Leticia Musore wa CHADEMA ahamia NCCR

"Uongozi wa juu wa chama haukuwa ukinishirikisha katika maamuzi, haukuijali nafasi yangu kama mwenyekiti wa Baraza la wanawake kitaifa, ndo maana leo tr 22 Novemba, nimehamia NCCR-Mageuzi" Leticia Ghati Mosore

Angeligombea jimbo lolote lile na hata kama angelikosa hivi sasa angelikuwa Bungeni..................Ni uvivu wake tu umemponza...........
 
mwenye jibu zuri hapa atakuwa DR.MKUMBO kwani ndio alipewa kazi kama consultant kutengeneza vigezo viti maalum,atuambie kama huyu alikuwa kati ya ishirini kama anavyodai.

Yaani katiba ya CHADEMA haina kipengele cha namna ya kuteua wabunge wa viti maalum hadi kazi anapewa consultant?
 
Mheshiwa Kitila Mkumbo ulaileyani,

Samahani nina kaswali kangu kadogo kuhusu huyu mama aliondoka CDM unaweza kuniambia alijiunga chamani lini? Na naomba pia unipe data hizo hizo kwa number 17. Naomi Kaihula mwalimu wangu wa CBE na 19. Mhe Rose Kamili.

Ningependa nijue vigezo vya kuwa rank hawa wakina mama maana kumbukumbu zangu zinaniambia mama Naomi alikuwa hana kabisa mambo ya siasa kwa miaka ya hivi karibuni na alikuwa akitufundisha CBE communication skills na development studies ila ameweza kuwa wa kumi na saba sambamba na Rose Kamili aliejiunga CDM karibuni.

Nitashukuru kwa majibu yako.

Songela sana......

hoja sio nani kaingia chama muda gani ,ila hoja ni kuwa kwa muda huo aliokaa amefanya nn?kwa chama na ukuaji wa demokrasia kwa ujumla. pili akipewa nafasi ya ubunge ataweza kufikia matarajio ya watz? tatu,dhamira yake,uwezo wake,n.k ni kwa maslahi binafsi ama kwa watz wote? na mwisho kuhusu kaihula alikuwa CDM tangu 2007 na ni katibu mkuu wa wanawake tangu mwanzoni mwa 2008. kuhusu ROSE KAMILI ni sawa na kuhoji mbona shibuda,kahigi wamekuwa wabunge?0samahani kwa kuwa msemaji wa DR MKUMBO.
 
Yaani katiba ya CHADEMA haina kipengele cha namna ya kuteua wabunge wa viti maalum hadi kazi anapewa consultant?

katiba inaeleza kuhusu process lakini vigezo ni juu ya ranking nani awe wa kwanza nani awe wa kumi nani awe wa 102, ndio maana alitafutwa consultancy wa kazi hiyo! na lengo lilikuwa kuondoa malalamiko kuwa kuna upendeleo,ila vigezo hivyo vilipitishwa na kamati kuu ya chama, nawasilisha.
 
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!


Orodha ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu-CHADEMA

Orodha ya wanawake 40 wa juu




1.Lucy Fidelis Owenya
2. Esther Nicholas Matiko
3. Mhonga Said Ruhwanya
4. Anna MaryStella John Mallac
5. Halima James Mdee
6. Paulina Philipo Gekul
7. Conjesta Leos Rwamlaza
8. Susan Kiwanga
9. Grace Sindato Kiwelu
10. Susan Lyimo
11. Regia Mtema
12. Christowaja Mtinda
13. Anna Valerian Komu
14. Mwanamrisho Abama
15. Joyce Mukya
16. Leticia Mageni Nyerere
17. Naomi Kaihula
18. Chiku Abwao
19. Rose Kamil Sukum
20. Christina Lissu Mughiwa
21. Raya Ibrahim Hamisi
22. Philipa Geofrey Mturano
23. Mariam Salum Msabaha
24. Rachel Mashishanga Robert
25. Sabrina Hamza Sungura
26. Rebecca Michael Mngodo
27. Cecilia Daniel Pareso
28. Subira Shabani Waziri
29. Leticia Gati Musore
30. Helen John Kayanza
31. Rosana Osemu Chapita
32. Mona Shomary Bitakwate
33. Evarim Adrian Mpangama
34. Asha Sudi Kayumba
35. Hija Rashid Wazee
36. Mary James Martin
37. Sophia Hebron Mwakagenda
38. Bupe Odeni Kyambika
39. Magreth Thadei Mangowi
40. Esther Cyprian Daffi

Kitila
Kwanza nikushukuru kwa kufanya siasa ya uwazi. Lakini naomba labda niulize ni vigezo gani vilitumika kuchagua hii list? Pili ni kwa nini baadhi ya wagombea walikuwepo kwenye list wakati teyari walikuwa wanagombea majimboni. Mfano Halima Mdee au dada Regia. Jee huoni kama kuna theory ilikuwa inatumika hapa kwamba kuingia bungeni ni lazima kwa baadhi ya wanachama wenu.

Tatu, jee kwa nini watu kama Mhonga wanaendelea kupewa hivi viti wakati wana capability ya kusimama majukwaani sababu tayari wameshakuwa bungeni kwa term moja.

Nne, Jee ni unamsimamo gani kuhusu swala zima la viti maalumu? Namaanisha ya kwamba what is the specific reason ya kuwa na hivi vitu and how your selection fits that particular reason.

Mwisho kwa wote, huyu mama ana haki yake ya msingi kwenda chama anachokitaka kwa lengo analolo litaka. Lakini ifahamike ya kwamba hii sifa ya ukabila na udini inajikita miyoni mwa wananchi, ni dhahiri kabisa Chadema inaweza kupay the price kwenye ballot 2015. Hivyo ni matumaini yangu ya kwamba kutafanyika mchakato wa kuzuia hii slow bleeding.
 
Huyo ndio Mbowe, anaiendesha. Chadema kama anavyoendesha bilicanas, hakuna uadilifu wala demokrasia, u dictator mtindo mmoja.
 
Kuama baada ya kunyimwa cheo ni dalili tosha kuwa alikuwa chadema kwa ajili ya maslahi yake binafsi
na si kwa kupigania maslahi ya watanzania wenzake na pia kudai ubaguzi baada ya kunyimwa cheo kunaifanya hoja yake kuwa na mashaka makubwa ingawa ni haki yake ya kidemokrasia kuamia chama akipendacho.
 
Huyo atakuwa amepandikizwa kapata mrungura

Yaani hapa utasikia mengi, utasikia hata mjumbe wa chadema kijijini kahamia TLP NCCR yaani ilimradi katangazi watu wamesikia.

Mafisadi angaika CHADEMA ni cha kinachokubalika kwa watu
tusiwe hivi jamani

Leticia ni binadamu na anjua anachofanya... CDM kwa sasa inaingia kwenye transition ambayo itai-define upya kama chama cha watu au cha kikundi cha watu.

In any organization, if you dont pass this stormy phase, mara nyingi unakua kwenye utopia au unakua goigoi...

All teh best Leticia, ila message to CDM kwamba you need to relook at what was the common goal for your executive members na kama wengine hawamatch hilo, au kama kuna haja ya kubadilika, badilikeni kupisha wenye moyo na nchi yao

I would rather see 1000 leticia leave than staying as a small party trying to keep leticia happy

To my knowledge, zitto was to go to NCCR some time ago, probably he better go now so that CDM dont have more destructive minds in their way to full opposition party
 
"uongozi wa juu wa chama haukuwa ukinishirikisha katika maamuzi, haukuijali nafasi yangu kama mwenyekiti wa baraza la wanawake kitaifa, ndo maana leo tr 22 novemba, nimehamia nccr-mageuzi" leticia ghati mosore

pole sana mama, mwanzoni niliona thread moja ya kulalamikia umekosa uteuzi wa viti maalum. Vigezo si viuliwekwa wazi kwa kila mtu. Nenda kawasubiri wapo wengine watatoka chadema kuja kugombea uras huko 2015. Shughulika kutayarisha makao kabisa.
 
Huyo ndio Mbowe, anaiendesha. Chadema kama anavyoendesha bilicanas, hakuna uadilifu wala demokrasia, u dictator mtindo mmoja.
vipi bana... hilo tawi la ccm (kafu) limekosa habari naona sasa hushindi kuchungulia CDM wanafanya nini... pole weee... kumbuka hata akina kambona walikimbia hadi nchi bana na CCM ikapeta, by then yalikua mageuzi... basi ndo hayohayo yanakuja

You cant stop the wind by whistling
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Kwa hiyo siku zote alizokuepo Chadema ilikuwa pouwa, mpaka sekunde chache walipoacha jina lake kwene 'viti vya njugu' ndio akapata mwanga kuna ubaguzi...bwe he he he..halafu kwa wanasiasa wene uono finyu kama huyu ndio tutegemee kuigeuza nchi kuwa nchi ya maziwa na asali ..

Btw, hapo hakuna mwanasiasa, mwanasiasa wa kweli hahami kwa kukosa fursa ya mafao ya ubunge, hasira au chuki, bali huhama kufuata au kusimamia principles.
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Waache waende na wengine tutegemee kurudi. Hiyo ndiyo political freedom.
 
vipi bana... hilo tawi la ccm (kafu) limekosa habari naona sasa hushindi kuchungulia CDM wanafanya nini... pole weee... kumbuka hata akina kambona walikimbia hadi nchi bana na CCM ikapeta, by then yalikua mageuzi... basi ndo hayohayo yanakuja

You cant stop the wind by whistling

Umechapia kidogo, wakati wa Kambona kulikuwa kuna TANU na si CCM. Pole
 
Kwa hiyo siku zote alizokuepo Chadema ilikuwa pouwa, mpaka sekunde chache walipoacha jina lake kwene 'viti vya njugu' ndio akapata mwanga kuna ubaguzi...bwe he he he..halafu kwa wanasiasa wene uono finyu kama huyu ndio tutegemee kuigeuza nchi kuwa nchi ya maziwa na asali ..

Btw, hapo hakuna mwanasiasa, mwanasiasa wa kweli hahami kwa kukosa fursa ya mafao ya ubunge, hasira au chuki, bali huhama kufuata au kusimamia principles.


Angalia kwa macho yote mawili tumia ubongo kwa unayoyaona mbele yako kisha geuka nyuma utamuona Dr Slaa akikimbia CCM kuingia CDM kwa sababu pacha na ya huyu mama kisha shusha pumzi zako na useme Mungu nisamehe kwa kuhukumu hakika hukumu ni kazi yako wewe tu kwani wewe ni hakimu wa kweli.
 
hta mm nina mashaka sana na huyu zitto nyepesi,mbona kama haeleweki ni wa chama gani,c angejiweka wazi tu kama yeye ni kuku au bata?
 
Back
Top Bottom