Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Kuna yeyote hapo nje atakayekua anayasoma na kutafakari maneno haya kwenye wino mwekundu?????????????????
Hapa unamuuliza nani hasa wewe?. Nani kakwambia mimi CHADEMA?, si wote wanaopinga udhalimu wa CCM ni CHADEMA au wapinzani.
Wapo CCM ndani ya chama wanapinga upuuzi huu wa kuchezea amani ya nchi na wapo wasiokuwa ma chama wanapinga upuuzi huu wa kuchezea amani ya nchi. Mwaka 1992 tuliporudisha mfumo wa vyama vingi, wakati Tanzania ilipokuwa na viongozi wanaofikiria wananchi zaidi ya matumbo yao na familia zao kama Mwl Nyerere walilisemea hili la kuambatanisha siasa na vyombo vya usalama.
Unapokuwa na watu waliokabidhiwa dhamana ya kulinda raia na mipaka ya nchi kwa mujibu wa katiba kuwa mashabiki wa siasa unajenga mazingira ya kulipua nchi, wananchi watakapokata tamaa na vyombo hivi.
Kwa kuwa leo hii nchi inashikiliwa na genge la watu waliojimbikizia mali kifisadi na wanahitaji kulindwa na mkono wa sheria, matokeo yake wanavunja katiba kwa masilahi binafsi. Hakuna haja ya CDM wala chama chochote cha upinzani kuwa na armed wing, Armed wing ni PUBLIC TRUST, siku wakisema wananchi NO tunataka kuongozwa na X badala ya CCM, maghala ya risasi yataisha na bado hawatarudi nyuma.
Hakuna kitu kibaya kama kupoteza public trust, na kwa hili serikali ya CCM imefanikiwa sana. Hakuna mtanzania leo hii anayeiamini mahakama, polisi, Usalama wa taifa, na hivi karibuni Shimbo alipeleka shombo hiyo JWTZ japo walimdhibiti na kuminimise damage. Huwezi jenga Public trust kwa oppression or aggression, wananchi hawapaswi kuwaogopa au kuwachukia Polisi, au TISS, Tume ya uchaguzi au mahakama, bali wanapaswa kuwaheshimu na kuwaamini.
Unapotumia vyombo hivi kisiasa kwa masilahi yako si tu vinakusaidia kubakia madarakani bali vinakufanya uongoze watu wasikuwa na imani nawe na kuvifanya vyombo vya dola kuonekana kandamizi badala ya saidizi kwa wananchi.