wanahangaika huku na huko kupata mlo mmoja wa siku.

Leo asubuhi Mh. magdalena Sakaya kasema kimsingi wabunge wote pamoja na wa CDM wameisha chukua hiyo posho in advance wanacho fanya ni ku-sign karatasi tuu, tunaomba muongozo wa waheshimiwa wabunge wa CDM je, ni kweli?
 
Asiyepokea posho na awe wa kwanza kumfukuza mwenzake, pia naomba kuuliza hivi Shibuda ndiye wa kwanza kukiuka kile kinachoitwa sera au msimamo wa chama? Je tuamini kuwa kuna watu CHADEMA inaogogopa kuwagusa kwa kuhofia kubomoka iwapo itathubutu kuwagusa? Nahitaji tu kufahamishwa ili twende sawa.
 
HAKUNA JIPYA!
Tuliyaona zamani tukasema,
si majembe ni magalasa,
si vitu halisi ni kanyaboya,
msivitegemee kwa maana ni bandia!
Tukapewa majina na kuonekana wasaliti na tusiopenda maendeleo!
ama kweli kusadiki wa toma kujionea!!
 
Ndugu zangu, taifa hili limeyumbishwa na mamluki wa CCM kwa mda mrefu.Cha msingi nchi yetu sasa inahitaj msimamo wa pamoja wenye maslah kwa watanzania,CDM na CCM wawajibikie uzalendo,taifa lipate ahueni.Tuache malumbano na ushabiki,uungwana ni vitendo!
 
cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka

Hujui siasa wewe, Shibuda hakuhoji CDM, alipingana na msimamo wa pamoja wa kambi nzima ya upinzani. Kama hawezi kushikamana na wenzake inatakiwa aonyeshwe mlango wa kutokea, aende huko anakutetea. Siasa siyo lazima aifanyie CDM aende hata CCJ kwa akina Nape!
 
Chadema mnapaswa kuonyesha njia ya jinsi ya kutoa maamuzi magumu... Kusema kwamba kukubali posho ni msimamo wake kibinafsi ni sawa, lakini cha kujiuliza yale maneno yake ya kushambulia chama na viongozi wake ni msimamo wake pia? fukuzeni shibuda, tunasema fukezeni. Tangazeni jimbo kuwa wazi, na jipangeni kwa uchaguzi mdogo. Ni afadhali jimbo lichukuliwe hata na shetani kuliko msaliti ndani ya kambi.
.

Nakuunga mkono dogo, Shibuda ni GAMBA baya, libandueni bado asubuhi, likipigwa jua likakauka kulibandua litatoka na ngozi. FUKUZILIA MBALI-Heri nusu shari kuliko shari kamili!
 
kwa kweli inauma sana tunapojinyima kuwachangia watu kama huyu mjinga shibunda pesa za
kampeni kmbe yupo kwa ajili ya tumbo lake si kwa ajili ya wananchi
 
Leo asubuhi Mh. magdalena Sakaya kasema kimsingi wabunge wote pamoja na wa CDM wameisha chukua hiyo posho in advance wanacho fanya ni ku-sign karatasi tuu, tunaomba muongozo wa waheshimiwa wabunge wa CDM je, ni kweli?
CHADEMA wathibitishe nini tena hapo, Mnyika alishasema hela ya posho inaenda moja kwa moja kwenye akaunti zao, na hakuna aliye cash the posho na kurudisha. Sasa Lissu na CHADEMA watuambie, utasemaje sera ya chama ni kupinga posho, na asiyepinga tunamfukuza chama, halafu unapewa posho unakula?
 
Bora shibuda hakutaka kujificha ktk hili wengine wote wanafki
CHADEMA wathibitishe nini tena hapo, Mnyika alishasema hela ya posho inaenda moja kwa moja kwenye akaunti zao, na hakuna aliye cash the posho na kurudisha. Sasa Lissu na CHADEMA watuambie, utasemaje sera ya chama ni kupinga posho, na asiyepinga tunamfukuza chama, halafu unapewa posho unakula?
 
Aliwaona wanafki ndo mana akajilipuaz coz pesa wameshachukua alafu wanapinga nn,ntafurah mkimfukuza shibuda coz maovu yenu yote yatakuwa hadhar no secret tena
Hujui siasa wewe, Shibuda hakuhoji CDM, alipingana na msimamo wa pamoja wa kambi nzima ya upinzani. Kama hawezi kushikamana na wenzake inatakiwa aonyeshwe mlango wa kutokea, aende huko anakutetea. Siasa siyo lazima aifanyie CDM aende hata CCJ kwa akina Nape!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom