Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Mimi sijaona jambo la kusifiwa kwa lema hapo.kwani mwanzo ni nani walifikia muafaka mpaka yeye akakataa?hapo naona uhasama unanukia ndani ya chadema.
 
Huyu Lema hana mapenzi mema kwa wananchi wa AR town, kwani wakubwa zake akina Mbowe walishafikia muafaka sasa yeye anaturudisha nyuma. Wana CDM mpelekeni Lema Milembe akapafanyiwe uchunguzi wa AKILI. Kila siku yeye analeta shari!
 
kwa mtaji huo basi CDM kuna ufa mkubwa sana. huyo naibu meya na hao viongozi wa kamati (e.g. fedha) si ni wanachama pia? nani ni nani hapa? kati ya waliochaguliwa, Lema na CDM?

in any case kuna CDM members walikuwa involved hivyo sauti ya chama ndiyo ya muhimu hapa
 
Hivi CDM kila mtu ni msemaje? Ngoja tuone kati ya Mbowe na Lema na zaidi
 
Mimi sijaona jambo la kusifiwa kwa lema hapo.kwani mwanzo ni nani walifikia muafaka mpaka yeye akakataa? hapo naona uhasama unanukia ndani ya chadema.

Ni nani walifikia muafaka mpaka yeye akakataa? Ni CCM lakini imekula kwao. Kama siku zote wanafanikiwa kwa wapuuzi wenzao hapo sasa watuambie wenyewe CCM, huu mwafaka umefikiwaje yaani waliohusika na mchakato ni akina nani? Na hatima ya masuala ya kesi bandia, mauaji ya raia na udhalilishaji yako vipi kwenye muafaka? CCM is awful

I voted for you Lema na hayo uliyoyasema ndiyo matarajio yangu kwa Mbunge wangu. Nasubiri natumaini pamoja na wengine haya mambo yawekwe sawa.

La zaidi tafadhali utuambie hatima ya utetezi wako Bungeni kuhusu Waziri Mkuu kulidanganya Bunge. TUNAHITAJI MAJIBU.
 
Labda naomba tu mnielimishe CCM ina wapiga kura wangapi na CHADEMA inawapiga kura wangapi? naomba jibu ili nifanye mahesabu yangu ya kumuunga mkono Lema kumpinga.

hili swali huwezi kujibiwa na limeulizwa several times
 
Huyu Lema hana mapenzi mema kwa wananchi wa AR town, kwani wakubwa zake akina Mbowe walishafikia muafaka sasa yeye anaturudisha nyuma. Wana CDM mpelekeni Lema Milembe akapafanyiwe uchunguzi wa AKILI. Kila siku yeye analeta shari!

Kwanza jipeleke wenyewe Mirembe. CDM wakubwa ni wanachama jibuni hoja za Lema ni hoja za sisi wana Arusha.
 
Ni nani walifikia muafaka mpaka yeye akakataa? Ni CCM lakini imekula kwao. Kama siku zote wanafanikiwa kwa wapuuzi wenzao hapo sasa watuambie wenyewe CCM, huu mwafaka umefikiwaje yaani waliohusika na mchakato ni akina nani? Na hatima ya masuala ya kesi bandia, mauaji ya raia na udhalilishaji yako vipi kwenye muafaka? CCM is awful

I voted for you Lema na hayo uliyoyasema ndiyo matarajio yangu kwa Mbunge wangu. Nasubiri natumaini pamoja na wengine haya mambo yawekwe sawa.

La zaidi tafadhali utuambie hatima ya utetezi wako Bungeni kuhusu Waziri Mkuu kulidanganya Bunge. TUNAHITAJI MAJIBU.

kama mwafaka ni wa CCM ilikuwaje hao ma naibu meya na mwenyekiti kamati ya fedha kutoka CDM wakagombea na kuchaguliwa? Huoni kama kuna contradiction hapo?
 
1. Mada imeandikwa ki-mkorogo mno, haileweki kichwa wala miguu. Inabidi ujaribu kuunganisha unavyojua ili kupata picha.
Swali la kujiuliza, huyu Mhe Lema anajua wazi uwezo wake wa kuchambua na kuandika mambo ni sifuri. Lakini amekosa hata msaidizi mmoja wa kumwandikia kauli nzito kama hii? Kutokwenda shule si kosa, kosa ni pale unaposhindwa kuwatumia waliokwenda shule wakusaidie.

2. Huyu mbunge anafahamika siku zote kuwa ni mtu wa shari. Lakini kwa hili la kupingana na busara za wenzake walioona yafaa kumaliza mgogoro wa Arusha kwa amani na wakasifiwa kwa hilo.....linamfanya Lema awe ni mtu wa kuogopwa kuliko ukoma.

3. Watu wa Arusha hatukumchagua ili atuletee umwagaji damu na kutukosesha utulivu wa kufanya kazi za kutuletea maendeleo. Kwa kweli sasa tunajuta kumchagua kichaa atuongoze. Tumeisha......!
 
Huo muafaka walikubaliana na nani?,ni lini uchaguzi wa Meya uliitishwa na Chadema wakashinda unaibu Meya?Mimi ni mmoja wa waathirika wa maandamano yale(nilipigwa na kitako cha bunduki mwilini mwangu sema ujasiri nao ulinisaidia kuwatoka polisi maeneno ya round about ya mnara wa mwenge karibu kabisa na azimio la Arudha).Haya magazeti yaliotangaza kuwa muafaka umepatikana ni lini?Mimi Kama mwanachama wa Chadema na Watanzania wote wenye mapenzi na chama cha Chadema tunataka kupewa habari kwa uwazi bila kificho chochote.Nnamuomba Lema Kama alivyoonyesha msimamo wake hapa basi atujuze huo muafaka ulifikiwa lini na yeye je alishiriki au alipewa taarifa na maelekezo tu toka kwa mkubwa wake?.Nnawaomba viongozi wangu wa Chadema heshima mliyojijengea hasa misimamo na uvumilivu uliopo na imani ya wananchi juu ya chama hichi wasiiporomoshe kwa style hii.Pamoja sana Lema Mungu akubariki na Mungu akibariki Chadema na watu wote
 
kAULI ILIYOSIMAMA...HII inatoka mdomoni mwa Lema Live, haijaongezwa au kupunguzwa neno!
Kuna watu hapa ndani baada ya kusoma habari kuwa CDM wamekubaliana kuingia muafaka na ccm, walisema kuwa lazima Godbless Lema atatoa kAuli, na hakika ndiyo hii hapa!
Jamani, jamaa ameeleweka, hasa kwa hoja kuu kuwa ishu si kugawana vyeo!
Spport you pal, hali ni tata sana mjini hapa, there was no way!

Kwahiyo kulikuwa na shinikizo la mhe lema kutoa tamko kutokana na hapo kwenye bold nyekundu?
 
1. Mada imeandikwa ki-mkorogo mno, haileweki kichwa wala miguu. Inabidi ujaribu kuunganisha unavyojua ili kupata picha. Swali la kujiuliza, huyu Mhe Lema anajua wazi uwezo wake wa kuchambua na kuandika mambo ni sifuri. Lakini amekosa hata msaidizi mmoja wa kumwandikia kauli nzito kama hii? Kutokwenda shule si kosa, kosa ni pale unaposhindwa kuwatumia waliokwenda shule wakusaidie.2. Huyu mbunge anafahamika siku zote kuwa ni mtu wa shari. Lakini kwa hili la kupingana na busara za wenzake walioona yafaa kumaliza mgogoro wa Arusha kwa amani na wakasifiwa kwa hilo.....linamfanya Lema awe ni mtu wa kuogopwa kuliko ukoma.3. Watu wa Arusha hatukumchagua ili atuletee umwagaji damu na kutukosesha utulivu wa kufanya kazi za kuteletea maendeleo. Kwa kweli sasa tunajuta kumchagua kichaa atuongoze. Tumeisha......!
Wewe ndio utakuwa kichaa namba1,rudia kusoma ulichoandika
 
kama mwafaka ni wa CCM ilikuwaje hao ma naibu meya na mwenyekiti kamati ya fedha kutoka CDM wakagombea na kuchaguliwa? Huoni kama kuna contradiction hapo?

Dhambi ile ile inaendelea, kukiuka taratibu. Muulize Lema yeye ni mjumbe na mpiga kura kwenye uchaguzi kama huo inavyoelekea hakupiga kura na sidhani Mary Chitanda alikuwepo kama alikuwepo ni ajabu kwa sababu kura za naibu meya zilizopigwa ni nyingi hiyo moja iliyopinga sidhani ni ya Chitanda.

Any way issue raised na Lema zinahitaji kutolewa maelezo. Kimsingi CCM ni wazoefu wa huu mchezo na hapa wanataka kuanzisha ugomvi ndani ya CDM kwa maslahi wanayoyatafuta. Kwa misingi huo mwenye muafaka huu ajitokeze aseme kilichotokea na kinachoendelea.
 
Hivi CDM kila mtu ni msemaje? Ngoja tuone kati ya Mbowe na Lema na zaidi

Kwani mtu akiwa mvuta bangi ndio kunamuondolea akili za bangi? hujui kama kuna mwingine amesema hataki Fiesta Mbeya? kama hii barua yake kweli huyu siwezi kumtofautisha na wahuni wengine.
Mimi sio mfuata upepo, nimepewa akili na mungu ili nizitumie. muhuni wa namna hii hawezi kunishawishi kumuunga mkono.
 
Niwaulize makada ya CDM, hayo makubaliano y kugawanya vyeo hayakupelekwa kwenye vikao vya chama kabla ya kuidhinishwa? Kama ni ndiyo Mh. Godbless anaruhusiwa kuhoji maamuzi ya chama nje ya vikao vya chama?
 
Lema nina hakika kuwa upo sahihi kwenye hili. CHADEMA msijidanganye kuwa mtu mmoja au wawili wanaweza kukaa chini kwa niaba ya wananchi wanaowaunga mkono na kutoa maamuzi kama yaliyofikiwa Arusha.

Kama ni Umeya achaneni nao simamieni haki, CCM walikuwa wameisha wa-fix kwenye hili it was a matter of time tu wangeanza kuli-spin na kumomonyoa support ya wananchi juu yenu. Kama nilivyosema hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...umeya-wa-arusha-wapatikana-6.html#post2127305 CHADEMA wajue kuwa wananchi wa Arusha na maeneo mengi Tanzania hawataki muafaka na CCM, kwani waliisha wakataa kwenye sanduku la kura japo hawasikilizwi matakwa yao kwa CCM kutumia dola kunng'ang'ania kuwatawala. Wananchi wanataka kuondokana na CCM, any deal which led to the continuation of CCM will only serve well to the CCM. Huwezi kuvunja sheria mpaka kufikia kupotezea watu uhai wao halafu, mwisho wa siku unakuja kulazimisha mazungumzo na muafaka wa kupeana ulaji, Jifunzeni kutoka CUF, wamejikaanga kwa mafuta yao. This was a big victory to CCM towards dismantling CDM.

Waachieni Umeya wao, hakikisheni mnasimamia utaratibu kufuatwa na kuhakikisha wauaji wana-face the legal action. Huwezi kutengeneza documentary, inayosikika afisa wa polisi akisema "Aje Killer mara moja aje killer", halafu ipite hivi hivi. Ni bora mgogoro uendelee mpaka 2015 kuliko ku-BOW kwa kupewa unaibu meya. Hongera Lema ninataka na Mbowe naye aliyekaa na counterparty wake Pinda atoe kauli kama hii bungeni. Kuwa hakuna muafaka uliofikiwa au utaofikiwa bila a, b ,c niliyotaja hapo juu. Otherwise this is the beginning of the end of the strong support for Chamema nationalwise and particularly in Arusha. Wananchi wana imani na ninyi, wakikata tamaa wataacha kuja kwenye maandamano yenu.

Naunga mkono hoja mia kwa mia kama wanavyosema mjengoni!!

Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kufikia muafaka wa kugawana madaraka bila kujua hatma ya waliouwawa na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wauaji.

Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuhalalisha kugawana madaraka kwa kisingizio cha maendeleo ya watu wa arusha bila kuzingatia madai ya msingi ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi wa meya wa arusha.

Kama bajeti ya maendeleo imepangwa na kuanza kufanyiwa kazi pasipo ushiriki ama uwepo wa madiwani wa chadema basi kulikuwa hakuna sababu yoyote ya chadema kugawana madaraka kwa kisingizio cha maendeleo. Maendeleo yatapatikanaje kama hakuna haki, usawa na utawala wa sheria?? Maendeleo yatatoka wapi ikiwa kiongozi aliyepo hana uhalali wa wapiga kura??

Katika hili, namuunga mkono Mh. Lema, ni muhimu kuzingatia msingi mkuu wa madai ya chadema kwamba ni sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, kama ni vyeo basi wangesema mapema.
 
Lema amekuwa akishuhudia jinsi Mhe Zito, Chairman Mbowe wanavyotoa press releases kuhusiana na mambo mbalimbali.
Ameona huu ni wakati muafaka na yeye aonekane kuwa yupo, anaweza kutoa tamko...ndo maana amemwaga hayo maji-taka hapo.
CHEAP UNETHICAL POPULARITY.
Shame on you Lema. You are a disgrace to Arusha people.
 
Watu wa Arusha hatukumchagua ili atuletee umwagaji damu na kutukosesha utulivu wa kufanya kazi za kuteletea maendeleo. Kwa kweli sasa tunajuta kumchagua kichaa atuongoze. Tumeisha......!

Watu wa Arusha hatuko wapuuzi kiasi chako usituwekee maneno mdomoni. Na kama uko Arusha jichunguze, maana nyinyi ndiyo maadui wa Arusha.
 
Lema amekuwa akishuhudia jinsi Mhe Zito, Chairman Mbowe wanavyotoa press releases kuhusiana na mambo mbalimbali.
Ameona huu ni wakati muafaka na yeye aonekane kuwa yupo, anaweza kutoa tamko...ndo maana amemwaga hayo maji-taka hapo.
CHEAP UNETHICAL POPULARITY.
Shame on you Lema. You are a disgrace to Arusha people.

Mbona kinakuuma au ulihusika na muafaka. Sisi wengine tulitaka Mbunge wetu atueleze kinachoendelea. Jibuni basi mlifikiaje huu upuuzi
 
Back
Top Bottom