Leo Bunge linaahirishwa, una maoni gani?

<font size="4">Baadhi ya wabunge wakapime afya zao</font>
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Yule ambaye huzunguka na gari lenye wasanii wengi wakati wa kampeni, mwenye kitambi kikubwa kuliko wote awe wakwanza!
 
je ungependa.... Magamba ni ze comedy tosha, upeo wao mdogo mno walikuwa wanatetea chama mda wte badala ya kuweka maslahi ya taifa mbele,
 
Kwa wale wa Prof. MAGHEMBE, hivi ameshawah hata kuuliza swal la nyongeza kama alishndwa la msing.
NB. Juz zilibuka tetes za prof. Mwandosya kujiuzulu. Kuna habar mpya?. Nijuzen wanaJf.
 
Kwa kifupi asilimia 98 ya wabunge wa ccm ni wasaliti wa nchi hii na hivyo mimi sitegemei jambo jipya sababu kama ili bajeti ya wizara ipite inatolewa ruswa sasa huoni kwamba hata hiyo pesa ikishatoka haitatumika ipasavyo?,mimi naamini hakuna asubuhi ktk nchi hii endapo ccm itaendelea kushika dora kama ilivyo sasa tunapokamilisha miaka 50 ya Uhuru ambapo wenzetu tuliopata nao uhuru kwa asilimia kubwa wametuacha mbali sana ambao hata rasilimali tulizo nazo tunawazidi mbali sana,hivyo aidha wabadilike au waachie vyama vingine.
 
Nawashauri baada ya Bunge warudi MAJIMBONI MWAO siyo kuzurura DAR watimize ahadi walizo ahidi wajue tunazikumbuka zote na hasa hawa watokao MBEYA !!!
 
Tunataka Taarifa jumla ya gharama zilizotumika kuwalipa wabunge kwa ujumla wake ili tufanye Tathmini kama kuna relation yoyote juu ya kiasi walichoingiza na kazi waliyoifanya.
 
Leo bunge linafikia tamati hadi msimu mwingine. Je, mbunge wako amekuwakilisha ipasavyo au ameenda kulala? Nini kifanyike? Bunge limetimiza wajibu wake?
Ha ha haa! Hii topic uloanzisha ni nzuri sana. Comedy! Tutakimiss sana kile kibwagizo cha naunga mkono hoja mia kwa mia baada ya kusema yafuatayo, "Mheshimiwa spika, Jimboni kwangu wananchi watano wameuawa na askari wa wanyama pori, Nyaya za umeme zimepita katika kata kumi na nane katika jimbo langu na hakuna hata kijiji kimoja chenye umeme, Ni asilimia mbili tu ya wapiga kura wangu wanapata maji ya bomba toka seminari ya ................, Jimbo langu lina kilometa sita tu za barabara ya lami, mwaka uliopita kinamama sabini na mbili walijifungulia barabarani kwa kukosa usafiri wa kuwawahisha kituo cha afya, Wananchi wangu waliohamishwa eneo la mgodo mwaka 2004 bado wanaishio katika jengo la mahakama. Hii inaonyesha Serikali yetu ni sikivu na inawajali wananchi wake. Naunga mkono hoja mia kwa mia."
 
Back
Top Bottom