ze encyclopedia
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 316
- 180
mmmh...T2015 CDM mbombo ngafu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda mpaka leo hajatoa majibu ya kilio cha wananchi wa Izimbwa wilaya ya Bukoba vijijini waliomtuhumu jaji Gabriel Rwakibarila kuhonga viongozi wa kijiji na kupewa ardhi bila kufuata taratibu za kisheria.
Pinda alisema atafuatilia,hii ni wakati wa ziara yake Feb 2011 alipofika katika kijiji cha Izimbwa.Huu ni upande wa pili wa jaji wa Kesi ya Lema.Kidumu Chama Chetu
Sijawahi ona presidential press service ya kipuuzi kama ya tanzania inayoongozwa na Salva Rweyemamu wanashindwa hata kujifunza kwa wenzetu wa Kenya!real sijapata waelewa hawa jamaa wanatumia kodi zetu bure very incompetent department at the state house.kuna mengi mazito ambayo walipaswa kutoa respose hata hili la Mheshimiwa Lema lilihitaji response ya haraka kiasi hichi shame upon you Id**ts of magogoni!
Waziri Mkuu Mizengo Pinda mpaka leo hajatoa majibu ya kilio cha wananchi wa Izimbwa wilaya ya Bukoba vijijini waliomtuhumu jaji Gabriel Rwakibarila kuhonga viongozi wa kijiji na kupewa ardhi bila kufuata taratibu za kisheria.
Pinda alisema atafuatilia,hii ni wakati wa ziara yake Feb 2011 alipofika katika kijiji cha Izimbwa.Huu ni upande wa pili wa jaji wa Kesi ya Lema.Kidumu Chama Chetu
Peter Saramba na Mussa Juma, Arusha
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema, jana aliweka wazi jambo alilodai siri nzito pale alipoeleza kuwa mwaka 2007 alikutana na rais Jakaya Kikwete katika kikao maalumu ambapo alimwomba akubali kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, ombi alilolikataa na kudai ni moja ya sababu ya chuki iliyotumiwa na dola kumvua ubunge.
Akizungumza kwenye ofisi za Chadema, mkoa wa Arusha mara baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua matokeo yaliyompa ushindi jana, Lema alitaja viongozi wengine wa serikali waliokasirishwa na misimamo yake akiwa bungeni ambao alielezwa wameahidi lazima avuliwe ubunge kuwa ni paoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Alsisema hata baada ya Dk. Baltilda Burian keteuliwa kugombea kupitia CCM pia alitumiwa ujumbe kumtaka ajitoe kwa ahadi ya kutafutiwa nafasi ya uongozi serikalini lakini pia alikataa hivyo Rais pamoja na viongozi wengine walimwekea chuki na kuahidi kumshughulikia, hivyo anaamini hukumu hii ni moja ya ahadi ya kushughulikiwa aliyoahidiwa.
Source: Mwananchi 06/04/2012
My take:
1. Hii imekaaje wakuu, kuna ukweli!?
2. Je, kabla Idara ya Mawasiliano ya Ikulu kutoa ile taarifa yake ambayo wengi wanasema haina hata hadhi ya kuwa taarifa ya serikali ya kijiji, waliyajua haya?
3. Je mambo yakishaonekana hivi ni busara wananchi nao kukaa kimya kwa kila kilichozoeleka kuwa serikali imesema?
Kama maswali haya hayajibiki ni wazi utawala uko likizo.