Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Nyie midebwedo msio na machogo hebu msijisumbue kwani ss bara hatupo tayari kuachia koloni letu zenji kwani lina mafuta na gas..

Chezea wabara weye....
 
Pasco, JF ikinyooshewa kidole nitashangaa sana! wale wa UAMSHO waliochoma hadi nyumba za ibada hakuna aliyeshtakiwa kwa uhaini. Mzalendo.net si tu wanatoa maoni bali wana video unazopaswa kuziangalia watoto wakiwa wamelala. Ni matusi kashfa tuhuma n.k

Tutauliza kama JF inachochea na ni uhaini,basi Jussa alitakiwa awe katika kifungo cha maisha n.k

Naunga hoja mkono

Let Zanzibar go, if possible July 1 2012

MUAMUSHO WAMECHOMA nyumba za ibada hii nyimbo inaimbwa na makanisa pamoja na magazeti yao , hawana ushahidi wowote wa hilo na wanajua ni nani kachome wamebakia kujifanya kulalamika humu kwenye mitandao na kwenye magazeti yao , soma kilichotokea

Jabir Idrissa

KUNA uhalifu umefanywa Zanzibar. Ni katika matukio mabaya yaliyoanza usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Watu wamechochewa kupambana na dola. Hili halijaelezwa na serikali. Polisi wamevamia nyumba za viongozi wa Uamsho na kuvunja milango huku wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi na familia zao sambamba na kuwatishia maisha. Polisi hawajalieleza hili. Amir (kiongozi) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed Hadi anasema usiku wa Jumamosi hiyo, akiwa kwake, alipata taarifa anafuatwa na polisi wa kuzuia fujo (FFU).
trans.gif
trans.gif


Akajiandaa. Mnamo saa 7.30 kweli wakafika. Wakataka mlango ufunguliwe. Hakuna aliyewatii. Wakarusha risasi hewani. Hakuna aliyetoka. Hakuna aliyepiga kelele kutokea ndani. Lakini, baada ya kuona vishindo vimezidi, Sheikh Farid akasema kwa sauti, "Nipo ndani na familia yangu tumepumzika. Kama mpo tayari, fanyeni chochote nje ila, ninaapa kwa jina la Allah, anayekuja ndani, tutakabiliana mimi sina bunduki."

Polisi hawakujali. Wakafyatua mabomu. Wakavunja mlango na kuvuruga walivyovikuta nje. Wakataka kuingia ndani. Wakakatazana, "hapana. Mnajua nani wamo ndani? Tuondokeni." Wakaondoka, anasimulia Sheikh Farid. Amepata simulizi kama hizo kwa viongozi wenzake wa Uamsho. Lakini sokomoko kama lililomkuta, lilitokea nyumbani kwa naibu wake, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, wakati mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.

Sheikh Azzan aliporudi Ijumaa, akapewa taarifa na familia yake kuwa walifika polisi wa FFU na kufanya fujo. Walifyatua risasi nje, wakavunja mlango. Wakapiga mayowe ya kumtukana matusi yeye na familia. Wakaondoka. Hakutulia. Alikwenda kupiga ripoti kituo cha polisi Mfenesini, karibu na anapoishi. Wakuu wakakana kufika kwake. Wakasema askari waliomfuata walitoka Mwembemadema.
Mwembemadema ni makao makuu ya polisi mkoa wa Mjini Magharibi.

Hawa ndio waliotuma makachero Jumamosi ile wakamshike Ustadhi Mussa Juma Issa, mmoja wa wahadhir wakuu wa Uamsho, kipenzi cha wahudhuriaji wa mihadhara ya jumuiya hii inayohamasisha Wazanzibari kuukataa muungano.

Wapo watu wamejitokeza kutoa ushahidi wa walivyoona polisi wanalipua nyumba na mali za vitegauchumi za raia wema, zikiwemo gari zilizoegeshwa Kisiwandui na Michenzani.

Mwanamke anayefanya kazi shirika la ndege la Kenya Airways, gari yake iliteketezwa kwa bomu lililorushwa na polisi. Matukio yote hayo katika siku mbili – Jumamosi na Jumapili.

Leo, taarifa zimepatikana za uhalifu wa Polisi uliofanywa Jumatatu, 28 Mei, muda mfupi baada ya watuhumiwa 30 wa fujo, walipoachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar. Kati yao wapo viongozi wawili, akiwemo Ustadhi Mussa, wa Uamsho.
Wakati wakili wao, Abdalla Juma akiwa Mahakama ya Ardhi, Vuga, vijana wa FFU walivamia ofisi zake Amani, yapata kilomita tano kutoka Vuga. Wakapitisha mitutu ya bunduki madirishani na kufyatua risasi na mabomu ya machozi.

Hawakujali wafanyakazi waliokuwa ndani. Ni mchana kweupe. Hapana, ni mchana wa mola muumba mbingu na ardhi siku ya kazi, Jumatatu. Ipo taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kulalamikia kitendo hicho. Wamemtumia barua Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, na kumtaka asake wahusika na kuwashitaki.

ZLS wamekiita kitendo hicho cha makusudi kilicholenga kutisha mawakili wasiwe imara katika kazi yao ya kutetea wananchi wanaposhitakiwa. Polisi wanatuhumiwa sasa kushiriki vitendo vya uhalifu katika kipindi kilekile ambacho wao wanatuhumu Uamsho kuzusha ghasia mjini Zanzibar.

Ninayaeleza haya ili kukumbusha historia ya kisiasa Zanzibar inayochefua. Siasa za maridhiano zilizoanza kustawi tangu 2010 mwishoni, zinachafuliwa kwa nguvu. Ni kama zilivyokuwa zikipandikizwa na kustawishwa siku zile za giza, mara tu mfumo wa siasa za vyama vingi, siasa za ushindani, uliporudishwa chini ya sheria ya Tanzania.

Sasa wapo wasiotaka amani Zanzibar idumu. Wapo. Pengine wanampenda Amani Abeid Karume, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ambao walizijenga, bali wanachukia matunda ya maridhiano.

Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Hapana; si peke yao.

Kwa jumla, vyombo vya dola, vya dola, vya dola. Dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola. Vyote vilitajwa kupandikiza chuki kwa wananchi, mgongo ukiwa vyama vingi na uimara wa CUF. Visima vikapakwa kinyesi, ofisi za umma zikawashwa kwa viberiti na makanisa yakachomwa kiajizi. Kanisa linawashwa, dakika mbili tu hao walinzi wamefika.

Ushetani ule ukakoma pale wananchi wa Shengejuu, kaskazini Pemba, walipovizia usiku kutafuta nani hasa wakihusika na vitendo vile vya kiharamia. Waliokutwa mpaka leo Polisi hawajawataja.

Ni askari polisi na mashushushu ndani ya Landrover iliyosheheni madumu ya petroli, mapipa ya kinyesi na viberiti vya kuwashia mabomu ya chupa.

Kutaka kuzubaisha umma wa Watanzania na ulimwengu, IGP Omari Mahita akaunda kikosi kuchunguza. Akamteua Robert Manumba, kachero aliyekuwa msaidizi mkuu wa DCI Adadi Rajabu, kukiongoza.

Alitaka wachunguze chimbuko, sababu na wahusika wa milipuko ile ya kishetani pamoja na vitendo haramu vya kupaka kinyesi madarasa na kukimwaga kwenye visima vya maji wanayotumia wananchi.

Tangu wakati ule, karibu miaka kumi sasa, si DCI Manumba ambaye sasa ndiye DCI, si IGP Mahita wala serikali iliyotoa ripoti ya uchunguzi huo.

Wananchi waseme nini hapo?

Lakini kwa sababu wahusika walijulikana na kufikia kukamatwa Shengejuu, zile fitna kuwa CUF walikuwa wahusika, zilifutika.
Tungalinao wakorofi wasiopenda maridhiano.

Wahafidhina ndani ya CCM wameibuka upya wakitaka kuharibu amani na utulivu. Hawawezi kuitaja CUF moja kwa moja maana wanashirikiana nacho kuendesha serikali.


Wametafuta pa kuingilia – Uamsho. Kwa kuwa taasisi hii imechukua jukumu la kupigania haki za wananchi wasioridhishwa na mwenendo wa muungano, wanawapakazia kuwa wanavunja amani.

Kumbe bado kuujadili Muungano wa Tanzania ni uhaini. Pamoja na serikali kuruhusu Watanzania watoe maoni yatakayotumika kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watawala hawapendi watu wafikiri tofauti na wao.


Tunaona kila viongozi wa polisi wanavyojitahidi kupotosha ukweli wa kilichotendeka mjini Zanzibar, ile dhamira yao ya kupotosha inawarudia. Wanatajwa baada ya kuonekana wazi wakivamia na kuharibu mali ikiwemo ofisi za wanasheria.

Mpanga ubaya mwisho humrudia. Hawajajisafisha, wamejiumbua. Na ndiyo matokeo ya polisi nchini kushabikia siasa. Wanasubiriwa watamshika nani mchoma makanisa. Bado watafute ushahidi kuthibitisha kesi ya watu 30, pamoja na wafadhili wa Uamsho.
 
nyie uzao wa watumwa ebu pumzikeni sasa, kila siku kelele tu!!. Dunia gani itakayowasikia nyie, hivi mnadhani Zanzibar huko nje wanaitambua kuwa ni nchi? Hata mkiandamana nchi za nje wanajua kuwa kitongoji kimojawapo ndani ya Tanzania ndo kimeandamana.
 
Pasco, Muungano uliridhiwa Zanzibar kama ulivyoridhiwa Tanganyika na vyombo halali vilivyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo na ambavo bado vipo. Wanaosema kwamba Muungano haukuridhiwa Zanzibar wanaandika historia upya; hawajui historia na hawataki kuijua. Na Wazanzibari wengi hawajui kuwa muungano uliridhiwa kihalali kabisa. Ndio maana wengine tunaona huo muda wa kuwafundisha watu historia hatuna; kama wanataka kuondoka wafunge mizigo, mapakacha na waende; kuna mamia ya Watanganyika walio tayari kushika nafasi zao ambazo wanazishikilia bara.

haya mbona unayaandika hapa tu huwezi weka muhadhara ukawaambia watu haya ??? unakimbilia JF na Magazetini tu !!!

Mbona waliokuwemo katika system tokea kuundwa Huo Muungano , wengine wahai wanasema vyengine???
 
Ndugu yangu Kwamwewe, uhalifu wa kuchoma moto umetokea mara 25. Siyo SMZ au UAMSHO wanaokanusha.
Watanganyika wamechomwa moto na wahalifu wameachiwa huru.
Hili la kuchoma moto linatokana na uchochezi wa lugha za 'Wakristo na muungano'
Ni mwendawzaimu peke yake atakayesikiliza hadithi za 'Alshabaab' za kukanusha upuuzi.

Huko tumeshatoka na sasa tunasema
Let Zanzibar Go!

Tuna vijana wetu kwa maelfu sasa wanjipanga kuchukua nafasi zao halali ndani ya nchi yao siku Wazanzibar watakapobeba mizigo.

Wazaznzibar walikuja na mabegi na wanapaswa kuondoka na mabegi na Watanganyika pia walioko huko wataondoka na mabegi. Hakuna Mzanzibar aliyekuja na nyumba au ardhi.

Let Zanzibar go sasa haina kurudi nyuma.
Hakuna serikali 3, mkataba wala ushirikiano. Ushirikiano ni kama ule wa Kenya au Malawi

It is time, we're tired. Let Zanzibar go!
The mantra should be Let Zanzibar go.
 
nyie uzao wa watumwa ebu pumzikeni sasa, kila siku kelele tu!!. Dunia gani itakayowasikia nyie, hivi mnadhani zanzibar huko nje wanaitambua kuwa ni nchi? Hata mkiandamana nchi za nje wanajua kuwa kitongoji kimojawapo ndani ya tanzania ndo kimeandamana.

wewe ungalikuwa mtumwa hata mimi ningalikutoa bure maana huna thamani yoyote huwezi kuuzika maana uwezo wa kufikiri huna
 
Pasco, Muungano uliridhiwa Zanzibar kama ulivyoridhiwa Tanganyika na vyombo halali vilivyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo na ambavo bado vipo. Wanaosema kwamba Muungano haukuridhiwa Zanzibar wanaandika historia upya; hawajui historia na hawataki kuijua. Na Wazanzibari wengi hawajui kuwa muungano uliridhiwa kihalali kabisa. Ndio maana wengine tunaona huo muda wa kuwafundisha watu historia hatuna; kama wanataka kuondoka wafunge mizigo, mapakacha na waende; kuna mamia ya Watanganyika walio tayari kushika nafasi zao ambazo wanazishikilia bara.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

Sio lazima kila mkataba uwe ni wa maandishi, lakini mkataba wowote wa ardhi, land au pango, lazima uwe wa maandishi!. Wewe unaweza kununua gari na kumzawadia mpenzi/mke/ ndugu au mzazi kwa kauli tuu na ukawa ni mkataba halali!.

Lakini kama una land yako, ukiamua kumzawadia yoyote, hata ukimzawadia kwa kauli, lazima maandishi yafuatie ndio yatakayo halalisha hiyo kauli!.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

Tumewanyanyasa sana, its about time now, we just lets them go!
 
Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.!

Muumini wa sera ya majimbo, hili neno, umetumia taaluma yako leo at least.
Natumai shule ulioitoa MMKJ ameielewa!
 
Mmh! nakula nondo tu hapa....sitii neno lolote leo ila najifunza vitu fulani kupitia uzi huu wa Mwanakijiji.
Wale wenzangu na mimi wa Mzalendo.net nawaombeni njooeni huku muangalie watu wanavyojua kujenga
hoja za nguvu! siyo nyinyi kazi yenu kushupalia udini tu kwenye mtandao wenu wa Mzalendo.net na ham
jui kujenga hoja. Back to the topic....tuendelee wana jamvi- nawasoma taratiiiiibu!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

Tumewanyanyasa sana, its about time now, we just lets them go!

Mkuu hapo nilipoweka rangi nyekundu umechanganya madawa/ umefanya madudu.

Isomeke Bunge la Tanganyika lilifuata sheria na katika kufuata sheria pia ilivunja sheria kwani baada ya sheria ile Bunge la Tanganyika halikukaa tena kama Bunge la Tanganyika. Nani aliwapa uwezo wa kuiua serikali ya Tanganyika na Bunge la Tanganyika?

Pia isomeke Muungano ni wa Tangayika tu. Hakuna nchi iliyoitwa bara au inayoitwa bara. Usifuate siasa za kisanii/ mazingaombwe.

Jikumbushe jina la Muungano. Lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na lilipofupishwa likawa Jamhuri ya Muungano wa TanZanIA.
Mazingaombwe/ kiini macho tu ndio yataleta neno bara.

Sio nia yangu kuanzisha mjadala katika hili lakini tusiwachanganye wananchi na wasomaji wa JF.

Let us call spade a spade!
 
Huu muungano wa kupe na ng'ombe wapi na wapi. kupe anataka kujitenga lakini ng'ombe ambaye ndio tanganyika unakataa badala ya kushangilia. mie naunga mkono. GO ZENJI GO! RASILIMALI ZENU ZA UROJO NA KARAFUU HATUZITAKI ACHILIA MBALI HAYO MAFUTA MNAYODAI YAPO. na wakiondoka mipaka iimarishwe kwa sababu mie nawaona kama somalia tu hakuna tofauti
 
wewe ungalikuwa mtumwa hata mimi ningalikutoa bure maana huna thamani yoyote huwezi kuuzika maana uwezo wa kufikiri huna
Niwe mtumwa kwani mimi nimekuambia ni Mzanzibar??. Wewe huoni watumwa jinsi wasivyojiamini kila siku kelele tu kuwa wanaonewa.
 
Mwanakijiji kwenye hii clip una la kusema tena?ni kwamba watu wanataka nchi yao ambayo mmeikalia kimabavu..
[video=youtube_share;hyIRz6fGenY]http://youtu.be/hyIRz6fGenY[/video]
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

Pasco na wewe umeendelea kuamini porojo kuwa 'muungano haukuridhiwa Zanzibar'; chombo halali cha Zanzibar (siyo Karume tu kama wengi mnavyotaka tuamini ) kiliridhia muungano. Wanaosema muungano haukuridhiwa Zanzibar wanakana historia.
 
Sioni sababu ya kuendelea kuwabembeleza Wazanzibari. Mtoto akitaka wembe mpe umkate! Hatutaki watu wa kujitoa mhanga kujiripua huku Tanganyika kisa ni wapigania uhuru wa Zanzibar. Watimue! Tunashindwa kupumua!
 
Mwanakijiji kwenye hii clip una la kusema tena?ni kwamba watu wanataka nchi yao ambayo mmeikalia kimabavu..

Nope nililolisema ndio nimelisema. Sasa hivi malalamiko yao ya kutawaliwa, kunyonywa, kunyanyaswa hayana msingi tena. Wakitaka kutoka njia ndio hizo tumeziweka wazi wao tu waamue ili wataitumia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom