Tango73
JF-Expert Member
- Dec 14, 2008
- 2,128
- 1,225
Kuwa na urafiki na Libya ni sawa swa kuwa na urafiki na mamba. Huyu Gadafi kaleta machafuko mengi sana hapa Africa. Kamuuwa Tolbert , na sankara Tom. Kumyenyekea gadafi msilaumu Kikwete. hata Nyerere amlinyenyekea sana gadafi. Kumbuka wakati ule alipoingilia vita vyetu na Uganda mwaka 1978 na kututia hasara nyingi. Watanzania karibia wote tulimlaani sana Gadafi kasoro Nyerere tuu. Maana Nyerere alienda mkutanoni wa OAU Libya na kumpigia debe gadafi achaguliwe kuwa mwenyekiti wa OAU huku akijua wazi kuwa wanachi wake wengi na mataifa mengi ya Africa,wamemkasirikia Gadafi. Sasa msimlaumu kikwete kama Nyerere nae aliingia mtegoni humo.