Mafuriko ya Libya: Nini chanzo chake, na kwanini hali ni mbaya sana?

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mafuriko makubwa yamesababisha vifo vya maelfu ya watu katika mji wa Derna, mashariki mwa Libya, na kusomba baharini vitongoji na wakazi wengi huku maelfu ya watu wakiwa hawajulikani walipo.

Chanzo cha mafuriko
Baada ya kuzipiga nchi nyingine za Mediterania, Dhoruba kali inayofahamika kwa jina la Daniel iliingia Libya mwishoni mwa juma, na kusababisha mvua kubwa iliyoambatana na maporomoko ya ardhi.

Mvua iliyonyesha kwa sababu ya dhoruba ilijaza kingo za mto ambao kwa kawaida ulikuwa na ukame, kwenye vilima vilivyo kusini mwa Derna. Shinikizo lilikuwa kubwa kwa mabwawa mawili yaliyojengwa kulinda jiji dhidi ya mafuriko yalijaa na kuanza kutiririsha maji katikati ya jiji.

Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) alisema siku ya Alhamisi kwamba maafa yangeweza kuepukika ikiwa nchi iliyogawanyika, iliyosambaratishwa na takriban miaka 12 ya migogoro na machafuko, ingekuwa na huduma ya hali ya hewa inayoweza kutoa tahadhari.

Katika karatasi ya utafiti iliyochapishwa mwaka jana, mtaalamu wa masuala ya maji Abdelwanees AR Ashoor wa Chuo Kikuu cha Omar Al-Mukhtar cha Libya alisema mafuriko ya mara kwa mara ya mto wa msimu, au wadi, ni tishio kwa Derna. Alitaja mafuriko matano tangu mwaka 1942 na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha matengenezo ya mara kwa mara ya mabwawa hayo.

Madhara yake yapoje?
Sehemu kubwa za jiji - baadhi ya maafisa wanasema robo au zaidi - zimeteketezwa. Takriban watu 30,000 wamekimbia makazi yao, kulingana na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni kando ya kingo za mto unaokatiza katikati mwa jiji. Matuta yenye vitongoji vizima juu yaliharibiwa au kusombwa na maji. Miundombinu ikijumuisha madaraja ya jiji imeharibiwa. Mafuriko hayo yaling’oa miti na kuharibu mamia ya magari, mengi yakipinduka ubavu au paa. Waandishi wa habari wa Reuters waliona gari moja likiwa kwenye balcony ya ghorofa ya pili ya jengo. Sehemu kubwa ya jiji imefunikwa na matope.

Umeme na usambazaji wa maji ulikatishwa baada ya mafuriko. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) iliripoti Jumatano kwamba umeme umerejeshwa kwa sehemu pamoja na huduma za mtandao.

Wangapi wamekufa na kupotea?
Maafisa wametoa idadi tofauti ya waliofariki na waliopotea, lakini wapo kwa maelfu. Katika mojawapo ya takwimu kubwa zaidi zilizotajwa kufikia sasa, Meya Abdulmenam Ghaithi alimwambia mtangazaji mmoja kuwa kunaweza kuwa na vifo 18,000 hadi 20,000, kulingana na idadi ya wilaya zilizoathiriwa.

Hichem Abu Chkiouat, waziri wa usafiri wa anga katika utawala wa mashariki, ameiambia Reuters zaidi ya watu 5,300 waliofariki wamehesabiwa kufikia sasa, na huenda idadi hiyo ikaongezeka sana na huenda hata maradufu.

OCHA ilisema Jumatano makadirio ni zaidi ya vifo 2,000 na angalau watu 5,000 hawajulikani walipo. Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) lilisema Jumanne karibu watu 10,000 walidhaniwa kupotea.

Je, ni changamoto gani zinawakabili waokoaji?
Uharibifu uliofanywa kwa miundombinu ikiwa ni pamoja na barabara na madaraja unatatiza sana juhudi za kutoa msaada, huku madaraja yote matatu ya Derna yakiharibiwa, OCHA ilisema.

Maafisa wa Libya wamesisitiza haja ya msaada wa utafutaji na uokoaji, na timu za uokoaji zimewasili kutoka Misri, Tunisia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uturuki na Qatar.

Waokoaji wameomba mifuko zaidi ya kuhifadhia miili. Huku idadi kubwa ya miili ikiwa bado haijapatikana, Meya wa Derna Ghaithi ameelezea hofu ya janga hilo.

Maafisa wa Libya wanasema nchi hiyo haijawahi kukabiliwa na janga la kiwango hiki. Lakini mwitikio umekuwa mgumu kutokana na kutokuwa na mshikamano mzuri na maridhiano ya kisiasa nchini humo.

Libya imekumbwa na migogoro na machafuko tangu mwaka 2011 wakati dikteta wa muda mrefu Muammar Gaddafi alipopinduliwa katika machafuko yaliyogawanya taifa hilo la Afrika Kaskazini katikati na kusababisha maelfu ya wanamgambo hasimu kuwania madaraka.

Ingawa Derna iko chini ya utawala wa Mashariki, serikali ya Magharibi iliyoko Tripoli imetuma msaada katika mji huo.

Citizen Digital

Pia soma: Janga lingine laikumba Libya, mafuriko yaua Watu 6,000, wengine 10,000 hawajulikani walipo
 
'Katika karatasi ya utafiti'? Ripoti ya kitafiti au andiko la kitafiti labda? Na Kulingana na taarifa ya au kwa mujibu wa taarifa ya...
 
Laana ya kumuua Muammar Gadaffi

Tena yameleta madhara makubwa sana pale Benghazi,kwa waasisi wa mapinduzi ya kumpindua Gaddafi

Malipo huwa ni hapa hapa duniani
 
Derna, wakati wa machafuko Misri viongozi wa kikristo walikuwa wanatekwa na kupelekwa Libya mji wa Derna kuchinjwa shingo zao, kumbe Mwenye nguvu alikuwa anawavumilia tu!!! Poleni sana
 
Na tetemeko la uturuki ni laana ya kumuua Gaddafi??
 
Derna, wakati wa machafuko Misri viongozi wa kikristo walikuwa wanatekwa na kupelekwa Libya mji wa Derna kuchinjwa shingo zao, kumbe Mwenye nguvu alikuwa anawavumilia tu!!! Poleni sana

Daah,hawa jamaa washenzi sana. Dini ya haki my ass
 
Laana ya kumuua Muammar Gadaffi

Tena yameleta madhara makubwa sana pale Benghazi,kwa waasisi wa mapinduzi ya kumpindua Gaddafi

Malipo huwa ni hapa hapa duniani
Yaani wewe ni nyambole kwelikweli, Morocco wao wamemuua nani.
 
Back
Top Bottom