Leticia Musore wa CHADEMA ahamia NCCR

Kwanza viti majina ya viti maalum sio ishirini,mbona cdm wamepata viti maalum zaidi ya 20.Muongo huyo alikuwa anavizia ulaji.
 
Safari ya kufa kwa Chadema imeanza.

Muda mfupi tulisikia M/Kiti Mbeya, sasa M/Kiti wanawake Taifa....more to follow.

Nilikuwa sahihi hata mimi kujitoa wiki iliyopita.

Hata kuku humwombea mwewe mabaya, fuatilitia uone kama dua zake zimeshatimia. Am afraid to say yours sound the same
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Hii inaonyesha kuwa alikuwa kimaslahi zaidi kwani mtu makini hawezi kuyumbishwa na kukosa ubunge "wakuteuliwa" Na kwa sababu inajidhihirisha hivyo kauli zake lazima ziwe zamfa maji mengi yata semwa ila kwa watu makini hatuwezi kuyumbishwa na maneno ya wafa maji kwani MAWIMBI YA KIKOMBE HAYAZAMISHI KIJIKO!!!
 

CDM wana viti 25. Katika orodha hiyo Tume imepiga msitari chini ya Ms Rebecca Mngodo ambaye alikuwa namba 26. Ukitoa jina la iron lady-Ms Mdee. Mbona kwenye kampeni hatukumsikia ili %age ya kura za CDM wabunge/Rais zitoshe kustahili 30 secial seats ili nae awemo. Mama Naomi Kaihula na dada Regia waligombea hivyo contribution yao kwa chama iko wazi. Utaratibu kwenye basi ukitelemka wengine wanapanda. Tunatakia kila la heri huko aendako!
 
Alitaka apewe viti vya ubunge nini?

Nakumbuka Lyatonga alitaka kuhamia CUF wakati fulani kwa sharti la nkuhama na uenyekiti wake jamaa wakamwambia kama unataka hamia ila uwe mwanachama wa kawaida. wengi wa viongozi wa upinzani ni makapi ya CCM walikuwa wakitetea sera za chama na kudumisha fikra za mwenyekiti ila kubwagwa kwao kwenye vinyang'anyiro vya uongozi mbalimbali ndio kumekuwa sababu ya kukimbilia upinzani. Navipongeza baadhi ya vyama makini kama CUF wao huwa hawawapi nafasi watu kama hao kuingia na kugombea kwenye chama chao ila kuna vyama MashaAllah leo mtu akijiondoa CCM kesho wanamtafutia sehemu ya kugombea mfano hai mzee wa CCJ alipo toka CCM mpaka CCJ na kukimbilia CDM walimpokea na kumfanyia mizengwe apate nafasi ya kugombea ubunge jimbo la segerea.
 
unauliza karafuu pemba. Angalia alivyokosa urais

Alipoukosa ubunge kwa tiketi ya CCM alikimbilia CDM namshauri kaukosa Urais CDM akimbilie CCM ili agombee Urais 2015. Ni ushauri tu jamani wamachamme msijeniua.....
 
duh mwacheni akajitulize haikuwa fair kumnyima nafasi ya uwakilishi wakati aliaminiwa na wanawake wa chadema tz
 
Alipoukosa ubunge kwa tiketi ya CCM alikimbilia CDM namshauri kaukosa Urais CDM akimbilie CCM ili agombee Urais 2015. Ni ushauri tu jamani wamachamme msijeniua.....
hawawezi kukuua mkuu wamechoka na kauli ya mpiganaji wao kipenzi
mbowe wa bilicanas aka mzee wa
left eyes kumtambua JK kama rais wa tz
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Wanasiasa wengi wanapenda madaraka ila Watanzania ni vipofu mfano hai jamaa yangu mmoja alitoswa ubunge jimbo la karatu akakimbilia chama fulani na sasa kaukosa ukuu wa kaya si mnaona alivyokuwa mbogo? nina wasiwasi atahama na chama ili apate uongozi. Wengi wanataka ukubwa na ulwa jamani tuwe macho............
 
bado Zitto ,yaani huyu siku akiondoka ntalipia hata kikosi cha matarumbeta toka pale magomeni na wale wacheza vibao kata wamsindikize huko CCM

tutakuwa pamoja, maana dogo ameshaanza kuwa kero chadema...isitoshe bungeni nafasi yake imeshakuwa covered na mpiganaji Mnyika
 
Kwenye Msafara wa Mamba na Kenge wapo.
Acha Kenge wote wajiondoe wenyewe mapema ili tubakie na (Mamba) wapiganaji wa ukweli wenye uchungu wa kuleta mabadiliko ya kweli.

Do u mean Dr Slaa ni mamba kwa kitendo chake cha kuhama CCM kuja CDM? Au akinya anye kuku? Brother and sister mie siasa za bongo zinanishinda sasa huyu jamaa alihama kutoka CCM kuja CDM tukampkea na kumpa ile fursa aliyonyimwa kule na dhumuni lake lilikuwa awe muheshimiwa akaupata! Sioni sababu ya huyo mama kusakamwa kwenda CCM ilhali katiba ya nchi hamkatazi pengine kuna mazuri ameyaona.
 
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!

Orodha ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu-CHADEMA
Orodha ya wanawake 40 wa juu
1. Lucy Fidelis Owenya
2. Esther Nicholas Matiko
3. Mhonga Said Ruhwanya
4. Anna MaryStella John Mallac
5. Halima James Mdee
6. Paulina Philipo Gekul
7. Conjesta Leos Rwamlaza
8. Susan Kiwanga
9. Grace Sindato Kiwelu
10. Susan Lyimo
11. Regia Mtema
12. Christowaja Mtinda
13. Anna Valerian Komu
14. Mwanamrisho Abama
15. Joyce Mukya
16. Leticia Mageni Nyerere
17. Naomi Kaihula
18. Chiku Abwao
19. Rose Kamil Sukum
20. Christina Lissu Mughiwa
21. Raya Ibrahim Hamisi
22. Philipa Geofrey Mturano
23. Mariam Salum Msabaha
24. Rachel Mashishanga Robert
25. Sabrina Hamza Sungura
26. Rebecca Michael Mngodo
27. Cecilia Daniel Pareso
28. Subira Shabani Waziri
29.
Leticia Gati Musore
30. Helen John Kayanza
31. Rosana Osemu Chapita
32. Mona Shomary Bitakwate
33. Evarim Adrian Mpangama
34. Asha Sudi Kayumba
35. Hija Rashid Wazee
36. Mary James Martin
37. Sophia Hebron Mwakagenda
38. Bupe Odeni Kyambika
39. Magreth Thadei Mangowi
40. Esther Cyprian Daffi

Mheshiwa Kitila Mkumbo ulaileyani,

Samahani nina kaswali kangu kadogo kuhusu huyu mama aliondoka CDM unaweza kuniambia alijiunga chamani lini? Na naomba pia unipe data hizo hizo kwa number 17. Naomi Kaihula mwalimu wangu wa CBE na 19. Mhe Rose Kamili.

Ningependa nijue vigezo vya kuwa rank hawa wakina mama maana kumbukumbu zangu zinaniambia mama Naomi alikuwa hana kabisa mambo ya siasa kwa miaka ya hivi karibuni na alikuwa akitufundisha CBE communication skills na development studies ila ameweza kuwa wa kumi na saba sambamba na Rose Kamili aliejiunga CDM karibuni.

Nitashukuru kwa majibu yako.

Songela sana......
 
Kama aliingia CHADEMA kupata ubunge akapigwa chini unategemea nini.... Na kama wakuu wake wamestukia kwa nini wampe Ubunge, eti kwa sababu ni mwenyekiti wa wanawake? Safari njema kwake
 
Back
Top Bottom