Leo ni leo huku kwetu Arusha (Mkutano wa CHADEMA)

watu wanazi kumiminika hapa kwenye uwanja huu wa NMC

tuhabarishe mkuu, kwenye yale maandamano nilikuwepo uwanjani tukapigwa mabomu nikakimbilia ile njia ya kuelekea fire, nipo dar asaiv, sipati picha hapo uwanjani.
 
Nasikitika sitaweza kuhudhuria mkutano mzuri kama huu,kazi zimenibana ila nipata simu toka katikati ya mji mambo ni mazito.
 
pia nami nimetoka moshi kwajili ya kutoa info za matukio yote ya mkutano wa chama makini sana chadema
 
na sisi madiwani tuliofukuzwa chadema tutafanya mambo yafuatayo:
1. tutakwenda mahakamani kupinga udikteta uliofanywa na viongozi wa chadema kutufukuza chaguo la wana Arusha

2. tutaandaa mkutano mkubwa jijini arusha ili kujibu mapigo ya mkutano wa leo pia kuwaeleza wananchi kinaga ubaga nini kinaendelea ndani ya chadema, na mchakato wa uchaguzi ulivyoenda na maovu yanayofanywa na Lema kuhujumu Arusha

Huo mkutano utaenda wewe na familia yako
 
MODs ningeshauri hii thread ipelekwe jukwaa la siasa ili watu wengin wafaidike nayo.
 
<br />
<br />
hiyo ni baraka kwani maji ni uwepo wa uhai wa viumbe wa Mungu duniani na ili vimtukuze.so mkutano unabaraka zote kutoka juu.mbarikiwe sana hiyo ni nguvu ya umma na ni nguvu ya Mungu.
Leo hakuna mabomu naona vijana wamejifunga vitambaa vyeupe kama siku hiyo
 
Tunaomba picha na uploaded speech or movie kwa hili tukio la Arusha. CHADEMA mko sawa, msinge wafukuza madiwani waasi hakuna mtu angewaelewa. Big Up CDM you are showing a way and maturity.
 
<br />
<br />
mkuu nipo maeneo ya karibu hapa aq nasubiria shughuli ianze pamoja man

tuhabarisheni wakuu! naikumbuka sana siku ya mabomu na siku tulipowaaga wahanga wa mabomu ya arusha. wimbo wa Taifa ukiimbwa kibwagizo ni Mungu ibariki CDM
 
Umati hapa ni mkubwa sana kila mahali ni bendera na vijana waliovaa magwanda.
Kuna mmoja amebeba bango limeandikwa "TULIWACHAGUA KWA KUWAAMINI, MMETUANGUSHA KWA KUPENDA MATUMBO YENU, NA KUSAHAU DAMU ILIYOMWAGIKA"
 
Back
Top Bottom