Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,200
- 27,252
Kesi ya kina Mdee na CHADEMA leo imeingia ukurasa mpya baada ya mawakili wa CHADEMA kusema hawana tena maswali kwa akina Mdee.
Hapo siku za nyuma mawakili hawa walishangiliwa sana jinsi walivyokuwa wakipambana na kina Mdee mahakamani na wengi wakashangilia pia jinsi walivyokuwa wanawahoji maswali na wapo waliosema "tutayajua mengi"
.....Ajizi nyumba ya njaa..... Leo hii wale mawakili wamenyoosha mikono juu na kusema hawana tena maswali kwao. Kwa lugha nyepesi mambo yanaenda kuisha
Tabu kubwa inabaki kwa washabiki waliokuwa wakisubiri kwa hamu kina mdee wadhalilike ili waandike kila aina ya andiko. Walisubiri kina mdee wateseke, wachekwe.
Wenye akili tuliwaambia mapema.
Viva Mdee, vivaaaaa
#kazi inaendeleaaaaa#
===
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefunga kuwahoji wabunge watatu miongoni mwa wengine 19 wa viti maalum waliofukuzwa uanachama na chama hicho, kikisema kuwa hakina maswali zaidi kwa wabunge hao.
Wabunge walioachwa kuhojiwa maswali ya dodoso leo Jumatatu Machi, 6, 2023 ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya na Ester Matiko.
Akizungumza leo Machi 6 wakati kesi hiyo iliitwa kwaajili ya Jesca Kishoa kuendelea kuhojiwa maswali ya dodoso, Wakili wa wajibu maombi, Hekima Mwasipu, amesema kesi hiyo ilipaswa kuendelea kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Jesca Kishoa lakini kwa upande wao wamefunga.
Wabunge hao 19 wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee walifukuzwa uanachama Novemba 2020 baada ya kwenda bungeni Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama hicho.