Elections 2010 Let's support John Mnyika!

Alaf umenikumbusha. Nina zaidi ya siku tatu sijaonja Kitimoto. Nadhani leo itapendeza kwenda kupunguzia hangover za weekend...

Mafisadi utaijua tu kwa michongo yao. Hili sasa ukilipa ofisi ya maana serikali lazima litengeneza ka-bar kadogodogo ofisini. :becky:
 
Waheshimiwa wanajamvi.
nimetumiwa ujumbe mahususi kutoka kwa mbunge mtarajiwa wa Jimbo la ubungo. Shime tujitokeze tukamuunge mkono kwani pamoja na kura yako lakini kuna gharama za kulinda kura. tushiriki wazalendo.
John Mnyika

Ndugu,

Asante sana kwa kuniunga mkono na kuwezesha kampeni mpaka sasa mimi binafsi pamoja na chama chetu cha CHADEMA kwa ujumla.

Tumedhamiria kudhibiti uchakachuaji wa kura kwa kuwa na mawakala makini na waaminifu watatu watatu kwa kila kituo kutoka kada mbalimbali mathalani wanachama, wasomi na wafanyakazi vijana kwa ujumla takribani elfu tatu (3,000).

Mawakala watahitaji maji, chakula, usafiri na mawasiliano siku hiyo ya Oktoba 31, 2010.

Hivyo basi, napenda kukukaribisha jumapili hii Oktoba 4, kwenye tafrija/harambee ya kuchangisha fedha na rasilimali nyinginezo "Fundraise", Landmark Hotel-Ubungo.

Tafadhali wasiliana na; Kenner (0719-516 747), Hawa (0715-185135)

Nakuomba usambaze na kuwafahamisha wengine wengi wenye kupenda kuona mabadiliko na wanaoniunga mkono ama kukiunga mkono CHADEMA.

Daima tukumbuke; Maslahi ya Umma Kwanza!

Wenu,

John MNYIKA.
 
Waheshimiwa wanajamvi.
nimetumiwa ujumbe mahususi kutoka kwa mbunge mtarajiwa wa Jimbo la ubungo. Shime tujitokeze tukamuunge mkono kwani pamoja na kura yako lakini kuna gharama za kulinda kura. tushiriki wazalendo.

Asante mkuu
 
nyota ya mnyika yaendelea kupamnda kila kukicha 03/10/2010 pale ubungo walipo kusanyika vijana zaidi ya miambili na kujitolea kuwa wtakuwa mawakala wake na hizo ni kura zake moja kwa moja jumlisha na wale marafiki wawanafunzi wa shule nyingine, kila mwanafunzi pale akiuwa akionyesha matumain na mnyika kwenye jimbo hilo lililotelekezwa na CCM miaka nendarudi ..... kila mwanafunzi alisikika akisema huu ni muda wa mabadiliko so people tupo tayari kupokea kiongozu makini kwaajili ya ubungo bora nba sibora kiongozi mnyika , slaa tunawaamini tunawahitaji kuratutawapa........... mnyika ndiyo mbunge wetu slaa ndiyo rais wetu.......
 
Mimi naishi tegeta naaidi kufanya kazi yoyote nitakayopewa na chadema siku ya kupiga kura.
 
Ccm wafeli ubungo ni kwa mbinu chafu za jana walizokuwa wanazifanya ili kamanda mnyika asifanye mkutano wake wa kampeni pale mburahati kiwanja cha barafu, mtendaji wa kata aliita polisi wakaja na gari tatu, ila kwakutumia nguvu ya umma tukafanya mkutano wa nguvu na wananchi waka mchangia kamanda hela za mawakala :
 
Mnyika aendelea kuikamata ubungo kwa kasi ya ajabu leo pale urafiki kwenye mdahalo uliyo kuwa umeandaliwa na forum leadership, aliwafanya watu kutaka aendelee kuonge yeye ndipo msimamizi wa wa mdahalo huwo alipo badili namna ya kuongea na kusema maswali ya sasa ni ya pamoja yaani yata jibiwa na wabunge wote ndipo angalau wakapata nafasi ya kuongea
 
Back
Top Bottom