LEMA anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa faida ya nani?!

Status
Not open for further replies.
Mkuu mbona jibu liko wazi kabisa kuwa ni Spika wa Bunge Bibi Kiroboto na Naibu wake Job Ndugai, pamoja na Uongozi mzima wa jeshi la polisi chini ya amri mbofu mbofu za Babe Mwanaisha ndio zinazompa umaarufu Lema na chama chake cha CHADEMA. Kwa maneno mengine ni kuwa kila umaarufu wa Lema au CHADEMA ukishuka kidogo basi watajwa lazima watakurupuka na waupaishe mpaka wanachi sasa tume ukinai huo umaarufu wa Lema na Chadema yake.

Hata Lema akitoka jela kesho utaona kama si Spika au Naibu wake au jeshi la polisi mmoja wapo kati ya hao watatu lazima wataupaisha tena umaarufu wa Lema na CHADEMA...kama huniamini stay tune!
 
Sasa wewe kweli hata hufai kuitwa fyatu ! Yaani kafukuzwa bungeni wewe unaona bora angekaa tu Dodoma, akawa anavinjari na malaya wa rwanda na burundi kama hao mawaziri wenu ambao licha ya kutofukuzwa bado wanatoroka bungeni na wakijua wamechukua posho, na wana wajibu wa kujibu hoja zinazohusu wizara zao ?? Wewe kweli unajiona una akili timamu au ni kama za yule Lusinde ??

Wewe mlikutana na Lema wapi akakueleza ana hamu ya kutolewa nje ?? Na ugomvi unaomuhusu ni upi, na usiomuhusu ni upi ? We all know kuwa anawanyima usingizi na kila fitna mnazojaribu kufanya anawapiga chini... !! Kwako wewe, mjenga hoja ni yule wa Kigoma aliyesema fu.. au yule cha pombe, omba omba Mkamia aliyeitwa wenzake mbwa. Kwako na akili zilizojaa masaburini unajifanya unajua mipango yake ya chuo.....??? WTF yeye ni mbunge wa arusha, chuo kipo hapo na hao ni wapiga kura wake, sasa wewe ulitegemea WAMA, Ze Komedi au TOT plus ndiyo waje wa kwanza chuoni kwa sababu mwanachuo kauawa ?? Una akili za kokroch km yule aliyekwenda na kudai ...mmeitaka sirikali, haya sirikali hii hapa ila kichwa imejaa konyagi haiwezi kuongea bila kipwazwa sauti.... !!! Hayo ndo mafunzo ya kukaa semina week 6, na ndiyo sera mpya kutoka Malaysia za jinsi ya kuongea na wananchi !!! Jamani tafuteni kazi za maana, za kutumia akili na kupata hela halali hizi za kusokomezewa ----- na kuandika ukijua ni ----- lakini basi tuu sababu ya tubuku kidogo mnajiaribu ubongo bila kujua !!

Alipombana huyo mzee wa kulia lia bungeni kuwa alisema urongo, si alifukuzwa na akaambiwa alete ushahidi. Akauleta sasa mbona issue ilipotezewa. Sasa leo nani atashangaa kusikia hamtaki awepo bungeni, na atoe nondo nani hasa kinara wa udini..!!

ha ha ha awe kama Zitto ehhh, that actually speaks volumes of what type of bots are behind all these...!! Kwa hiyo nyie mnajua kuwa ZK ni powa ehh... senkyu vere machi kwa kutoa jibu tena ktk sentensi ya mwisho kabisa !!

Ila simu yake hamuipati ng'o na hamtaweza kufuta zile sms zenu ambazo mnajua zitawarudi milele !!

Kafukuzwa bungeni kwa siku tano lakini hakufukuzwa Dodoma, Na kama una akili timamu Lema tangu mapema alikuwa anatafuta kutolewa nje..Aliongea anachoongea bila kujenga hoja yoyote ya maana lakini Naibu spika akampotezea..baadae ndio akajiingiza kwenye ugomvi usiomuhusu. Kwa wenye akili Lema huwa hana hamu ya kukaa bungeni, Ameshapewa jukumu la kuhakikisha wanavyuo hawakai salama na ndio anachotamani kutekeleza muda wote..Yalipotokea ya Arusha kaja fasta kana kwamba alikuwa anasali yatokee saa ngapi..No wonder huwa inafikiriwa mengine huwa mnapanga yatokee mpate kwa kuanzia...Eti alikuwa anawatuliza ni lema au mwingine..Kwa akili ipi ya kutuliza watu....AJIFUNZE KWA ZITO kama kweli anataka kuwa mwanasiasa...Unless ana mambo yake anayotafuta kama wengi tunavyoendelea kuthibitisha...
 
upo sawa mkuu unajua watu hawapendi kuambiwa ukweli mimi sijaona kitu ambacho lema amekifanya toka amekuwa mbunge zaidi ya maandamano, vurugu na shida tu ndani ya A town hili ni jiji la kitalii bwana wala usiongee sana nani asiyemjua kuwa alikuwa mpiga debe ndiyo shida yenye mkuu achana nao waeleze ukweli siku zote unauma mtu wangu
 
Mkuu kwangu mimi sijaangalia kushikiliwa kwake kwa jana tu,nimejaribu kuangalia yaliyotokea kuanzia nyuma hadi jana,na umaarufu ambao tayari alikuwa no,ilikuwa ni wakati wa yeye kukaa chini na kutengeneza siasa zile za ushawishi na kuepukana na matatizo kama haya yanayomkumba,huku ni kumpotezea muda Mkuu,huu muda angeliutumia kutengeneza ujasiri kwa vijana wengine kwa sababu tayari yeye ameonyesha na karuka viunzi vingi.ka hiyo vijana wangejifunza kwake kwa sababu amepambana na tembo kwa mikono na kumshinda.
Mbona hueleweki? Mara aache vurugu, mara afunze vijana ujasiri. Hakika hujui unenalo na uandikalo.
 
lema ni maarufu kitambo tu na hana haja ya kupata umaarufu ili hali anajua yeye ni maarufu, anachokifanya ni kutetea haki kwa kueleza ukweli pale panapostahili!!! CDM 4ever!!!
 
Lema anahatarisha Amani lakini amepata dhamana ponda kesi ya ardhi dhamana imefungwa nchi inaubaguzi Wa waziwazi
 
Wabunge wooooote wa CCM pamoja na Mawaziri wake bila kumsahau Spika na Naibu wake wote hao WANATAFUTA UMAARUFU KWA KUBEZA KAULI ZA VYAMA VYA UPINZANI. Utakuta Mbunge anainuka na kusema "...Bajeti hii naiunga mkono asili mia 100 lakini kwa niaba ya wananchi wangu napenda kuiomba serikali ifanye hivi na vile kwani haijawatendea haki wapiga kura wangu...." Be staright call a spoon a spoon and a spade a spade not a big spoon.
 
Tangu uchaguzi mkuu wa 2010 umalizikie na Lema kupewa ubunge wa Arusha, mji huo haujajua neno amani. Kila kukicha kuna jambo na viashiria vya kuhatarisha aman, na mbunge huyo ameshaenda mahakamani na gerezani mara kadhaa pendingine kuliko mbunge ye yote katika historia ya Arusha au Tanganyika. Sitashangaa kama hili la kulipua makanisa atakuwa hahusiki...Brother Lema huoni sasa utatuletea machafuko?:angry:
 
Lema huyo huyo kasababisha mtafaruku katika Baraza la Madiwani Arusha, Madiwani wa Arusha wakatimuliwa Chadema, Kahamasihsa Maandamano na kuteta kizaa zaa, Mara kahamasisha vurugu za wanafunzi, mara apelkwa mahakamini na gerezani, mara kulipua kanisa...huyu mtu yupo sawa kweli?:twitch:
 
upo sawa mkuu unajua watu hawapendi kuambiwa ukweli mimi sijaona kitu ambacho lema amekifanya toka amekuwa mbunge zaidi ya maandamano, vurugu na shida tu ndani ya A town hili ni jiji la kitalii bwana wala usiongee sana nani asiyemjua kuwa alikuwa mpiga debe ndiyo shida yenye mkuu achana nao waeleze ukweli siku zote unauma mtu wangu

Basi ni mpiga debe mwenye skills zilizotukuka kama anaweza kucommand respect na kushawishi kula zaidi ya 58 elfu kiasi hicho kwa wana A town haihataji wewe uone amefanya nini
 
Tangu uchaguzi mkuu wa 2010 umalizikie na Lema kupewa ubunge wa Arusha, mji huo haujajua neno amani. Kila kukicha kuna jambo na viashiria vya kuhatarisha aman, na mbunge huyo ameshaenda mahakamani na gerezani mara kadhaa pendingine kuliko mbunge ye yote katika historia ya Arusha au Tanganyika. Sitashangaa kama hili la kulipua makanisa atakuwa hahusiki...Brother Lema huoni sasa utatuletea machafuko?:angry:

basi mkuu wa mkoa,RPC,OCD,RCO,Regional inteligence officer wote wafukuzwa kazi hawana wafanyaalo kulinda usalama wa Arusha
 
Basi ni mpiga debe mwenye skills zilizotukuka kama anaweza kucommand respect na kushawishi kula zaidi ya 58 elfu kiasi hicho kwa wana A town haihataji wewe uone amefanya nini

Respect? what respect...do you call absurdity (illogicality) to be a respect? you must be joking. Anacommand akili za watu wenye fikra sawa na yeye, mtu mwenye busara zake hawezi hata siku moja kumfagilia mtu kama Lema
 
WEWE MLETA MADA 'NAONA UNAJITAHIDI KUTAFUTA UMAARUFU JF KWA KUPITIA LEMA' umeamua kujiunga na CHILISOSI au kila mtu anatafuta umaarufu KIVYAKE?
 
TAHADHALI IKIKUKWAZA ACHANA NAYO.

Wakuu habri ya Sikukuu?,natumaini hamjambo wote,kwa wale wagonjwa poleni mungu atawasaidia mtapona. Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia siasa za Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema,na kujiuliza maswali mengi mengine nimejkuwa sipati majibu hata kidogo.

Tafadhalini naomba tujadili hili kwa uungwana mkubwa ili tusije tukaondoa maana halisi ya maudhui yangu,Tangu kuingia kwake madarakani Arusha hakujatulia,kila siku ni migogoro na vurugu ambazo mwisho wake ni lazima mtu apotee maisha!. Kwa wale wenye kumbukumbu sahihi mtakubaliana na mimi kwamba katika uongozi wake watu si chini ya wanne wamekwishapoteza maisha kutokana na vurugu,sitaki kuingia kwa undani juu ya hili lakini kwa wale wenye kumbukumbu nadhani mnalitambua.

Ni huyu huyu Lema ambaye amejikuta mara kadhaa akitolewa Bungeni kama si kukwazana na viongozi kadhaa ndani ya Bunge kutokana na maneno yake kadha wa kadha haijalishi iwe kweli ama si kweli,lakini yametokea!. Mara nyingi nimekuwa pia nikufuatilia kauli zake kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara,ukisikiliza kwa makini uangundua kwamba Lema ni Mtata,ni mtu ambaye anaonekana kukata tamaa ya maisha na sasa kujaribu kutumia njia za mkato ikiwemo jazba kutafuta ufumbuzi.

Nimemsikia mara nyingi sana akithibitisha kwamba hapndi kuonewa na pale anapobaini kwamba anataka ama ameonewa basi ni lazima asimame kidete kujitetea ama kutetea haki yake,hili ni jambo ni sahihi na namuunga mkono,lakini tunatofautiana katika kuidai hii haki,yeye anatumia nguvu kubwa zaidi. Kuna viongozi wengi sana ambao ukiwatizama wamefanya mambo makubwa na mazito katika kuhakikisha kwamba wanajitetea ama kuwatetea na wengine ama wale wanaowaongoza,lakini wamekuwa wakitumia hoja ambazo mwisho wa siku zinaleta mana halisi.

Kwa mfano yupo JOHN MNYIKA,ZITTO KABWE,DK.SLAA,HALIMA MDEE,na wengineo wengi wa leo,jana na juzi,lakini hatuawahi kusikia vurugu kwenye maeneo yao wala watu kuuawa,nilitegemea kwamba Baada ya Lema kurudi Bungeni na kwa sababu amekiangusha chama kikubwa kama CCM angetulia na kujaribu kuwaonyesha watanzania kwamba yeye ni mtu wa namna gani katika nchi hii,lakini matarajio yangu yamekuwa tofauti.

Ndiyo mana nashawishika kuamini kwamba pengine Lema anatafuta umaarufu kutokana na hivi vituko vyake vya kila siku!,lakini ni vituko ambavyo vinaanza sasa kumfanya adharaulike katika jamii,kwa sababu watu wanaanza kuzoea kwamba LEMA ni wa vurugu. Ombi langu kama Lema atatoka na kurejea tena mitaani,kuna haja ya viongozi wa CHADEMA kukutana nae na kujaribu kuzungumza nae,mbona wenzake wanakua na hoja na zinapenya na kupokelewa vizuri na jamii?!,kwa nini aisijifunze kwa wenzake.

Mwisho hakuna mtu anayependa kuonewa hapa Duniani,hata mtoto mdogo ambaye bado ananyonya akiona mama yake anamsumbua sana kwenye titi huwa anapiga ngumi ama kuficha na kupiga mateke kuashiria kwamba hapendezwi na yanayojitokeza.Narudia Lema akitoka salama Polisi na kurejea mitaani aachane na hizi vurugu akae na wananchi wake wafanya shughuli za maendeleo,naamini wameshaelewa madhumuni yake.

inawezekana wewe pamoja na wengine wa level yako hamjui level ya Lema. Lema is far ahead of many of us can think.
  1. Lema ni maarufu tayari long time
  2. kila mtu anamchango wake kwa jamii namna alivyojaliwa huwa hatufani hata siku moja ukuona watu wanafanya mambo kwa kufanana basi ujue mmojawao anacopy na kupaste (hatumii uwezo wake) kama wanavyofanya viongozi wa ccm.
  3. Nikiangalia hata hao unaowataja (Zitto , Mnyika nk ) pamoja na kuwapima kwa hoja zao lakini nao kimtazamo wala hawafanani.
  4. Wanamapinduzi huwa wako hivyo (hasa kwa watu wenye mtazamo wa wogowoga kama wakwako)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom