Lindi: Vijiji 4 kuhudumiwa na Tanki la Maji la lita 10,000, Wananchi waomba miundo mbinu iendane na mahitaji

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Wananchi wa Kijiji cha Ruyaya, Kata ya Lihimalyao, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, wameitaka Serikali kuwajengea tanki kubwa litakalo wasaidia kuhifadhi maji na kuondokana na tatizo la huduma hiyo lililopo sasa.

Kilwa. Wananchi wa Kijiji cha Ruyaya, Kata ya Lihimalyao, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, wameitaka Serikali kuwajengea tanki kubwa litakalo wasaidia kuhifadhi maji na kuondokana na tatizo la huduma hiyo lililopo sasa.

Wananchi hao wameyasema hayo, walipoongea na Mwananchi Digital, wakidai tanki lililopo ambalo lina uwezo wa kuhifadhi lita 10,000; halitoshelezi mahitaji ya maji kwa kijiji chao na vijiji jirani na kwamba pia kukatika kwa umeme mara kwa mara, kumeongeza adha ya upatikanani maji.

Mwananchi Digital imeelezwa kuwa, tanki hilo lina hudumia vijiji vya Ruyaya, Mangisani, Kisongo na hata baadhi ya sehemu katika Kijiji cha Lihimalyao.

"Maji yana patikana japo ni kwa uchache, umeme unakatika mara kwa mara na huku tanki lililopo ni dogo, la lita 10,000 na hivyo kushindwa kuhifadhi maji mengi kulingana na mahitaji yetu,” amesema Abdallah Mkopi, Mkazi wa Kijiji cha Ruyaya na kuongeza;

“...wahitaji ni wengi hivyo tunapata adha, foleni inakuwa kubwa, koki zipo mbili tu tena zinatoa maji taratibu, huku watu wakisubiri kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kufanya mambo mengine ya kimaendeleo."

Mkazi mwingine wa Kijij hicho, Rahama Jonasi, amesema akina mama wanaamka saa kumi usiku kupata maji, ambapo kutokana na foleni, wanalazimika kukaa mapaka saa tatu asubuhi ndipo wanapata maji. Na huu ndiyo msukumo wa wao kuiomba Serikali iwapatie tanki kubwa na umeme wa uhakika.

"Watu wa maeneo ya Mangisani, baadhi ya wakazi wa Lihimalyao na wenyeji wa hapa Ruyaya wote tunategemea chanzo kimoja hivyo watusaidie kupata tanki kubwa ili tatizo liishe," amesema Yusuph Mohamedi.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira wilayani Kilwa (Ruwasa), Mhandisi Ramadhani Mabula, amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo ya tanki.

"Uzuri kijiji chao kina chanzo cha maji na yanapatikana, changamoto inajitokeza kwa sababu kuna vijiji vya jirani kama cha Mangisani, Kisongo wanategemea kuchota maji hapo, kama maji yangetumika kwa wakazi wa Ruyaya tu yangetosheleza," amesema Mhandisi Mabula.

Mabula ameongeza kwa kusema kwa sasa unafanyika upembuzi yakinifu ili kubaini gharama halisi za ujenzi wa tanki kubwa, ili ziweze kuombwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndio maana nasema wewe sometimes akili zako zinakua hazina akili. This is serious, wewe unaleta jokes? Seriously? Una bahati Leo ni Jumapili
Wewe utakuwa kuni wa kuchomea wengine maana unadhani una Haki ya kutukana siku zingine isipokuwa jpili.Hamnazo
 
Wewe utakuwa kuni wa kuchomea wengine maana unadhani una Haki ya kutukana siku zingine isipokuwa jpili.Hamnazo
Sijawahi kukutukana na sijalelewa kwenye familia ya CCM! Acha kukwepesha mada, Lindi hawana Maji, Tank la 10,000 ni dogo sana! Mbunge wake Ni nani?
 
Back
Top Bottom