Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Muungano ulikuwa na matatizo toka siku ya kwanza ya kuundwa kwake.
Utavunjika tu siku ccm itatoka madarakani, kama ccm itaendelea kuwepo tusitegeemee mabadiliko yoyote yale.
Nakubaliana nawe kuwa ulikuwa na matatizo, kwa mawazo yangu muungano wowote ni kitu chema iwe ulianza vizuri au vibaya. Cha kufanya ilikuwa kurekebisha matatizo ya kuuweka sawa, ila hawa jamaa ukiwaangalia sicho wanachotaka. Wanataka kwanza nchi yao halafu waamue waungane na nani, kitu ambacho si kibaya ila wanaitaka toka kwa nani ndio shwali. Kwanini wasijaribu kujiondoa wenyewe waone kama kuna mtu atawashika mkono?

Ila mimi nina wasiwasi kuwa hawa jamaa kuna janja ndani yao, taarifa ya habari ya Channel Ten Mzee Mwinyi akiwa na umati mkubwa wanawakebehi wanaotaka kuvunja muungano. Kwani hawajuani!, si mchezo unaochezwa hapa? ili waendelee kuonewa huruma kama wanaonewa kweli na maisha yawe ya kuvyonza tu.
Hata kama unamdai mtu kitu, hapa achukue message ipi, hamtaki au mnataka?. Kama hawataki kweli wachukue ushauri waliopewa.
 
I support this movement na tena wafanye haraka.Ikiwezekana wabunge wao kutoka zanzibar wasije kabisa kwenye kikao kijacho. Tumewachoka na lazima walielewe hilo
 
zanzibar2.jpg


Msitunyonye bana nyie! Msitunyonye mnatudhiri! Tuachaneni angalau tujikung'ute kidogo! Tumekuwa mafukara; mtu mwenye miaka kumi na tatu amepinda mgongo kama mtu wa miaka sabini na tano! … tunachotaka sasa hivi mtuachie tupumue!
– Mhadhara wa Uamsho Zanzibar Machi 4, 2012.


Nimekuwa mtetezi wa Muungano kiasi kwamba nimegundua nimebakia peke yangu. Wengine wanautetea Muungano kwa kutumia vitisho na wengine wanautetea kwa kutumia dharau. Binafsi ninaamini muungano unaweza kutetewa kwa hoja maridhiwa zenye kuonesha kuwa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wananufaika na wataendelea kunufaika zaidi katika Muungano kuliko nje ya Muungano. Kwamba hoja za kupinga muungano kwa madai kuwa Wazanzibari wanaonewa na kuwa Zanzibar inakaliwa kama koloni na Tanganyika haina mshiko, ni ya kupuuza na ina uwezo wa kuteka akili za watu wasiotaka kufikiria.


Baada ya muda mrefu kuwa mtetezi pekee wa Muungano kelele za hivi karibuni zimenibadili kabisa mawazo yangu na sasa nimekuwa na nitaendelea kushakizia muungano uvunjwe ili wale wanaoitaka Zanzibar yao wapewe na ili watu wa bara tuhangaike mambo mengine kuliko kuonekana tunawakandamiza Wazanzibari. Ile hofu ya Mwalimu kiasi cha kuachilia mambo mengi ya Zanzibar kuwa tukiungana kuwa nchi moja kamili kabisa Zanzibar watajiona wamemezwa imetimia kwani pamoja na kuwapa kila kitu Zanzibar bado wapo ambao wanaona wanamezwa!


Ni kutokana na ukweli huu kwamba hakuna kiongozi au mwanasiasa wa Tanzania awe mzee au kijana mwenye uwezo wa kuutetea Muungano kisomi na kisiasa na kuwapinga wenye hoja dhaifu ndio maana leo naendelea na hoja yangu ya kuwasaidia Wazanzibar watoke kwenye Muungano, wawe na nchi na taifa lao na zaidi ya yote waweze baada ya kutoka kwenye Muungano kuanza mahusiano mapya na bara kama nchi mbili zilizo sawa. Ninaamini tunaweza kuhusiana vizuri zaidi baada ya Zanzibar kutoka na kuwa taifa lao wenyewe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo Muungano hauteteleki – zaidi ya kutumia vitisho vya dola.


Tunawapenda sana ndugu zetu Wazanzibari kiasi kwamba hatutaki kuwang'ang'ania. Wapo kwao wenye kutuchukia sana kiasi kwamba hawataki hata kufikiria sisi ni ndugu zao. Wanatuangalia kwa dharau na kebeki wao wakiamini utukufu wao wa "Zanzibar" isiyokuwepo ndiyo tunu waliyonayo. Ukiwaskiliza sana baadhi ya wapinga muungano kwa kweli kabisa wamejawa chuki isiyo na kifani na chuki hiyo imezaa matunda meusi katika madhihirisho ya chuki dhidi ya watu wa Bara na Wakristu.


Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi hawataki kukifikiria ni kuwa hawa watu wanaopinga Muungano wao wanadai "nchi". Sasa hakuna aliyewauliza kwamba mbona katiba ya Zanzibar imefanyiwa mabadiliko na kuitangaza kuwa Zanzibar ni nchi? Sasa kama tayari Zanzibar ni nchi wanachodai hawa ni nini? Haiwezekani kuwa wanachodai ni nchi kwani nchi tayari wanayo na Katiba ya Zanzibar inasema hivyo! Wanachotaka siyo nchi! Wanachotaka ni kuwa nje ya Muungano! Hivi ni vitu viwili tofauti.


Ndio maana basi katika makala ya leo nataka kuwasaidia Wazanzibari hawa na wale ambao wanaamini kuwa muungano haustahili kuteteewa kwa hoja bali kwa vioja. Pendekezo langu ni njia nyepesi za Wazanzibari kujiondoa kwenye Muungano bila kufanya maandamano, mihadhara wala kuwashtumu watu wa Tanganyika. Wazanzibari wakitaka kutoka kweli kwenye Muungano wanaweza kufanya hivyo ndani ya wiki chache tu na wakawa nchi. Nina uhakika serikali ya Muungano haitotumia nguvu kuwalazimisha kubakia! Nyerere mwenyewe alishasema kuwa hawezi kuwalazimisha Wazanzibari kubakia kwenye Muungano.


Njia ya kwanza
Njia ya kwanza na nyepesi zaidi ya kuweza kujitoa kwenye Muungano ni kwa wananchi wa Zanzibar wakiongozwa na hawa wana- uamsho wawatake watendaji wote wa Muungano wenye asili ya Zanzibar kuachia nafasi zao mara moja na kurudi Zanzibar!


Hii ni pamoja na majaji, wabunge, mawaziri, maafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama, na wantedaji wengine ambao wako kwenye Muungano. Badala ya kuililia Tanganyika kila kukicha kuwa inawabana mashehe wa Zanzibari wenye kuongoza vuguvugu la kutoka kwenye Muungano waanzishe mihadhara ya kuwataka Wazanzibari wenzao ambao wanatumikia Muungano waachilie nafasi hizo.


Binafsi ningependekeza kama wataniruhusu waanzishe harakati hizo ili viongozi wote hawa waachilie nafasi zo ifikapo Disemba 10, 2012. Hii ni pamoja na Makamu wa Rais Ghaib Bilal, jaji mkuu na wengine.
Hawa wote wakishawishiwa kuondoka Wazanzibari wajiandae ama kuwapatia pensheni au kuwatafutia nafasi kwenye serikali ya nchi ya Zanzibar.


Sasa hawa wote wakikubali kuondoka kwenye nafasi zao za Muungano Zanzibar itapata wataalamu wengine wengi ambao wamekuwa wakitumikia Muungano na hivyo kujiongezea hazina ya wataalamu mbalimbali. Lakini pia itafungua ajira za Watanganyika wengi ambao wangeweza kushika nafasi zinazoshikiliwa na Wazanzibari hasa kwa vile Wazanzibari hao wako kimya na hawajitokezi kuutetea Muungano ambao wanautumikia.


Pamoja na kuwataka viongozi wao na watendaji mbalimbali watoke kwenye Muungano katika harakati za mwanzo za Zanzibar kujitenga wana uamsho hawastahili kulalamikia Watanganyika. Hawahitaji kuendelea kuwaghilibu vijana wa Kizanzibari kuwa inanyonywa na sasa wanahitaji kupumua. Mashehe wa uamsho waende mbali zaidi katik akudai nchi yao. Waanze kuwahamasisha Wazanzibari walioko bara kuamua kuondoka bara na kurudi Zanzibar ili kuendesha shughuli zao huko.


Watu kama kina Bakheresa wenye biashara kubwa bara itabidi watiwe hamasa waamue kuondoka bara. Siyo hawa tu bali pia wale Wapemba na Wazanzibari waliona maeneo ya ardhi Bara. Hivi ndivyo ilivyotokea Sudan ya Kusini ambapo baada ya nchi hiyo kujitenga Wasudan ya Kusini waliokuwa wanafanya kazi Khartoum waliacha kazi zao na wengi wao wameamua kurudi kwenye nchi yao kuanza kuijenga.


Wengi tunakumbuka kuwa baada ya Rwanda chini ya Kagame kutulia kwa kiasi Wanyarwanda wengi ambao wengine waliishi kama Watanzania waliacha kazi zao na kurudi kwao Rwanda kuijenga nchi y ao. Nakumbuka baadhi ya wahadhiri kwenye taasisi mbalimbali nchini ambao tuliwadhania ni Wahaya au Waangaza walipoamua kuacha kazi zao kumbe walikuwa ni Wanyarwanda.


Hili pia litakuwa na faida kubwa sana kwa Zanzibar kwani itapata watu wengi zaidi wenye uwezo na utajiri mkubwa na vile vile itabidi iwaandalie viwanja vipya vya kilimo na makazi maana vile vya bara itabidi waviachilie kuwapisha Watanganyika ambao wanalalamikia kukosa ardhi au kupatiwa ardhi isiy nzuri. Na pia wafanyabiashara hao wa Kizanzibari watakaporudi Zanzibar na kama watataka kuja kufanya biashara Tanganyika itabidi waje kama wawekezaji na hivyo watasaidia katika ukuaji wa uchumi wa Tanganyika kama wageni wengine. Na kama watakuwa wajanja kama wageni wengine wanaweza kutengeneza mamilioni zaidi kuliko wanavyofanya sasa kama raia wa Tanzania!


Hivyo hilo ni jjambo la kwanza nawashauri wana uamsho; hamasisheni Wazanzibari waondoke Tanzania bara ili warudi Zanzibar ambako watapatiwa nafasi bora zaidi za ajira. Mtakapofanya hivyo, na watu wa Bara nao itabidi waanze kuondoka Zanzibar japo hapo nina uhakika kutakuwa na kazi kidogo. Watu wa Bara ni kina nani Zanzibar?


Njia ya pili
Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema,"Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.


Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano.
Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa Bara au Serikali ya Muungano.


Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya Katiba ya Zanzibar.


Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la?


Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.


Swali liwe rahisi tu:
Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014 na yasipotatuliwa basi kipengele cha "b" kitatimia.

b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa kwenye Muungano ifikapo Julai 1, 2014.



Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie", maana yake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014. Baadhi ya watu ambao wamesoma hoja yangu hii ya pili wamedai – na mimi nikakubali – kuwa mwaka 2014 ni mbali sana. Hivyo, Wazanzibari wakitaka kujitenga wanaweza kuja na sheria kwenye kikao kijacho cha baraza la wawakilishi na ninapendekeza Mjumbe Jussa alete muswada wa swali la kura ya maoni ili Wazanzibari wafanye hima ya kujitoa kwenye Muungano.


Nina uhakika wapo Watanganyika ambao watashukuru sana kwa wao pia kupewa nafasi ya kupumua kuliko kila siku kuimbiwa "Zanzibar, Zanzibar"; kama kweli inavyosemwa Muungano ni kama koti likibana unalivua ni wazi kuwa wanaobanwa na koti hilo sasa siyo Zanzibar tena bali ni watu wa bara na sasa wameamua kuwapa Wazanzibar uwezo kamili (absolute power) kujitoa kwenye Muungano bila kufanya mihadhara mingi wala kushindana na dola.
Njia hizo hapo juu zitawasaidia Wazanzibari wanaotaka kujitoa watoke salama hasa kwa vile inaonekana hakuna Wazanzibari wanaoutaka Muungano. Watu wa Bara hatutaki kuonekana tunawang'ang'ania Wazanzibari wakati nguvu yote ya kutoka kwenye Muungano wanayo wao.


Ni matumaini yangu serikali ya Rais Kikwete ambayo imeshindwa kujenga hoja na kuwajibu kwa hoja wana uamsho haitotumia nguvu kuzima harakati za kujitoa kwenye Muungano. Tena ningependa kabisa kutoa pendekezo kwa serikali ya Muungano kukataza kabisa Polisi na JWTZ kuingilia kati mikutano ya wanauamsho na badala yake waache kazi hiyo kwa Valentia, JKU na KMKM.


Vikosi vya Muungano vikae pembeni kabisa kwani vitaonekana vinalazimisha watu kuupenda Muungano. Kama Muungano haupo moyoni, muungano hauwezi kuwepo ulimini! Kama watu wanataka mfumo wa Muungano au mambo fulani yabadilike basi tungeona juhudi za haraka za kutatua kero zote za Muungano badala ya hili la "subirini mkatoe maoni kwenye tume". Watanzania wameshatoa maoni ya kutosha kuhusu Muungano kiasi kwamba kama CCM na serikali yake wangekuwa na uwezo wa kuyatatua basi wangekuwa wamekwishayatatua.


Nidhahiri kuwa hakuna mwenye uwezo huo na sasa kilichobakia ni sote kwa pamoja kutoka Bara tuseme nasi pasi ya shaka kuwa LET ZANZIBAR GO- Iacheni Zanzibar iende.


Itaenda wapi zaidi ya kuwa kwenye kivuli cha Tanganyika ndani au nje ya Muungano


HUU NI MWANZO WA "LET ZANZIBAR GO MOVEMENT 2012"; Kama unaunga mkono kuwaacha Wazanzibar wajitoe kwenye Muungano weka kwenye sahihi yako "I support Let Zanzibar Go Movement 2012"! Tuwasaidie waharikishe wajitoe kwani hakuna kiongozi yeyote ambaye amekuwa na uwezo wa kuutetea Muungano kwa hoja maridhawa badala ya kutumia vitisho na mikwara.


Mwanakijiji and . co umekuwa na ka huu ugonjwa wa Zanzibari , nilikuuliza zamani kama unaunga mkono

muungano au unawapinga uamsho ni jambo gani linawazuia kuweka muhadhara mukawaeleza watu hayo mnayoyaona ni bora ,

Sio kila mtu ana access na internet au kununua gazeti , wengi wa wale wanaohudhuria mihadhara , uwezo wa kupata mlo mmoja unawashinda.

Uamsho wanatumia haki yao kikatiba au nyinyi mumenyimwa haki hiyo ??? mnapita vichochoroni kama wezi tu!!!!

Kama mnazo hoja teremkeni uwanjani msitie mafitina ya kanisa muwape watu nafasi ya kuwahoji

AU TAYARISHENI MDAHALA NA UAMSHO WATU WAAMUE UKWELI UKO WAPI
 
MMKJJ,
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, hoja yoyote ya kuuvunja muungano ni uhaini!.
Angalieni jf tusije nyooshewa vidole tuu wachochezi!.
Tukiamua kufuata sheria, taratibu na kanuni, muungano ni kwa bara tuu, kwa Zanzibar hauna legitimacy, hivyo kuuvunja from that side ni haki yao.Naunga mkono hoja!.Pasco.
Pasco, JF ikinyooshewa kidole nitashangaa sana! wale wa UAMSHO waliochoma hadi nyumba za ibada hakuna aliyeshtakiwa kwa uhaini. Mzalendo.net si tu wanatoa maoni bali wana video unazopaswa kuziangalia watoto wakiwa wamelala. Ni matusi kashfa tuhuma n.k

Tutauliza kama JF inachochea na ni uhaini,basi Jussa alitakiwa awe katika kifungo cha maisha n.k

Naunga hoja mkono

Let Zanzibar go, if possible July 1 2012
 
Mzee Mwanakijiji,
Nitakwambia haswa shiriki za kihisia zilizowakumba Wazanzibar...Na naweza sema ni swala la kiasili ambalo limetokana na utamaduni wetu pale ambapo imetumika hata ktk ndoa zetu hivyo kuwafanya Wazanzibar waishi ktk maisha ya What if?...


Ni kwamba zamani ktk ndoa zetu mwanamke akiolewa huchukuliwa kama chombo cha kutotoa watoto, kulea na kutunza nyumba lakini mwenye jina na familia na mali zote ni baba. Na ilitokea hata wakati baba amefariki basi urithi huchukuliwa na wanandugu wa Baba, na kumwacha mke arudi kwao hana kitu, hivyo ktk fikra za utamaduni huu mchafu wanawake wengi siku hizi hutazama kwanza maslahi yao. hata ktk mahari ya ya ndoa tu, huomba wajengewe nyumba, wafunguliwe biashara, wengine wakitazama utajiri wa bwana yote haya ni katika kujilinda wao na nasaba yao.- kule kwa baba na mama zao.

Wapo wengine huwaibia waume zao fedha ama kuficha baadhi ya mapato na matumizi ili apate kujijenga kwao kwa sababu mke huyu huishi kwa fikra za What if mmewe akimwacha atabakia na kitu gani? hufikiria kwamba ndoa yoyote haina guarantee ya kudumu hivyo lazima ajiandae yeye kuachika na familia yake ni kwa baba na mama yake sii mume. Na ktk utekelezaji wa fikra hizi utakuta familia haiwezi kuendelea kwa sababu Ufisadi unatoka ndani na NDIVYO TULIVYO.

Hivyo Wazanzibar kwa fikra zao wanataka bara tuwajengee makwao (tupeleke maendeleo Zanzibar), tuwafikirie wao kana kwamba ipo siku Muungano huu utavunjika na wao hawatakuwa wamepata kitu isipokuwa Bara ambayo imejijengea jina la ubwana. Na ukisikia vilio vyao kwa makini utagundua ni tamaa ya fikra za What if, maana wanazungumzia vitu visivyokuwepo leo, sijui Mafuta yasiwe ya Muungano lakini wanatumia Umeme wa bara bure wakati ni ktk wizara zile zile wasizotaka ziwe ktk muungano. Kifupi ni madai ya mke alopata kazi hataki kuchangia ktk matumizi ya familia kwa madai ya kwamba wewe sii mume kazi yako nini?..mbona wataka hata fedha za mke kuiendesha familia hapo wakimwona mume sii mwana familia ila mtu wa nje alokaribishwa ktk familia - Ni asili ya Wangazija na watu wa Pwani!

yaani umeandika upuuzi mtupuuuuu yaani kama ni mtihani bac 0+++=000000000000000000000, unajua watz wengi ni wajinga hawajui haki zao linapo kuja swala la kudai haki zao watawala ni rahisi sana kubadili upepo hoja sio nani ananufaika na muungano nani hanufaiki wananchi wa znz wanataka mabadiliko ya mfumo wa muungano wameona mfumo uliokuwepo hauna faida kwao je ni kosa kisheria?

Wanataka kura ya maoni iitishwe ili tusipoteze pesa na muda kuwalazimisha watu kuunda katiba wakati muungano wenyewe haupo kisheria kwa ujinga wetu watz maendeleo tutaendelea kuyaona kwenye tv tu aibu tupu
 
MMKJJ,
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, hoja yoyote ya kuuvunja muungano ni uhaini!.

Angalieni jf tusije nyooshewa vidole tuu wachochezi!.

Tukiamua kufuata sheria, taratibu na kanuni, muungano ni kwa bara tuu, kwa Zanzibar hauna legitimacy, hivyo kuuvunja from that side ni haki yao.

Naunga mkono hoja!.

Pasco.
Pasco, katiba ya JMT kwa sasa imakiukwa sana, i.e tuna makamo wawili wa rais vs chief minister.

Naunga mkono kwamba sasa wanzanzibari wafanye hima ili waipate nchi yao, ni haki yao kabisa, wasikubali kunyonywa tena na Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wasiojua ukweli wa mambo, msingi mkuu wa muungano ni dhima ya Nyerere na Karume in good faith!.

Baada ya dhima ikafuatia kitendo cha kuungana rasmi kwa kuchanganya udogo na kusaini zile hati za muungano.

Baada ya hapo muunngano huo uliridhiwa bara tuu (ratified) kwa bunge la Tanganyika kuupitisha mkataba huo uliokuwa na mambo 11 hivyo kupata nguvu za kisheria!.

Zanzibar nao walitakiwa kuuridhia mkataba huo wa muungano kwa kuuratify lakini jambo hili halikufanyika!. Hivyo wanasheria wangeweza kabisa kuishitaki Tanzania kwa kuipora mamlaka Zanzibar na kuikalia kimabavu miaka yote hiyo!.

Kufuatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria wa muungano kule Zanzibar, hivyo Wanzanzibar wako huru kujitoa kwenye muungano kwa amani kabisa kwa kung'ang'ana kuwa sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

Maadam Wanzanzibari wanacholilia ni haki na uhuru wao, nawaombeni tuwateende haki kwa kuwapatia wanachotaka.

Naiunga kauli ya Mzee Mwanakijiji kwa asilimia 100%, "Let them go!."
 
Kwa wasiojua ukwe wa mambo, msingi mkuu wa muungano ni dhima ya Nyerere na Karume in good faith!.

Baada ya dhima ikafuatia kitendo cha kuungana rasmi kwa kuchanganya udogo na kusaini zile hati za muungano.

Baada ya hapo muunngano huo uliridhiwa bara tuu (ratified) kwa bunge la Tanganyika kuupitisha mkataba huo uliokuwa na mambo 11 hivyo kupata nguvu za kisheria!.

Zanzibar nao walitakiwa kuuridhia mkataba huo wa muungano kwa kuuratify lakini jambo hili halikufanyika!. Hivyo wanasheria wangeweza kabisa kuishitaki Tanzania kwa kuipora mamlaka Zanzibar na kuikalia kimabavu miaka yote hiyo!.

Kufuatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria wa muungano kule Zanzibar, hivyo Wanzanzibar wako huru kujitoa kwenye muungano kwa amani kabisa kwa kung'ang'ana kuwa sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

Maadam Wanzanzibari wanacholilia ni haki na uhuru wao, nawaombeni tuwateende haki kwa kuwapatia wanachotaka.

Naiunga kauli ya Mzee Mwanakijiji kwa asilimia 100%, "Let them go!."
Mkuu Pasco, mimi shida yangu ni hapo kwenye red. Wadai kwa nani, kama hawajui la kufanya wamepewa ushauri wa bure. Hakuna mwenye uwezo wa kuwapa, hasa ukizingatia ni vigeugeu. Kwanza wakubaliane wanachotaka halafu yote yako mikononi mwao wenyewe!
 
Nawaunga mkono wazanzibari, wajitenge wabaki na nchi yao yenye ukubwa wa eneo za kilometa za mraba 2500, watuachie tanganyika yetu yenye ukubwa wa kilometa za mraba 943000.

Naunga mkono pia wazanzibari walioko tanganyika warudi zanzibar bila kudhulumiwa chochote katika kile wanachokimiliki, na pia naunga mkono watanganyika walioko zanzibar warudi tanganyika. Kwa wale watakaoamua kubaki katika nchi isiyo yao basi wakae kama raia wa kigeni, kwa visa maalum- na ofcourse hawawezi kuwa na haki sawa kama wenye nchi yao(raia).

Naunga mkono hoja pia kwamba, ni jukumu la wazanzibari kujitoa katika muungano wao wenyewe, uwezo wa kujitoa wanao, sasa sijui kwa nini wanazunguuka, wakati wakiamua kutumia vyombo vyao kama vile raisi wao, baraza lao la wawakilishi, serikali yao ya mapinduzi, wanaweza kabisa kujitoa.
 
yaani umeandika upuuzi mtupuuuuu yaani kama ni mtihani bac 0+++=000000000000000000000, unajua watz wengi ni wajinga hawajui haki zao linapo kuja swala la kudai haki zao watawala ni rahisi sana kubadili upepo hoja sio nani ananufaika na muungano nani hanufaiki wananchi wa znz wanataka mabadiliko ya mfumo wa muungano wameona mfumo uliokuwepo hauna faida kwao je ni kosa kisheria? wanataka kura ya maoni iitishwe ili tusipoteze pesa na muda kuwalazimisha watu kuunda katiba wakati muungano wenyewe haupo kisheria kwa ujinga wetu watz maendeleo tutaendelea kuyaona kwenye tv tu aibu tupu

wee iko na problem aisee! bongo yako haiko sawa kabisa.
 
Forget muungano,

The entire idea of a nation-state as alluded in it's genesis at The Peace of Westphalia in 1648 is going extinct.

This idea has been a foreign one that was shoved down our throats from the get go, and now that corporatocracy rules over nation-state sovereignty, and all the flying dual and trio nationalities, and hyphenated Tanzanians working in Canary Wharf and vacationing in Ibiza, it is becoming even less relevant. Lest I am branded an elitist, whether tomorrow or fifty years in the future, this is the trend.

I wrote extensively about this here at JF.

Search for Westphalia. We need to define things, not simply work with given definitions whose genesis did not have us in mind.
 
siku muungano utavujika, nawabie kwamba wa zazibari wataazisha madai megine, mtanibishia sababu wegi mnaburuzwatu hamwelewi mnafanyanya nii
 
Let Zanzibar GO! GO Go. Zanzibar!
Unfortumetelly though, who is a Zanzibari?
 
Kwa wasiojua ukweli wa mambo, msingi mkuu wa muungano ni dhima ya Nyerere na Karume in good faith!.

Baada ya dhima ikafuatia kitendo cha kuungana rasmi kwa kuchanganya udogo na kusaini zile hati za muungano.

Baada ya hapo muunngano huo uliridhiwa bara tuu (ratified) kwa bunge la Tanganyika kuupitisha mkataba huo uliokuwa na mambo 11 hivyo kupata nguvu za kisheria!.

Zanzibar nao walitakiwa kuuridhia mkataba huo wa muungano kwa kuuratify lakini jambo hili halikufanyika!. Hivyo wanasheria wangeweza kabisa kuishitaki Tanzania kwa kuipora mamlaka Zanzibar na kuikalia kimabavu miaka yote hiyo!.

Kufuatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria wa muungano kule Zanzibar, hivyo Wanzanzibar wako huru kujitoa kwenye muungano kwa amani kabisa kwa kung'ang'ana kuwa sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

Maadam Wanzanzibari wanacholilia ni haki na uhuru wao, nawaombeni tuwateende haki kwa kuwapatia wanachotaka.

Naiunga kauli ya Mzee Mwanakijiji kwa asilimia 100%, "Let them go!."

Pasco, Muungano uliridhiwa Zanzibar kama ulivyoridhiwa Tanganyika na vyombo halali vilivyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo na ambavo bado vipo. Wanaosema kwamba Muungano haukuridhiwa Zanzibar wanaandika historia upya; hawajui historia na hawataki kuijua.

Na Wazanzibari wengi hawajui kuwa muungano uliridhiwa kihalali kabisa. Ndio maana wengine tunaona huo muda wa kuwafundisha watu historia hatuna; kama wanataka kuondoka wafunge mizigo, mapakacha na waende; kuna mamia ya Watanganyika walio tayari kushika nafasi zao ambazo wanazishikilia bara.
 
Naomba kuuliza maswali mawili matatu ya kizuushi...kwa kuwa Zanzibar wanayo katiba yao, Raisi wao, bunge lao, serikali yao, bendera yao na wimbo wa Taifa lao na kwa kuwa bunge la Muungano halina nguvu huko;

  1. Ni mamlaka gani hiyo wanayoililia kuwa inawabana mpaka wanashindwa kupumua?
  2. Ni mamlaka gani hiyo inayowashurutisha kubaki ndani ya Muungano kama hawaupendi?
  3. Ni mamlaka gani hiyo inayoizuia Zanzibar kuendesha kura ya maoni kuhusu Muungano?
Mimi naamini kuwa kisiki kinachowakwamisha katika madai yao ni wao wenyewe Wazanzibari kupitia katiba yao, Raisi wao, wawakilishi wao na serikali yao. Kwa nje wanapiga kelele kuwa hawautaki Muungano lakini ndani mioyoni mwao wamemganda Mtanganyika kama kupe ili wazidi kuneemeka kwa chenu chetu lakini chetu chetu!

Wanaogopa kura ya maoni, jambo lililo ndani ya uwezo wao, na badala yake kutafuta kisingizio na kuanza kuwanyooshea vidole watu wasiohusika. UAMUSHO, kwa kutambua huu ukweli kuwa hawawezi kuwashawishi Wazanzibari kupitia ama viongozi wao au serikali yao, hasira zao wanahamishia kwa Kanisa na Watanganyika.

Rai yangu kwa Wazanzibari ni kuwa kama kweli hamuutaki Muungano, njia ni nyeupee...fungasheni virago muone kama kuna Mtanganyika hata moja atakayewalilia. Lakini hii ya kujaribu kukwepa mapungufu na ulafi wenu wa kutaka huku na kule mwataka, uvumilivu wa Watanganyika unakaribia kikomo kwa chokochoko na matusi yenu.
 
Mkuu Pasco, mimi shida yangu ni hapo kwenye red. Wadai kwa nani, kama hawajui la kufanya wamepewa ushauri wa bure. Hakuna mwenye uwezo wa kuwapa, hasa ukizingatia ni vigeugeu. Kwanza wakubaliane wanachotaka halafu yote yako mikononi mwao wenyewe!
Shedafa, kwa vile muungano uliundwa in good faith, vivyo hivyo tuuvunje in good faith!. Wabara walioko Zanzibar wale watakaotaka kurejea, wabebe vinavyobebeka na visivyobebeka tuwaachie zawadi ndugu zetu.

Wale wa bara wenye mizizi Zanzibar, wasifukuzwe bali waachwe, wakipenda kupewa uraia, wapewe na wale wanaopenda uraia wao wa bara, then wapewe resident permits kama wageni!.

Vivyo hivyo, Wanzanzibari walioko huku bara, wale wenye mapenzi ya kubaki bara, kwa sababu zozote zile, wasibughudhiwe wao na mali zao na biashara zao, waachwe huru kuamua kurudi au kubaki.

Watakaoamua kurudi, vile vinavyobebeka, wabebe kilicho chao na visivyo bebeka, wavitoe zawadi kwa ndugu zao!.

Watakaomua kubaki pia watakaotaka uraia tuwape, wasiotaka uraia tuwape resident permit kama wageni wengine wote.

Kwa sisi ni ndugu wa damu, hakuna viza kuingia Zanzibar au kutoka Zanzibar kuingia bara!.

Spirit ya kuvunja muungano iwe smooth with no hurt feelings na tena sisi tuwandee wema ndugu zetu hawa hata kama wao wametutenda!.

Nawaombeni sana tusiwaadhibu Wanzanzibari na Wapemba walioneemeka na muungano kwa makosa ya mafaatani, vichaa na wendawazimu wachache wasiowatakia mema wenzao!.

Let them go!.
 
Kila nikifikiri naishia kuamini kuwa wanzanzibari "wengi" walitaka/wanataka serikali tatu, yaani Serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika na serikali ya muungano. Haya yalikuwa mahesabu kama yangekubalika basi wangepata 'vyote' zanzibar huru, na ATM! Maana hainiingii akilini kwa nini wawe na power ya kubalisha katiba yao, wawe na bendera, wimbo lakini washindwe kusema 'sisi ni taifa huru'. Shida iko wapi?

The sooner the better, tumalizane haya mashauri ili mipango mingi na ya gharama kubwa iliyo chini ya muungano iangaliwe upya. Tuna vitambulisho vya utaifa, tuna tume ya katiba. Hivi vyote viko kwenye level ya muungano. Ni vema tujue moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom