Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Huo muafaka walikubaliana na nani?,ni lini uchaguzi wa Meya uliitishwa na Chadema wakashinda unaibu Meya?Mimi ni mmoja wa waathirika wa maandamano yale(nilipigwa na kitako cha bunduki mwilini mwangu sema ujasiri nao ulinisaidia kuwatoka polisi maeneno ya round about ya mnara wa mwenge karibu kabisa na azimio la Arudha).Haya magazeti yaliotangaza kuwa muafaka umepatikana ni lini?Mimi Kama mwanachama wa Chadema na Watanzania wote wenye mapenzi na chama cha Chadema tunataka kupewa habari kwa uwazi bila kificho chochote.Nnamuomba Lema Kama alivyoonyesha msimamo wake hapa basi atujuze huo muafaka ulifikiwa lini na yeye je alishiriki au alipewa taarifa na maelekezo tu toka kwa mkubwa wake?.Nnawaomba viongozi wangu wa Chadema heshima mliyojijengea hasa misimamo na uvumilivu uliopo na imani ya wananchi juu ya chama hichi wasiiporomoshe kwa style hii.Pamoja sana Lema Mungu akubariki na Mungu akibariki Chadema na watu wote
Mkuu, maandamano ya CDM Arusha wote tumeyaona Askari walipopiga mabomu ya machozi na risasi hewani watu wote walisambaa kwa kasi ya ajabu vitu vilivyobakia barabarani ni yebo yebo na kandambili mkuu, labda Mama Slaa ndio anaweza kusema sababu alipigwa wewe kaka sikukuona au wewe ndio ulikuwa unaendesha ile gari iliyovunjwa vioo na polisi
 
Namshauri ajitoe cdm aanzishe chama chake cha fujo atapata wafuasi wengi espicial humu jf
 
Niwaulize makada ya CDM, hayo makubaliano y kugawanya vyeo hayakupelekwa kwenye vikao vya chama kabla ya kuidhinishwa? Kama ni ndiyo Mh. Godbless anaruhusiwa kuhoji maamuzi ya chama nje ya vikao vya chama?

Huyu jamaa ni mtata sana na sio kuwa hayakuidhinishwa na chama yeye ni muumbe pia kwenye baraza la madiwani anajua mwanzo mwisho ila nimelipotezea tamko lake kwani limechukua muda mrefu sana alipima wananchi watachukuliaje ile hadaa yao ya kusema uchaguzi haukuwa wa haki na huru wakati wao wenyewe walifanya hivyo hivyo kule hai.
 
Sokomoko,

Sio wanaJF wote wanaopenda vurugu........Wengi ni Analysts and Great thinkers.Tuyadumishe haya,mapambano tuliyo nayo ni ya Fikra,na hayo ndiyo mapinduzi ya Kweli katika Karne hii.Tuatakapofikia kikomo cha hayo basi hayo uliyosema hufuata na mara nyingi huanzishwa na watawala.
 
Watu wa Arusha hatuko wapuuzi kiasi chako usituwekee maneno mdomoni. Na kama uko Arusha jichunguze, maana nyinyi ndiyo maadui wa Arusha.

Mkuu usifuate mkumbo, katika kauli nitakazomkumbuka JK maisha yangu yote ni ile ya mbayuwayu yaani changanya na zako. simuungi mkono hata chembe Lema kwenye hili. mimi sio mpumbavu.
 
Demokrasia inapovamiwa,ni hatari kabisa kuliko kuishi bila demokrasia.
Ni heri uwe moto au baridi kuliko vuguvugu maana nitakutapika, haya ni maneno ya mungu kwa mujibu wa biblia, sasa na wewe wacha mafumbo weka msimamo wako clear kama unaunga mkono Lema au lah!
Kijana inatakiwa chumvi uite chumvi na sio mkubwa wa jiko.
 
Mkuu, maandamano ya CDM Arusha wote tumeyaona Askari walipopiga mabomu ya machozi na risasi hewani watu wote walisambaa kwa kasi ya ajabu vitu vilivyobakia barabarani ni yebo yebo na kandambili mkuu, labda Mama Slaa ndio anaweza kusema sababu alipigwa wewe kaka sikukuona au wewe ndio ulikuwa unaendesha ile gari iliyovunjwa vioo na polisi
Acha ushabiki kwenye mambo ya msingi yaliogharimu maisha ya watu,wewe hauna tofauti na Pinda kuletewa habari wakati hali halisi hauifahamu na ni vizuri pia usitetee kitu usichokifahamu.Risasi zilipigwa hewani inamaana hao waliofariki waliuwawa na nani?au kwa kitu gani?Acha ushabiki pls kuwa makini sn sbb ipo siku utashabikia kifo cha baba yako
 
Mkuu usifuate mkumbo, katika kauli nitakazomkumbuka JK maisha yangu yote ni ile ya mbayuwayu yaani changanya na zako. simuungi mkono hata chembe Lema kwenye hili. mimi sio mpumbavu.


Sawa lakini heshimu maoni yangu pia kwa sababu nina uhakika Mh. Lema anayasema yaliyo ndani ya mioyoni mwetu minus wewe. Kisome alichoandika Lema, huwezi kuwa na muafaka wa kugawana vyeo. Muafaka ni kitu kipana chenye lengo la kusahihisha yaliyojitokeza Liipi lililosahihishwa kati ya aliyosema Lema? Narudia una haki ya maamuzi yako, lakini uwe mvumilivu kwa mawazo yetu pia.
 
Arusha mayoral seat controversy resolved

A long stading dispute between CCM and the opposition parties of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) and Tanzania Labour Party (TLP) over Arusha’s mayoral seat has been resolved.
His worship Gaudance Lyimo of CCM has now been recognized by the opposition parties as the bona fide mayor of the city following a meeting on June 20 which resolved the matter and also elected Mr. Estomih Mallah Deputy Mayor for a period of four years until 2014. The TLP councilor will be deputy mayor of Arusha for 2015 only.
Speaking in the full council meeting, the Chairman of the mediation session , Mr. Michael Kivuyo, who is also Councillor of Sokon One Ward, said that they had been brainstorming about the matter for four months and they have realized the wisdom of resolving the conflict in order concentrate in serving the people.

SOURCE: ARUSHA TIMES
 
Acha ushabiki kwenye mambo ya msingi yaliogharimu maisha ya watu,wewe hauna tofauti na Pinda kuletewa habari wakati hali halisi hauifahamu na ni vizuri pia usitetee kitu usichokifahamu.Risasi zilipigwa hewani inamaana hao waliofariki waliuwawa na nani?au kwa kitu gani?Acha ushabiki pls kuwa makini sn sbb ipo siku utashabikia kifo cha baba yako
Lema ndio analeta ushabiki, tunataka mbunge wa kuleta maendeleo jimboni kwake na sio mshereheshaji (mc )
 
Atapata pia machalii na vibaka wa Arusha, hao ndio watu wake wa karibu.

Nampongeza Lema. Hao unaowaita machalii na vibaka hawakuzaliwa hivyo, nina hakika hata wewe kama usingepatiwa nafasi ya upendeleo na god father wako ungekuwa kwenye group la vibaka. Vibaka ni matokeo ya wananchi kutokuwa na ajira halali za kuwaingizia kipato. Huwezi kumaliza tatizo la vibaka kwa kuajiri polisi wengi bali ni kukuza uchumi unaweza kuzalisha ajira za kutosha miongoni mwa wananchi. Katika mambo ambayo serikali ya Tanzania imekuwa ikiyapuuzia ni suala la ongezeko la vijana wasio na ajira nchini. Hakuna Taifa linalokuwa na amani ya kweli na kudumu kama sehemu kubwa ya raia wake hawawezi kuyamudu maisha yao kwa ukosefu wa ajira. Ningekuwa mimi ni wewe ambaye anatetea serikali mpaka povu linamtoka kwa kuwa amepachika kimrija chake kwenye buyu kuu, ningekosa amani kuwaona vijana wengi wanaishia kuwa vibaka.

Hawa vibaka ndiyo mtaji mkubwa wa kisiasa kama atatokea mtu wa kuwashawishi kuwa akiingia madarakani atawatengezea mazingira ya kujipatia riziki zao kihalali kwa kukuza uchumi from tha bottom up, siyo huu wa sasa tunaoambiwa unakuwa ambao unaishia katika level ya kina kishongo na washirika wake kujilimbikizia posho mpaka za kuumwa mafua.
 
Safi sana LEMA wewe ni kamanda wa kweli,haki ni lazima isimame,viongozi wa kiafrika wamezoea kugawana madaraka pindi wanapopindisha sheria,LEMA wewe ni shujaa wa ukweli,hakika msemo wako wa no bora kufa nikiwa nimesimama nikitete haki,kuliko kufa nimekaa haki yangu ikipotea.BIG UP LEMA.We love you,we trust you.
 
Sawa lakini heshimu maoni yangu pia kwa sababu nina uhakika Mh. Lema anayasema yaliyo mioyoni ndani ya mwetu minus wewe. Kisome alichoandika Lema, huwezi kuwa na muafaka wa kugawana vyeo. Muafaka ni kitu kipana chenye lengo la kusahihisha yaliyojitokeza Liipi lililosahihishwa kati ya aliyosema Lema. Narudi una haki ya maamuzi yako uwe mvumilivu kwa mawazo yetu pia.

Waliomchagua Lema bado wanamuunga mkono, sasa utashangaa mtu yuko mwanjelwa na wala hakumpigia kura na bahati mbaya sana hayuko arusha na hajui hali iliyoko huko lakini anataka kujivika joho la kuwa msemaji wa watu wa arusha.

Katika mambo yote watakayokubalina katika muafaka, kugawana vyeo haiwezi kuwa ndio sukuhuhisho la uvunjwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi. Na hakuna maana yoyote ya muafaka kama muafakja hauzungumzii wauaji kuchukuliwa hatua za kisheria!!
 
Ni heri uwe moto au baridi kuliko vuguvugu maana nitakutapika, haya ni maneno ya mungu kwa mujibu wa biblia, sasa na wewe wacha mafumbo weka msimamo wako clear kama unaunga mkono Lema au lah!
Kijana inatakiwa chumvi uite chumvi na sio mkubwa wa jiko.

Matola,

Haitakaa itokee,siwezi kumuunga mtu mkono kwa sababu nitakuwa shabiki,au kipofu.Ukitaka kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa Objective utaona umuhimu wa kuunga mkono hoja na si mtu. Kwanza kabisa Hoja yoyote inayosaliti waliomwaga Damu kwa ajili ya haki,makosa ya kikanuni na hila za kisheria na kimamlaka SIWEZI KUIUNGA MKONO KAMWE,Tafakari.

Kuhusu suala la Arusha,Naamini utata uliopo utajadiliwa ndani ya Chama.Kuna wanaoniandikia Inbox tangu juzi.Hili suala ni lazima maamuzi yafanyike kwa kuzingatia uzito wa Damu za watu zilizomwagika,naamini kama ni fursa ya muafaka ilikuwapo hata kabla ya tarehe 5 January,2011...sasa sijui kama CCM waliona busara baada ya kuona Damu ama ni kipi kipya! Ni lazima mazingira yoyote ya muafaka yazingatie conditions zilizolazimisha maandamano ya January 5, Maslahi ya umma kikanuni,kisheria na haki kwa Ujumla ili tuwe na moral Authority ya kutumia nguvu ya umma katika harakati ,so nje ya hapo ni mjadala mwingine na mpana zaidi.Naomba niishie hapo kwa sasa,ilka natoa Rai kwa WanaJF,Wanamapinduzi wa kweli hawafuati mkumbo,tuwe analytical na nahimiza umuhimu wa kuwa na mijadala mikali mikali ili tuwe na solutions ambazo ni practicals.WanaJF ni wachambuzi mmenielewa
 
Mh! Kambale wako wengi CHADEMA. Kila mtu ana sharubu chama kile. Tamko hili lilipaswa kutolewa na Mwenyekiti Mbowe au KM Dr Slaa. Vinginevyo tutafute definition sahihi ya DEMOCRACY, UWAJIBIKAJI WA PAMOJA, UTAWALA wa SHERIA na mambo kama hayo.
 
nilikuwa naangali ile documentary ya arusha hapa....kweli ningeshangaa sana kuona lema analowanisha msomamo ghafla namna hii.....
Baada ya ile tarifa ya mwafaka na majibu marahisi kutoka kwa madiwani wa CDM....na ukizingatia ukweli ambao kwangu mimi si wakuadisiwa bali wa kushuhudia kuanzia sekeseke la uchaguzi wa meya, maandamano + mkutano na kufanikiwa kupata CD zote za maziko ya tarehe 12-01-2011...ilikuwa haingii akili kuingia makubaliano kirahi namna hii...
 
Huyu Lema hana mapenzi mema kwa wananchi wa AR town, kwani wakubwa zake akina Mbowe walishafikia muafaka sasa yeye anaturudisha nyuma. Wana CDM mpelekeni Lema Milembe akapafanyiwe uchunguzi wa AKILI. Kila siku yeye analeta shari!
Wala hahitaji kupimwa akili. MALEZI ya baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ndilo tatizo. Kuna watu mle ni maarufu na mashuhuri kuliko chama chenyewe! Hili nalo lisipotazamwa vizuri litakigharimu sana CHADEMA. Dr Slaa kuwa mkali kidogo kama ulivyofanya kwa Kafulila.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom