Lazima tuwekane sawa kuhusu UKIMWI

Swali: Je, kuna tofauti gani ya vionjo (ladha) wakati unafanya tendo la kujamiiana kwa kutumia kondomu Vs Unapofanya bila kutumia kondomu? Ipi inakuwa tamu, bila ya kondomu (kavukavu) au unapokuwa umevaa kondomu?

Jibu: Mimi kama domo kaya.... nasema mapenzi bila ya kondomu ndio matamu zaidi huwezi kula pipi kwenye nailoni lake.... na kondomu pia sio nzuri sana na wala siziamini sana cos zingine ni kavu zinachubua msuguano ukizidi mwanamke hupata michubuko....... Pili kondumu zingine zinanuka mfano mzuri ni salama kondomu, na pia salama kondomu zinamafuta ambayo baadhi ya watu huwa yanawasababishia muwasho sehemu za siri.

Ushauri: Mimi kama domo kaya ushauri wangu ni kwamba ili ufanye mapenzi mazuri na matamu bora uchague mmoja umpendae kwa dhati muuende mkapime na baada ya hapo fungeni ndoa ili mfanye mapenzi yenye amani na sio ngono ambazo mwisho wake huwa ni wasiwasi.... ukitoka kajipu kidogo tu unadhani sijui tayari nimekanyaga miwaya....

Hilo ndio jibu langu na ushauri wangu nasubili wenzangu nione mtajibu nini ili tujifunze.
 
Jibu: Mimi kama domo kaya.... nasema mapenzi bila ya kondomu ndio matamu zaidi huwezi kula pipi kwenye nailoni lake....

Domo Kaya,
Huo ndiyo ukweli ninaouamini kuwa ni ukweli! Shida ni kuwa tunalishwa kila aina ya uongo na Watu wa Magharibi ili wafanye biashara zao kupitia kwetu na ndiyo maana UKIMWI hautaisha hadi hapo.....

Ushauri: Mimi kama domo kaya ushauri wangu ni kwamba ili ufanye mapenzi mazuri na matamu bora uchague mmoja umpendae kwa dhati muuende mkapime na baada ya hapo fungeni ndoa ili mfanye mapenzi yenye amani na sio ngono ambazo mwisho wake huwa ni wasiwasi....

Tena hizo Ndomu zenyewe sina uhakika kama zimekuwa improved maana they were there even before UKIMWI! Twas meant for uzazi wa Mpango, zimegeuzwaje leo kuwa kinga ya UKIMWI?
 
Mi nadhani tuanze kukubali hali halisi ya mazingira yetu. Halafu ndio tujadili mbinu za kupambana na matatizo yetu, bila hilo hatuendi popote

Kwanza, UAMINIFU katika mahusiano si kasumba ya mtanzania wa kiume. Ingawaji na kinadada wa kisasa wajakuja kwa kasi sana katika kasumba hii.

Pili, kuwa na MPENZI ama MKE MMOJA ni nje ya tamaduni zetu. Jamii haishangai hata kidogo pale ambapo, mwanaume anapokuwa na mke na kimada, ama mpenzi na mshikaji. Ila itamshangaa na kumlaani pale mume huyo atakapojali kimada na kuacha familia yake na njaa

Tatu, PESA, MAFANIKIO, na MAENDELEO yanaruhusi kuwa na wanawake wengi.

Nne, WANAWAKE wamekubali kwa kiasi kikubwa sana mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja.

Tano, MARAFIKI wa MWANAUME, wamekubali kuwa shemeji kwa kila mwanamke anayeletwa mbele yao.

Sita, UKWELI kuhusu tabia za chumbani za Tanzania haziweki bayana. Kila mtu anajisifia kivyake tu. Mi nimepiga goli saba kumbe hata moja hakufanikiwa, sembuse asema ukweli kuhusu matumizi ya kondomu?
 
Yes to nationwide AIDS tests

Adam Lusekelo
Sunday News; Tuesday,June 12, 2007 @00:02

The prez, Jack Mrisho, talked to the press the other day. Among the things he said was a mandatory HIV/AIDS test for the whole nation. Poa sana!

I know there are some people who don't even know that the damn thing is killing a lot of our brothers and sisters. I know that there are Tanzanians out there who do not even know a thing called a condom. Leave alone the bullcrap about people dealing with the disease from Dar.

I think the prez has made a very sexy point. Let everyone have an AIDS test.

Now the prez was once a soldier. In fact he ended up being a colonel before he was lured to the joys of politics. He knows that good military leadership means being just that - a leader. When you have an objective you have to attack. When you attack you have to be the first to come out of the trench and go firing with everything you have got.

Then your men will come out attacking with you. Then they will respect you and you will win their undying loyalty. Watakulinda,. Our Jack says that there should be a nationwide check-out for AIDS thing. There should be a leadership thing, I think. Jack should order all his ministers to have an AIDSA test. Then we will come to the principal secretaries.

We want those results to be public. Then, of course, we go to Tanzania's unbuilt capital of Dodoma were our legislators should be subjected to AIDS tests. We want independent guys to be witnesses. I hear there are some guys who go to these medicals and bribe them to say that the guys who have undergone the tests are negative. They bribe even for that!

But if the prez says so and pays some medics handsomely he could have great results. Frankly I believe that all our civil servants should have mandatory AIDS tests. After that show of great leadership the rest of us honest citizen of the United Republic of Tanzania will queue to hospitals to test- for AIDS. But right now things are a bit sketchy. The parliamentarians don't think that they can encounter HIV/AIDS.

“I am a member of parliament, you know, how can I have AIDS?” asked an MP who was confronted by a prostitute, who wanted him to put on a condom. The MP was in an advanced stage of intoxication, But since his mind had shifted from his head to his gonads from the booze, he accepted the use of the condom. Praise to the woman for insisting.

Mbwene2@yahoo.com

Good points Adam we must start with the president himself with an independent agency.
 
Haya ya tamu na chungu jamani vipi tena?
Ebu nambieni na wale wanaopanda na kushuka mnazi!...inakuwaje?
Starehe yoyote ile ni ktk akili yako!.. hata sayansi yasema hivyo.
Ukizoea ugali bila chunvi utaiona tamu yake tofauti na uji wa sukari!. Muhimu zaidi shibe!

Nilikuwepo.......
 
hivi yuko unaeiona sukari chungu? au kali? nnaona hapa tunakubaliana sukari ntamu wajemeni
 
Ilikuwa siku ya jumatano usiku , mishale ya saa 6 hivi usiku , niko zangu sehemu na rafiki zangu kadhaa , ghafla nikapata simu natakiwa niangalie email zangu kuna ujumbe wa kujibu hapo hapo , nikaamua kutafuta internet café ya jirani na hapo .

Nikapata café moja , kwa taarifa yako kuna café mbazo zinafungwa milango lakini taa zinawaka ndani hapa kinondoni na baadhi ya maeneo ya ilala , kariakoo na mwananyamala , ukienda katika hizo café usiku huo utakutana na watu wa ajabu ajabu lakini wengi ni vijana wanafanya kazi zao

Nikapata sehemu ya kukaa , ilipofunguka hiyo computer nikakuta mtu aliyekaa kabla yangu ni mwanamke na alikuwa anachat katika chatmoja inaitwa darhotwire , jambo na darchat kwa mpigo , kufungua hizo chat nikakuta kumbe aliongea na kijana mwingine ambaye naye alikuwa yuko nyumbani kwao wakapeana namba yule kijana akamwambia atamfuata kinondoni .

Na hii ndio aina mpya ya maisha kwa baadhi ya watu haswa wale wanaouza miili yao anangoja muda wa usiku hata mchana anaenda internet café anajipachika jina nzuri anasema yuko nyumbani au anajiita mwanafunzi ametoroka shule wanaume wanajichanganya wanamtaka anawakubali wanamalizana juu kwa juu

Internet café hizi ziko nyingi kama nilivyosema , na hawa wasichana hawalipi karo ya kutumia internet wakati huo wanalipa kesho yake akishapewa posho na mtu ambaye amekubaliana nao wakati huo , ndio maana ukikutana na mwanadada katika mtandao akasema anajiuza uwe makini sana

Kuna wengine ni ukweli kabisa wanajiuza hiyo sio siri , na wengi wanajigeuza kujifanya yeye mwanafunzi wa chuo Fulani au sekondari Fulani ili kuwavuta watu zaidi na ili hata wewe ambaye unamchukuwa uwe a wasi wasi lakini usiweze kumiliki ufikiri ni mwanafunzi si unajua wanafunzi wako chini ya wazazi au walezi wao ?

Kwahiyo hata siku ukimkuta na mwanaume mwingine anaweza kusema kaka yake au mwanafunzi mwenzake wewe utafanya nini ? na ninajua vijana wengi siku hizi wako bize hawana muda wa kumfuatilia na kumjua mwanamke au mwanaume anayemtaka yeye anaingia tu kichwa kichwa mpaka mwishoni anakuja kushituka ameshaliwa .
Na vijana wengi wanaathirika sana na magonjwa haswa ukimwi kwa njia hii kwa sababu ya kukutana na watu waongo wanaotumia mitandao kujifucha ukweli wao , wazazi angalieni sana watoto wetu wanavyochat na kukutana na watu kadha wa kadha adhari zake na mambo mengine yanayotokea katika hii dunia ya sasa

Kuna umuhimu wa hizi internet café kupitiwa upya kuangaliwa mambo wanayoyafanya haswa nyakati za usiku , kama sio kufanya biashara hizi za kuuza wasichana wengine wanashikiri katika kudurufu miziki haswa ya nyumbani , nilishangaa siku moja nimeingia www.aresgalaxy.org na kukuta kuna top10 bongo flava za kitanzania mtu anazo katika computer yake hapo kinondoni na hana wasi wasi .

Wengine wanatumia mida hiyo kufanya mipango yao mengine ya kihalifu kama unavyojua , usiku huku miji mingi haswa marekani ni asubuhi au mchana kule wanaamka na wanafanya kazi ni rahisi zaidi kwa vijana kuingia net huku wakaanza kudanganyana na watu wa ulaya kupata ulaji na fadhila zingine .

La mwisho zaidi tembelea www.youtube.com tafuta mfano bongoflava utakuta miziki kibao ya vijana wetu mengine imewekewa hati miliki na kampuni ambazo mimi zijawahi kuzisikia hapo bongo kwa shuguli za utengenezaji wa video hata muziki lakini katika mtandao unazikuta

Ndio maendeleo hayo au sio ?
 
Tanzania kama mataifa mengine mengi duniani yametangaza vita isiyoisha ya Ugonjwa hatari wa ukimwi , moja ya kampeni kubwa kabisa ilizinduliwa na Mkapa kisha akaja kupewa nguvu zaidi na raisi wa zamani wa Marekani Bill Clinton Enzi hizo , Lakini leo hii Raisi Kikwete nae ametangaza vita dhadi ya ukimwi viwanja ya mnazi mmoja .

Amekuja na msemo wake TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA KAPIME , wanajaribu kuwashawishi watu haswa vijana wakapime wajue afya yao ili wawe na mipango mema ya maisha yao hapo mbeleni , nimeona watu wachache sana wamejitokeza kupima au kuangaliwa afya zao .

Wengi wameenda katika tamasha kwa sababu raisi amesema kitu , raisi alipomaliza hutuba watu wanatoka nje na kufunga masikio yao , na kuanza kuonyesha tamaa zao bila kuogopa na kujiamini , na wengine pale pale uwanjani wametamani wasichana warembo wameamua kuondoka nao

Naamini kabisa katika matamasha kama yale lazima kutakuwa na wasichana au waneume warembo ambao wamekuja kuuza sura zao pale , wanapenda kuitwa kuongea nao , baadaye uende nae hoteli au mghahawa kumnunulia chochote na muanze mambo ya ngono .

Ukienda kule katika vilabu vya usiku au hata bar hizi za mitaani , kuna wanawake wanajiuza mule haswa vijana watoto wabishi kabisa masikini wa mungu , hawa vijana maisha magumu wameamua kujitoa mhanga wauze miili yao ili waweze kupata chochote

Je kama wanaharakati wa ukimwi wakaongea na wenye bar waanze kuwaelimisha kuhusu ukimwi hawa wakina dadapoa na kakapoa wanaojiuza usiku itakuwa taabu au gharama kubwa ? sidhani kwa sababu hawa ndio chachu ya kusambaza UKIMWI mahala popote haswa kwa watu walevi .

Wakati fulani nilitembelea bar moja inaitwa KILITIME shekilango , bar hii siku hizi inawatu wachache sana , uchache ule usifikiri wale wameenda bar ? la hasha wengi wanasubiri watoto wadogo wanaokuja kujiuza mule bar , hawa watoto wadogo wanatolewa mikoani kwa minajili ya kuja kusomeshwa au kufanya kazi mjini

Wakifika mjini waajiri wao wanawafungia ndani na kuwafungulia usiku kwenda katika bar kama KILITIME kwa ajili ya kuuza miili yao kisha pesa wanampa yule mwajiri ndio maana pale KILITIME jiulize mbona kuna mimama imekaa pembeni inafanya nini ? ILE MIMAMA NDIO MABOSI WA WATOTO WALE

Ina maana wanaharakati wa ukimwi hawajui kwamba kuna watoto wanatolewa mikoani kuja kufanyishwa umalaya mjini haswa katika kumbi za starehe bila ya wazazi wao kujua au kuwa na taarifa kuhusu wanao ? je kule nyumbani wanakotoka hawafuatiliwi hata na wazee wa nyumba kumi kumi au wamitaa kujua watoto wao wanafanya nini mijini ?

Ungejengwa utaratibu maalumu wa njia za kuchukuwa wafanyakazi wa ndani toka mikoani , mfano mtu anaenda kuchukuwa msichana wa kazi anaacha picha moja kwa mwenyekiti wa mtaa na kwa wazazi wa mtoto , anaacha kopy ya kitambulisho chake na taarifa zake zingine za msingi

Halafu wawe wanafuatilia mara kwa mara kujua mtoto wao anaendeleaji kama huyu mtu akimfanyisha mtoto umalaya basi atashugulikiwa kisheria kwa sababu watakuwa wanamjua kutokana na taarifa alizoleta hapo mwanzo .
Wafanyakazi wa ndani wote watambuliwe kama wafanyakazi halali , mishahara yao iwe mizuri ili wasipate vishawishi vya kutegewa watoke nje ya nyumba kwa uraisi wawe na chama chao ambacho kitawawakilisha katika malalamiko yao .

Mwaka 2003 nilitembelea kijijini moshi vijijini , kwenda kusalimia ndugu jamaa na marafiki , nilitegemea kukutana na wale vijana ambao nimekuwa nao toka enzi hizo , badala yake nilikuta wengi wao wagonjwa , wengine wameondoka hawajulikani walipo , wamebaki wazee wanaotunza watoto wao ambao ni wagonjwa .

Nilipodadisi nikaambiwa wengi wao ni waathirika , wengine wanakuwa na mke hapo kijijini na mwanamke mjini , anapatwa maradhi , akizidiwa anakuja kijijini anakuja kumpa mke wake bila mke kujua au na pengine yeye hajui si hajapima ? huyu kijana akirudi mjini mke wake huku kijijini anakuwa mpweke hawezi kuvumilia mpaka mwezi wa 12 kwahiyo na yeye wakati Fulani anatembea na vijana wa kijiji ANASAMBAZA .

Kwa sababu kijiji ni mbali kidogo na mjini na nauli ni bei ghali , vitu kama kinga haviji kijijini na kama vikija ni bei ghali kutokana na usafiri , hata vikiwa bei rahisi vijana hawana elimu ya kutosha ya matumizi ya hizi zana wanakosea kuvaa , wengine wanatumia kinga zaidi ya mara moja au zaidi

Hizi ni changamoto chache ambazo wanaharakati za ukimwi na ulezi wanapaswa wapambanue na kuweza kupambana nazo kuandaa matamasha haisaidii kwa sababu wanaoweza kuja katika matamasha ni wachache sana , wengi ni wenye uwezo walioadhirika zaidi wako vijijini wengine hawajui kusoma wala kuandika ukibandika tangazo pale ataona ni urembo tu hana cha kufanya .

Tumekuwa katika vita hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa na tunaona watu wanazidi kushambuliwa na ukimwi , tunazidi kupoteza maisha ya vijana wetu ambao tumewasomesha kwa gharama kubwa na kuzidi kukata tama wengine wanasema heri wafe na ukimwi kuliko kuteseka na hali ngumu ya maisha hapa duniani


Basi kuna uhumimu kwa wanaharakati wa ukimwi kuwa karibu zaidi na wanachi na waathirika zaidi wapange mipango endelevu ya kupambana na ugonjwa huu , kama adui anakushinda ni wajibu kubadili mbinu na njia mbadala za kupambana nae na ndio inachotakiwa kwa ukimwi

UKIMWI UPO UTAENDELEA KUWEPO LAKINI TUNAWEZA KUUPUNGUZA KWA KUKUBALI UKWELI NA KUBADILI NJIA ZA KUPAMBANA NA UGONJWA HUU , NI WATU KUWA WAWAZI NA KUSHIRIKIANA KWA HAKI KATIKA UTENDAJI KAZI WAO NA KUELIMISHA JAMII

VITA INAENDELEA
 
Na Yona F Maro

Sio kila muathirika wa UKIMWI ni mzinzi , muhini au alipata ugonjwa huo kwa njia ya ngono au njia zingine zinazohusiana na zinaa au uzinzi , sio kwamba kila mgonjwa wa ukimwi ametaka kupata ugonjwa huu au alitegemea kupata ugonjwa huu , Lakini ni ukweli usiofichika wengi wa waathirika walijua au walikuwa na uelewa kidogo wa janga lili na mengine yanayoendelea .

HADITHI FUPI

Jana usiku nilitembelea bar moja mwananyamala inaitwa MK , nilikaa chini karibu na kituo cha basi nikawa namsubiri rafiki yangu Fulani , pembeni yangu alikuwa dada mmoja mrefu amekaa na mwanaume mmoja , wanakunywa wanapigana mabusu na kadhalika

Yule msichana akatoka pale kwenda juu , na mimi nilitoka kwenda msalani ufika huko juu nikakuta yule msichana ameingia choo cha wanaume na mwanaume mwingine wanafanya ngono ya chap chap huku yule mwanaume mwingine ameachwa chini pale na bia yake kaambiwa amekuja msalani .

Nilipotoka pale nikakutana na rafiki yangu mwingine hapo hapo juu , ghafla yule msichana akaitwa na mwanaume mwingine kule kule juu , akakaa nae akaagiza kinywaji kisha akamwambia yule mwanaume kwamba amepata simu ya dharura anarudi nyumbani kwake kidogo atarudi

Kumbe harudi nyumbani anarudi chini kwa yule kidume wake aliyemwacha pale , akaa kidogo pale akavamia jukwaa la kusakata rhumba akaanza kusakata rhumba pale na vijana wenzake huku maisha yanaendelea wakaanza kupenda namba za simu pale pale .

Sikujua kama wale wavulana wanajuana au hawajuani au yule msichana ni changudoa anajiuza au hajiuzi lakini alichokuwa anafanya hakikubaliki hata kidogo na kuvunja maadili kwa kiasi kikubwa .

MAISHA YA NGONO

Kijana mdogo yuko zake secondary labda form 2 hivi , anaanza mahusiano ya kimapenzi na mtu , akifika form 4 labda yuko na mpenzi mwingine halafu tuseme huyu kijana sio mwaminifu kwa mpenzi wake ni mtu mwenye tamaa za kimaisha na kadhalika , akimaliza form 4 anaenda A Level ambako anakuwa mbali na mpenzi wake huko alipo anapata mpenzi mwingine , kama ni sehemu mbali sana hawezi kuwasiliana na wazazi wake kama anashida mbali mbali , basi anaweza kupata wapenzi wengine wa kusaidia mambo yake ya kimaisha na kimasomo .

Huyu kijana wakati wa likizo anarudi nyumbani anakutana na yule mpenzi wake wa nyumbani wanafanya mapenzi na kufurahia maisha yao ya mapenzi , kijana kamaliza ALEVEL anaingia chuoni huko nako anakutana na changamoto kibao za kimaisha na anakutana na vishawishi kibao na anakubaliana na vishawishi hivyo anaingia mtegoni napo anafanya mapenzi na anasa zingine .

Akimaliza chuo anatafuta kazi , mtu aliyempatia kazi alimwomba rushwa ya ngono anatoa ngono , kule kazini kidogo anakuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi wake au wafanyakazi wenzake mbali mbali , bado mpenzi wake anaye .

Kijana huyu anaamua kuingia katika ndoa , wanaishi lakini ghafla wanaaanza kumuumwa na kusumbuliwa na maradhi , kupimwa wanakutwa na UKIMWI , sasa kivumbi kinaanza kumtafuta mchawi ni nani .

Kama unavyoona hapo kijana ameanza mapenzi siku nyingi sana na amekuwa na wapenzi mbali mbali wakati wote huo alikuwa hapimi kuangalia afya yake mpaka alipoingia katika ndoa ndio anapima kujua afya yake tena baada ya kuonekana afya yake iko shakani

Kwahiyo vijana wengi na watu wengi wanaishi na virusi kwa zaidi ya miaka 10 au 5 bila wao kujitambua kama wanaukimwi na kama afya zao ziko salama ili waweze kupanga maisha yao mazuri ya mbeleni , hali inazidi kutisha sana .

KUANGALIA AFYA

Wengi hatuna mazoea ya kupima afya zetu kwa ujumla , mfano mimi nina ratiba ya kuangalia afya yangu kila miezi 2 , hiyo imeshawekwa katika ratiba yangu ya maisha yangu siku zote , kwa jumla ya miaka zaidi ya 10 mfululizo sijawahi kusumbuliwa na ugonjwa wowote zaidi ya mafua ambao ni ugonjwa wangu sugu vyengine siumwi .

Kijana yuko katika mahusiano na mtu hataki kujua afya ya mwenzake , sasa najiuliza kama wanapenda kuishi wote kwa miaka 30 ijayo kwanini usijue afya ya mwenzako kwa faida zako wewe ? siku yoyote anaweza kusumbuliwa na hiyo afya yake kama humjui au kama ulikuwa hauna taarifa si ndio unaanza kuona mzigo kumbeba mwenzako na ndio mnakimbiana ?

Kupima afya iwe ni wajibu wa kila mtu haswa vijana ambao taifa linawategemea kwa ajili ya shuguli zaidi sasa hivi na hata siku zijazo , kama vijana hawataki kupima afya zao , taifa haliwezi kujua na halitamudu kuwahudumia vijana wote walioadhirika kwa sababu ya takwimu ndogo au za uwongo walizokuwa nazo .

UKIMWI SIO MWISHO WA MAISHA

Kama unaenda kupima ukajua umeathirika ongea na mpenzi wako nae ajue kuhusu kilichokusimu , uwe wazi kwa mpenzi wako kuhusu mambo haya , wengi hawataki kusema na badala yake wanavunja ndoa au mahusiano na kwenda kuanza maisha mengine na wapenzi au wanandoa wapya

Wengine wanafikia hata hatua ya kwenda makanisani kubadilisha dhehebu na kuokoka , nimeona makanisa mengi ya kilokole siku hizi yamevamiwa na watu waliokata tamaa wameathirika wanaenda kutumia kioo cha ulokole kujisafisha huku wanaendelea na dhambi zao kwa kasi ile ile

Niliwahi kwenda katika msiba mmoja , huyu kijana alikuwa mwathirika , alipoona anakaribia kufa akaamua kwenda kuokoka na kufuta uvumi mitaani kwamba jamaa alikuwa yuko safarini na alikuwa mbeba silaha za maangamizi , kweli mchungaji akampokea yeye mchungaji si anataka sadaka tu ? hataki zaidi ukitoa sadaka wanafanya sala na kukupa huduma zote

Huyu kijana akafariki baada ya wiki 3 hivi , katika mazishi yake mchungaji akamsifia kijana yule kwamba alikuwa kijana mwerevu , mfanyakazi hodari na msikivu , lakini mungu amemchukuwa ghafla kwa ugonjwa wa malaria tunasikitika sana lakini nasi tunaenda huko huko , wote tutaitwa na muumba kwenda kwa njia kama ile tuliyojia nayo

Mchungaji akamaliza kwa hutuba yake , na hapo vijana waliokuwa pembeni wanasikiliza wakaingiwa na ushawishi kwa kwenda nao kujificha makanisani walivyojua wameadhirika , na ni kweli makanisani siku hizi wamejaa wazinzi , waasherati kuliko kipindi chochote cha maisha watu wanatumia makanisa na ulokole wao kuuhadaa ulimwengu .

MSIMAMO WA MAISHA

Wakati Fulani nikiwa secondary mwalimu wangu alifundisha somo Fulani la kujitambua , anasema kijana lazima ujue kwanini umezaliwa , kwanini uko hapo ulipo sasa hivi , unatakiwa ufanye nini kwa maisha yako na wengine wanaokuzunguka na mwisho wa siku ufanye nini kuwa na msingi bora wa maisha yako ya mbeleni .

Kama hauna msimamo wa kujua wewe ni nani na majukumu yako katika dunia hii , pia huwezi kuwa na msimamo wa maisha ya kimapenzi na uhusiano na mpenzi wako , katika kutumia kinga au zana wakati wa kufanya vitendo vya ndoa incase ukitakiwa kufanya hivyo .

Kuna tatizo lingine la vijana wengi kutokuwa na msimamo kuhusu maisha yao yote kuanzia ya kimapenzi na mambo mengine , katika hili siwezi kumshambulia kijana peke yake , tuangalie wazazi wao wanafanya nini au walifanya nini kuhakikisha kijana wao anakuwa mtu mwema na kumweka katika maadili yanayofaa ili kukabiliana na maisha huko mbeleni anapoenda .

Baba yetu alikuwa na mazoea ya kutuita mimi na ndugu zangu wengine kuongea na sisi kila baada ya mwezi mmoja , kuuliza unafanya nini , una mipango gani na kama umeshindwa kitu ni kitu gani umeshindwa , na je kama unataka msaada kutoka kwake wa aina yoyote ile .

Siku moja baba yangu aliniita mbele ya wadogo zangu wengine na baadhi ya ndugu zangu wengine , akanipeleka sehemu Fulani hivi , kumbe alikuwa ameninunulia nyumba ya kuishi eneo hilo , wakati huo sikuwa tayari kwa zawadi za nyumba kwa sababu kuna majukumu mengine nilikuwa natekeleza nisingeweza kuilinda ile nyumba .

Ile nyumba nikaikataa akapewa mdogo wangu mwingine huyu akaikubali bila kufuata ushauri wa rafiki zake na jamaa zetu wa karibu , matokeo yake akaiuza ile nyumba akanunua magari , akaapenda anasa nyingi magari yale yalipata ajari , wasichana aliokuwa nao wakamkimbia akaamua kurudi nyumbani kuomba msamaha aendelee na masomo .

Nilikataa ile zawadi kwa sababu nilijua nisingeweza kuitunza kutokana na majukumu mengine niliyokuwa nayo wakati huo , kwahiyo nilionyesha msimamo wangu hapo na sikuona umuhimu wa kupewa nyumba wakati nilikuwa ndio naanza maisha nilitakiwa kufanya kazi nipate pesa nizalishe na mimi niwe na yangu sio nyumba za zawadi .

Baba yangu ni kati ya wazazi wachache wanaojali sana familia yake na watu wake wa karibu katika mambo yake popote anapoenda na kutembelea , wazazi wengi wanatakiwa wawajengee watoto wao uwezo wa kuwa wawekezaji wazuri na wazalishaji wazuri katika stali zao za maisha .

Kama mtu ukilelewa vyema ukawa na msimamo wake wa maisha hautaweza kuhujumiwa katika mambo mengi tu hapa duniani moja wapo ni hilo la vishawishi vya anasa mbali mbali katika maeneo unayotembelea .

CHANGAMOTO KWA VIJANA

Tunajua kwamba ukimwi upo na utaendea kuwepo hatuna budi kuwa na misimamo yetu haswa ya kujua afya zetu kwa njia ya kupiima ili tuweze kuwa wema na wenye malengo na maisha yetu ya baadaye , ukishapima na kujua majibu yako lazima utakuwa na msimamo Fulani katika maisha yako , lazima utakuwa na mabadiliko Fulani katika maisha na mwenendo wako

Lakini mwisho wa siku suala la ukimwi ni binafsi sana , huwezi kwenda kuongea na kumuelimisha mtu kuhusu UKIMWI kama yeye mwenyewe hajaamua kujielewa na kujitambua majukumu yake katika jamii inayomzunguka .

Nawapa pole wale wote waliadhirika na ugonjwa huu popote walipo lakini wawe na matumaini na maisha mema hapo mbeleni , siwezi kuwalaumu au kuwaponda sio wote wamepata ukimwi kwa kujitakia , wengine wameambukizwa na wapenzi wao wasio waaminifu , wengine bahati mbaya mahospitalini au katika ajali zingine makazini au sehemu wanazotembelea

Wengine ni kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huu .
 
Nafikiri Nondo yupo Right maaana Kama swali lilivyosema hawataki unafiki mimi naona kaelezea sawa as long as nahakika hamna wana JF under 18 humu ukisema utumie Tafsida ndio unarudi pale pale kwenye Uoga na Unafiki safi kuwa wazi ndio maana ya Forum.
 
Kwa mwamko nilioupata kutokana na Uzinduzi wa KAMPENI ZA KUPIMA UKIMWI naona niweke na kusaidiwa mawazo bayana;

Nimekaa nikafikiri nipo njia ya panda tatizo langu mimi linakuja Uhakika wa kwamba Ukivaa Kondom kweli Hupati Ukimwi? Na kuna research yeyote ilishafanyika ikaonesha ya kwamba Kondom imewakinga watu kupata Ukimwi au ndio watu wanapata mgongo wa kuanzisha NGO's?

Pili naomba kujua UKIMWI NI UGONJWA AU NI UPUNGUFU WA KINGA HALAFU NDIO MAGONJWA YANAFUATA?

Tatu, Je ni busara kupima Ukimwi? Na kama ni busara kuna msaada wowote ambao wahusika wanatoa baada ya kugundulika kwamba Umeathirika hasa kwenye suala la Lishe na sio Ushauri nasaha?


Nne, kwa mujibu wa watu ambao wameathirika wanasema madawa ya kurefusha maisha yanamadhara kama Ganzi za Miguu je wahusika wamejaribu kuliangalia hili?

Mwisho je wana JF tumeshakwenda Kupima kujua Afya zetu?

Hapo naomba msaada wenu waungwana maana tusiwe tukawa tunapaka Rangi Upepo halafu hatuji tunakokwenda.
 
Pinokyo! Swali halijibu swali mkubwa wangu! Jiachie tuu we sema kama umepima au ndio umekimbia Majibu.
 
Tafiti Mbalimbali zimeonesha kondomu zinasaidia kupunguza maambukizi ya ukimwi, nadhani hata kwa common sense utagundua hilo ni kweli; Lakini tilia maanani KUPUNGUZA!
Kuhusu UKIMWI = ni Upungufu wa Kinga Mwilini, Ni hali inayojitokeza baada ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI kuwepo mwilini kwa muda mrefu na kuharibu kinga ya mwili. Kumbuka vitu viwili; HIV - ambacho ndo kirusi kinashambulia immune system na kusababisha AIDS ambao ndio UKIMWI.
Kupima ni vizuri, JK asema kujua tatizo ni mwanzo wa kupata jawabu, kwa unajipanga kujilinda usiambukizwe ama kupanga uboreshe vipi maisha ukiwa nao;
Dawa zipo tena za bure kwa sasa, unachofanya ni kuji-register tu kwenye clinics zaitwa CTC ambazo ni kwa msaada wa mashirika mbalimbali hasa PEPFAR, mfano kupitia ICAP (columbia university), MDH (Harvard University), EGPAF na kadhalika.
Miguu kupooza, ganzi na kadhalika vyaweza kuwa ni side effects za dawa, lakini UKIMWI per se unasababisha ganzi na miguu kuuma vilevile, inaitwa HIV- polyneuropathy, kwani hivi virus pia vyaathiri mishipa ya fahamu; cha muhimu ukishaji-register jamaa wanakupa dawa na kukufanyia monitoring monthly kwa hiyo mtakuwa mnaona dawa zipi zinakufaa na symptoms zipi zitibiwe vipi! Au sio!
Tukapime wana JF.
Asanteni.
 
Wabunge wametaka Sheria ya Kazi na Ajira kuangaliwa upya, hususan suala la uhamisho wa kazi kwa watumishi wake, kwa kuwa linaongeza wimbi la nyumba ndogo pamoja na maambukizi ya Ukimwi.

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/07/31/95477.html

Ndani ya hiyo link jambo kuu lilozungumziwa ni rushwa! pengine wameoanisha uhamisho vs nyumba ndogo vs rushwa wakapata jibu la tatizo la msingi la watanzania.
Mambo yanozungumzwa na wabunge wetu huko bungeni mengine yaleta raha kweli; nyumba ndogo zasababishwa na uhamisho! watuambie wale wanoruka ukuta kwenda nyumba ya pili kama mwenye mali huwa kahamishwa!

NB Nimeiweka katika siasa kwasababu yatoka bungeni kunakojadiliwa mamby ya siasa
 
Kawawa awataka wajumbe NEC-CCM kupima Ukimwi
Mwandishi Maalumu, Dodoma
HabariLeo; Wednesday,August 01, 2007 @00:02

MZEE Rashidi Mfaume Kawawa amewataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kujitokeza na kupima kwa hiari virusi vya Ukimwi.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa NEC ulioanza jana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema Mwenyekiti wao, Rais Kikwete ameonyesha uongozi wa mfano kwa yeye na familia yake kujitokeza na kupima virusi kwa hiari na mbele ya hadhara, hivyo nao hawana budi kumuunga mkono kwa vitendo.

“Mwenyekiti wetu ameonyesha uongozi wa mfano, amejitokeza yeye na familia yake na kupima, amewahimiza wananchi kujitokeza na wanajitokeza kupima. Yeye mwenyewe ameonyesha mfano.

“Mimi nimefurahi kwa hiyo na sisi viongozi tumuunge mkono kwa kupima,” alisema Mzee Kawawa na kushangiliwa na wajumbe.

Mzee Kawawa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na kiongozi aliyeshika nyadhifa mbalimbali katika chama na serikali, aliwaeleza wajumbe hao kwamba yeye na familia yake wameitikia wito uliotolewa na Rais Kikwete wa kupima kwa hiari.

“Mimi mwenyewe na familia yangu tumeitikia wito wa Rais na tulikwenda kupima, sasa nasema wajumbe wenzangu wa NEC tufuate mfano huu kwa vitendo sote kabisa, sote kabisa tuuitikie wito huu kwa vitendo. Kwa wale ambao hawajapima tukapime na tuache visingizio,” alisisitiza.

Mzee Kawawa na familia yake walipima VVU katika Hospitali ya Kijitonyama Dar es Salaam, Julai 15 mwaka huu siku moja baada ya uzinduzi wa kitaifa wa kampeni ya upimaji kwa hiari.
Aliwaeleza wajumbe hao kwamba maneno aliyoyazungumza Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa hiari wa VVU Julai 14, viwanja vya Mnazi Mmoja yalikuwa ya hekima sana.

Katika hatua nyingine, wajumbe wa Kamati Kuu na NEC wamempongeza Mwenyekiti wao, Rais Kikwete kwa uongozi wa vitendo ambao yeye na Mama Salma Kikwete wamejitokeza na kupima VVU kwa hiari na kuwahamasisha wananchi.

Akipokea pongezi hizo za Mzee Kawawa na NEC, Rais Kikwete alimshukuru Mzee Kawawa na wajumbe wa CCM na NEC na kueleza kwamba, kampeni hiyo ya kitaifa aliyoizindua Julai 14 na kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa hiari kupima VVU, imepokelewa vizuri sana duniani kote.
 
Back
Top Bottom