Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Hapa hakuna mpango! kuna watu wamefanya blunder ya mwaka and they don't want to own up. Binafsi, kama kulikuwa na maridhiano kati ya madiwani wa Chadema na wale wa CCM pale Arusha, na wakakubaliana na wakapigiana kura, without coercion or threats kwa manufaa ya manispaa yao. That settles it. Chadema Taifa wanatakiwa kutambua na kuheshimu makubaliano hayo. Vinginevyo, ioneshwe kuwa Chadema taifa ilitoa agizo au maelekezo (kwa maandishi) kwa madiwani wake kutoshirikia majadiliano yoyote ya muafaka bila kutoa taarifa HQ. Hiyo ndio itakuwa sababu pekee ya Taifa kutotambua muafaka huo.

Tulio kataa tangia asubuhi yale makubaliano tuliona mbali sana.
 
Umekosea KIMSINGI. Tatizo lilikuwa la kitaifa, sio la CDM Arusha. Waliokamatwa na waliouawa sio wa CDM Arusha tu. Swala la haki katika uchaguzi ni la kitaifa. CDM Arusha hawakuwa na uhalali wa kuanza mazungumzo ya maridhiano bila RUHUSA toka CDM Taifa.

Maridhiano BATILI hayatakiwi kutambuliwa na kuheshimiwa na CDM Taifa kama unavyosema












Maridhiano BATILI hayatakiwi kutambuliwa na kuheshimiwa na CDM Taifa kama unavyosema


Suala hapa si viongozi wa Chadema kitaifa kupigwa au kufungwa wala mgogoro sio maandamano na matokeo yake. Maandamano na matokeo yake yalitokana na mgogoro kati ya madiwani wa CCM na CHADEMA wa Manspaa ya Arusha. Viongozi wa Chadema kitaifa hawakujitokeza katika maandamano kutaka mmoja kati yao achaguliwe kuwa Meya wa Manspaa ya Arusha bali walikuwa wanawaunga mkono madiwani wa Arusha kama wananch wengine hata wasio Chadema wangeweza kuwaunga mkono. Kuwaunga mkono hata hivyo hakumfanyi Mbowe Mbunge na Diwani wa Mji wa Hai kuwa Diwani wa Arusha mjini. Matokeo ya maandamano ya Arusha na kukamatwa kwa viongozi wa Chadema kulileteleza kifunguliwa kwa kesi ya jinai kati ya si Chadema na CCM bali Mbowe na wenzake binafsi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa hali hiyo bado naungana na Mwanakijiji kwamba mgogoro wa Arusha ni wa Arusha na wala si Tanzania nzima. Ndio maana hata kabla ya maridhiano ya Arusha madiwani wa CCM na Chadema Kinondoni, Kigoma na Hai kwa mfano walikuwa bado wanashirikiana kama vile hamna mgogoro Arusha





[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom