Lissu amlima barua Shibuda

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
SIKU chache baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA) kupingana na msimamo wa chama hicho kwa kuunga mkono posho, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, amesema chama hicho kiko tayari kwa lolote kuhusu mbunge huyo.

Lissu aliyasema hayo ofisini kwake jana alipotakiwa kuzungumzia kuhusu hatima ya mbunge huyo.

“Namwandikia barua leo kumtaka aeleze kwa nini msimamo wake ulikuwa kinyume cha wa kambi ya upinzani na kama yupo tutamkabidhi leo, baadaye tutalipeleka kwenye Kamati Kuu ya CHADEMA yenye nguvu ya maamuzi, ikiwamo kumfukuza uanachama.

“Tuko tayari kwa lolote kuhusu Shibuda hata kwenda kwenye uchaguzi mdogo, kama anaona CHADEMA ni mbaya arudi alikotoka au kama ataona atageuka jiwe, atafute sehemu nyingine ya kwenda,” alisema Lissu.

Alisema wao binafsi hawawezi kuchukua uamuzi wa kumfukuza Shibuda zaidi ya kutangaza kumtenga, bali wenye uamuzi huo ni kamati kuu ya chama.

Alisema baada ya kuwasilisha utetezi wake kabla ya kumpeleka kwenye kamati kuu watakaa kwanza na kumjadili na kuchukua hatua dhidi yake, kwani suala hilo liko wazi.

Kuhusu mabaya ambayo Shibuda anayaendeleza kuhusu CHADEMA, Lissu alimtaka ayaendeleze na kumponda kuwa hana kipya zaidi ya kuzungumza ‘matapishi.’
“Shibuda hana chochote kipya zaidi ya matapishi ya wale wa jana na juzi waliokuwa wakisema kuwa CHADEMA ni cha familia ya Mtei (Edwin) na mkewe Mbowe, ni cha Wachaga. Nje ya hayo sijui kama ana kipya,” alisema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu, mbunge huyo aliingia kwenye chama hicho mwaka jana alipopata ubunge na kwamba hakuna anachokijua kuhusu chama hicho.

Wakati akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wiki iliyopita, Shibuda alikigeuka chama chake (CHADEMA) kuhusu posho akitaka ziongezwe hadi kufika sh 500,000.

Shibuda alikwenda mbali zaidi na kumtaka waziri mkuu kufanyia kazi haraka ongezeko hilo la posho, ambalo alilibatiza jina la ujira wa mwia.
 
Shibuda ni gamba mlimwingizaje huko?
Huyu mtu ni nyoka hafai kabisa . Mpeni talaka tatu
 
cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka
 
We hujui kama ukubwa ni jalala takataka zote utatupiwa wewe.
 
Yani shbuda ni kama Mtkila hapaswi kuaminiwa, cha msingi hili jambo linaweza kuyumbisha chama na jambo muhimu Shibuda angekabiziwa kwa Mbowe kwani Anauwezo mkubwa wa ku'solve matatzo bila kuathiri mustakabali wa chama na mfano hai ni alivyomalza suala la Zitto siku alpogoma kushiriki kutoka nje JK alipokuwa anahutubia bunge.
 
"Namwandikia barua leo kumtaka aeleze kwa nini msimamo wake ulikuwa kinyume cha wa kambi ya upinzani na kama yupo tutamkabidhi leo, baadaye tutalipeleka kwenye Kamati Kuu ya CHADEMA yenye nguvu ya maamuzi, ikiwamo kumfukuza uanachama.

KATIBA YA CHADEMA

UANACHAMA:
5.1 Sifa za kuwa MwanaChama

5.1.1 Awe raia wa Tanzania.
5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi
5.1.3 Awe na akili timamu
5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.
5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama
.
5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.

Kupinga posho lilikuwa ni wazo la Zitto au ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

Na kama imeandikwa sehemu kwamba kupinga posho ni
Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA ni kwa nini Lissu asifukuzwe uanachama: Hivi tunavyoongea hapa Lissu anakula posho ya Wabunge, kwa sababu hakuna mtu hata mmoja aliyerudisha posho, uongozi wa Bunge na Serikali walikataa ku entertain kukataa posho, kupokea back posho ya mtu. Kwa hiyo Lissu anakula posho, afukuzwe CHADEMA kwa kukiuka Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?
 
ukiniambia Zito, shibuda au Lissu kdogo nitakusikilza lkn si kwa Mbowe

Hilo liko wazi Mbowe ni kisiki cha mpingo, si utani ndiyo maana wengi wanaona tatizo ni mbowe kwa sababu kijana yule yuko ''firm'' acha kabisa tena yule anatisha na ni mjenga hoja na anazisimammia kwa akili zote.Mtamchukia sana F.A.mBOWE hadi mtatapika.Shibuda must go na ndiyo atajua utamu wa sera za CDM kwani kwa sasa nje ya CDM hana umaarufu.
 
KATIBA YA CHADEMAUANACHAMA:5.1 Sifa za kuwa MwanaChama5.1.1 Awe raia wa Tanzania.5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi5.1.3 Awe na akili timamu5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama.5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga naAhsante mkuu kwa kutujuza.? Viongozi wakuu wa CDM wawe makini sana na hoja za Kibunda Msukuma. On my side swarp him away, he is lyk a bat.
 
we vipi wewe kwani hiyo nchi unawapa wewe? hebu nenda ukadai chenji ya radar huko hapa hapakufai

cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka
 
Shibuda ni mtu mnafiki tena mamluki. Nadhani hiyo itakuwa angalizo tosha kwa vyama vya siasa kwa siku zijazo kutokupokea watu ovyo ovyo hususani wale waliokataliwa na vyama vyao kwa sababu mbali mbali! Nadhani Shibuda avuliwe uanachama kisha aende akapige kelele Tanzania nzima kaonewa au ajiunge na Mrisho Mpoto kutunga na kuimba mashairi.
 
Hivi mbowe na kikwete nani anaonekana na IQ kubwa? nadhani dr aliyopewa kikwete haiendani na mambo anayofanya

ukiniambia Zito, shibuda au Lissu kdogo nitakusikilza lkn si kwa Mbowe
 
KATIBA YA CHADEMA

UANACHAMA:
5.1 Sifa za kuwa MwanaChama

5.1.1 Awe raia wa Tanzania.
5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi
5.1.3 Awe na akili timamu
5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.
5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama
.
5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.

Kupinga posho lilikuwa ni wazo la Zitto au ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

Na kama imeandikwa sehemu kwamba kupinga posho ni
Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA ni kwa nini Lissu asifukuzwe uanachama: Hivi tunavyoongea hapa Lissu anakula posho ya Wabunge, kwa sababu hakuna mtu hata mmoja aliyerudisha posho, uongozi wa Bunge na Serikali walikataa ku entertain kukataa posho, kupokea back posho ya mtu. Kwa hiyo Lissu anakula posho, afukuzwe CHADEMA kwa kukiuka Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

5.1.6 Ameacha chama kilicho mpa ubunge yuko pale kusimamia chama cha magamba
 
Yote mtasema badala yake mtajikuta hamna kitu mkononi. Mbona hamji na hoja za maendeleo nyie wanaCCM? hebu tuambieni tatizo la umeme litaisha lini? mnekuwa mnakuja na hoja humu tungewaeleweni lkn nyie mmebaki kujibizana na CDM tu. CCM ni kama dereva aliyeacha usukani wake na kuanza kubishana na abiria wake unategemea nini hapo?

KATIBA YA CHADEMA

UANACHAMA:
5.1 Sifa za kuwa MwanaChama

5.1.1 Awe raia wa Tanzania.
5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi
5.1.3 Awe na akili timamu
5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.
5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama
.
5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.

Kupinga posho lilikuwa ni wazo la Zitto au ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

Na kama imeandikwa sehemu kwamba kupinga posho ni
Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA ni kwa nini Lissu asifukuzwe uanachama: Hivi tunavyoongea hapa Lissu anakula posho ya Wabunge, kwa sababu hakuna mtu hata mmoja aliyerudisha posho, uongozi wa Bunge na Serikali walikataa ku entertain kukataa posho, kupokea back posho ya mtu. Kwa hiyo Lissu anakula posho, afukuzwe CHADEMA kwa kukiuka Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?
 
Chadema mnapaswa kuonyesha njia ya jinsi ya kutoa maamuzi magumu. Hakuna kinachowezesha Shibuda kubaki chamani. Pamoja na kwamba ni msaliti, kichwa chake hakitofautiani na cha mwendawazimu. Anapopambana haangalii mshale wake unaelekea wapi. Kusema kwamba kukubali posho ni msimamo wake kibinafsi ni sawa, lakini cha kujiuliza yale maneno yake ya kushambulia chama na viongozi wake ni msimamo wake pia? fukuzeni shibuda, tunasema fukezeni. Tangazeni jimbo kuwa wazi, na jipangeni kwa uchaguzi mdogo. Ni afadhali jimbo lichukuliwe hata na shetani kuliko msaliti ndani ya kambi.
.
 
Toa hayo magamba kabla hayajagandamana mwilini ili ccm wajifunze jinsi gani wanaume walivyo na maamuzi magumu maana nina uhakika kijana yeyote kutoka chadema anaweza kusisimama pale coz wananchi washapata tuition ya kutosha kutoka cdm
 
Chadema hapa tunawaomba mfanye maamzi magumu kwa huyu shibuda, ni gamba baya sana ndani ya chama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom