Leo tarehe 26/08/2011 ndio siku ya mwisho ya Vikao vya mjadala wa Bunge la Bajeti. Kumbukumbu sahihi zinanionyesha kuwa kikao hiki cha leo ni kikao cha 57, ya kikao kikubwa cha 4 la Bunge la 9. Mengi yamezungumzwa, tumeshuhudia mijadala mikali na yenye ukinzani mkubwa kama vile..

1. Kukwamishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini,

2. Kuongezwa billion 95 katika wizara ya uchukuzi,

3. Kusimamishwa kazi na kuundwa tume ya bunge juu ya sakata la Nd. David Jairo-Katibu mkuu wa wizara ya nishati,

4. Sakata la uhuzwaji holela wa UDA (Shirika la usafirishaji dar es salaam),

5. Mvutano mkubwa kati ya wafanyabiashara wa mafuta na Ewura as wel as serikali,

6. Kusimamishwa kazi kwa Afisa wanyamapori kwa sakata la twiga walioporwa kwenda Qatara

7. Sakata la ununuzi wa Rada na report toka kitendo cha kijasusi cha upelelezi cha Uingeleza-SFU

8. Ongezeko la mshahara la 8.6% kwa wafanyakazi wa umma na ongezeko la kima cha chini kutoka sh. 135,600/= mpaka 151, 000

9. Kuletwa kwa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano

10. Kujiuzuru kwa pacha mmoja kati ya RACHEL Bw. Rostam Azizi,

11. Kufariki kwa Mbunge Mussa Silima (Rest In Peace).

Katika hayo na mengine mengi HEBU KWA PAMOJA TUFANYE TATHIMINI JUU YA UNDENDAJI KAZI WA BUNGE HILI.

Nawasilisha!

namba 4 ni kuuzwa si kuhuzwa