Hawa jamaa waishie tu huko kwao. Na hii global warming threat, sijui wataenda wapi masikini kisiwa hicho kikifunikwa na maji. Poor Zanzibaris:coffee:Nonda, mkuu ebu tazama picha hiyo hapo juu kisha utuambie kama kweli hao ni Magamba?.. Hawa ni wananchi wenye hasira na wenye kuitaka haki yao kwa nini nasi tusiwasikilize ikiwa tunawasikia watu wa Palestine au Burma..
Maadam tunawapa muda tosha ifikapo July mosi 2014 wawe tayari wameisha fanya maamuzi ya kura za maoni basi hatuna sababu ya kuendelea kulonga. Kazi kwao, badala ya kuandamana walivamie bunge lao kesho na kuomba kupiga kura za maoni kama walivyofanya mwaka 2010.
Viongozi wa serikali ya mseto kutoka CUF na CCM Zanzibar (baraza la Mapinduzi) wapeni wananchi wenu haki yao ya msingi, tena kama ikiwezekana nasi bara tuandamane kuwaunga mkono Wazanzibar ili wapewe ruksa ya haki yao kudai kuondoka ktk Muungano ifikapo July 1 2014.