Lema kupanda kizimbani pamoja na viongozi wa CHADEMA wa Arusha mjini

Break news: mbunge wa arusha mjini Godbless Lema apelekwa jela: aacha waraka waukombozi kwa wananchi wake na watanzania wote soma waraka hapa:

JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.
Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu ...wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi. Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi .
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!.
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.
Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu. Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasa
bila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ," JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu. Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.
Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011. (Posted in facebook by Kilewo on John John Mnyika group)

Kama ni waraka wa Lema kweli, je kuna haja ya kulalamika au kusikitika au ilikuwa ni dhamira yake kuona kama sheria za nnji zinafanya kazi au ni legelege?...... (Mungu ibariki Tanzania)

Jeshi la Police Arusha majuzi baaday a kuwalinda baadhi ya viongozi wa UVCCM katika uzinduzi wa Kata na kuhutubia na Police walikuwepo wakitoa usalama na baadae Police wakaruka na kusema UVCCM MKiti James Millya Natafuta na Police kwa kutoa maneno ya kashifa kwa mtoto wa Rais JK anaitwa Ridhwani na kuhutubia bila kibali sasa Police hawa watupe taswila hizi mbili kwa CDM Mbunge Lema alitoka kwa Miguu kurudi officen kwake hii ni hali halisi ambayo kila audhuriapo mahakamani huwa anarudi kwa miguu akiwa na wafuwasi wake lipi kosa hapo ? Je Police wanatumia nguvu kuwalazimisha wananchi ndio huo Udictator au?

My Take;

Police ndio Chanzo cha vurugu ndani ya nchi hiii wameshindwa zuia sukari kutoroshwa katika mipaka yetu wao wanakuja kamata rais wanao tembea pammoja sipati picture kamili hapo.

Mechi ya simba na yanga watu wamerudi wakishangilia ambao ndio ulikuwa ni balaaaa zaidi je kama wenzao wange amua kuwa rushia mawe kwa kuzomewa lakini haikutokea iweje hii ya wafuwasi wa CDM kuambatana na mbunge wao akitokea mahakamani kwenda officen kwake nyie mseme ni maandamano?

Viongozi wengi baada ya kutoka mahakamani huwa kuna attendence ya waandishi wa habari kuwauliza kuhusu kesi au kumuuliza kiongozi muhusika aliye toka mahakamani ana nini la kusema juu ya kesi yake leo hii police yetu ndio wa kwanza kuivunja sheria ya nchi kwa kuficha mapungufu yao ya kiutendaji. Police wetu wanaongoza kwa kukamata rai wasio na makosa na kushindwa kukamata raia wanao vunja kanuni za nchi kama huko rombo kagera sukali inavushwa mipakani Police wapo wananangalia mpaka leo hatujasikia wakina nani wametajwa kuhusika na hiyo kesi ila ukipitia kwenye mabank unaona transaction za watu zina ongezeka kila after two weeks na hakuna mtu anajiuliza vipi mbona huyu mtu akija akirudi tena account yapanda ni biashara gani ya week mbili ina ingiza 20mils esp mikoa ya kanda ya ziwa na kilimajaro arusha?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom